Bodi ya mikopo na Makato mapya

Balungi

JF-Expert Member
May 25, 2011
234
162
Naomba kujuzwa na wadau wa elimu na sheria, hivi katika mkataba na hii bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kubadili makato kama wanavyopenda wao hakuna namna ya kuungana tukawashtaki kwa kukiuka mkataba maana wengi tuliingia kwa kuvutiwa na makato ya 8%?? Au waliweka kipengele cha kubadili mkataba kwa namna wao watakavyoona? Nauliza hivi kwa vile mkataba wangu ulipotea kipindi nahama nyumba ya kupanga.
 
Blaza, wahanga tupo wengi sana. Mimi mshahara wangu jumla nakatwa 51%.

Cjui kama ni rahisi, kushindana na maamuzi ya RAISI
 
January hawajanikata 15%. Mi kwangu yote hewala. Wakinikata 15%, June namalizana nao HESLB. Wakiendelea kukata 8% December au January 2018 namalizana nao!
 
Tanzania ina wajinga wengi sana, tunashinda kulalamika mitandaoni tuu. NENDA MAHAKAMANI WEWE, KUWA KAMA MTIKILA (RIP).
Mi sina uwezo kipesa wa kufungua kesi peke yangu na si mwanasheria, ndo maana natafuta watu wenye nia tufungue shauri mahakamani
 
January nimechezea za uso wamekwala 15% walume ndago hawana mchezo,soon nawapelekea cheti changu cha kifo hakuna namna acha nijiue kwenye makaratasi kwanza niibukie upande mwingine.
 
Naomba kujuzwa na wadau wa elimu na sheria, hivi katika mkataba na hii bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kubadili makato kama wanavyopenda wao hakuna namna ya kuungana tukawashtaki kwa kukiuka mkataba maana wengi tuliingia kwa kuvutiwa na makato ya 8%?? Au waliweka kipengele cha kubadili mkataba kwa namna wao watakavyoona? Nauliza hivi kwa vile mkataba wangu ulipotea kipindi nahama nyumba ya kupanga.
Aiseh! Hizi baraka zilipitishwa na bunge letu hili!
 
Mkataba ni kila kitu hivyo wakitaka kuvunja mkataba wakae na wakopaji sio wabunge nje na hapo wadau tupo tayari kwenda kupinga mahakamani
 
Acha Maneno, Lipa MKOPO (in Darassa's voice). Ulikopa kusoma BA in Kiswahili what do you expect?
 
Back
Top Bottom