Bodi ya Mikopo inawaibia Watanzania

Hii kitu inaumiza sana

Unakatwa kwenye salary, makato hayapelekwei na hazina. Ukija kuenda deni limepaa. Ukiwaambia wanajifanya kustuka, wanarudishia makato yako na kutoa kwenye deni ulilonalo hivi sasa (Kila siku retention fee inapanda, yaani kila siku deni linakua ....hata Bank sio hivyo.). Yaani ni wizi tu

Mishahara ni ile ile, haijapanda tangu 2015 ila serikali imeongeza makato ya bodi kwa watumishi wake kutoka 8% hadi 15% halafu baada ya hapo wanataka tuwe wazalendo.

Bora ukope bank ulipe hili deni, ni nafuu sana
 
Tulishaongea humu kilichofanyika ni upuuzi mtupu, hakuna tofauti tena kati ya vyuo vikuu vya umma na binafsi. Haingii akilini kijana aliyesoma chuo kikuu cha umma kama UDSM, SUA, Mzumbe akatwe zaidi ya milioni 20 wakati lecturers na miundombinu mingine ya chuo inalipwa na serikali. Ideally, hawatakiwi kurudisha zaidi ya milioni tano na makato kwa mwezi yasizidi elf 20 maana ndo vijana wanakuwa wanaanza kazi mishahara inakuwa bado midogo. Acheni unyanyasaji huu kwenye elimu ya vijana wa kitanzania
 
Mkuu umenifumbua nlkuwa sieleew chochote
 
Hii ni bodi ya kunyonya watoto wa masikini
Watoto wanaingia mikataba ya kukatwa 8% lakini wakati wa kutekelezwa wanakatwa 15% bila upande wa pili kusikilizwa.
 
bado kuna ambao wamemaliza mikopo lkn kuna taarifa kuwa bado wanaendelea kudaiwa pamoja na kumaliza kwani bodi hawatoi clearence report na kufuta ktk system hivyo usumbufu kwa waliomaliza madeni.
 
Wee mpumbavu wa kusifia kila kitu hayakuhusu!
 
Kuna nchi nyingi sana zinasomesha vyuo vikuu bure.. kwanini isiwe Tanzania.
Bure ghali,zitaje hizo nchi
Halafu kukopeshwa pesa malipo mpaka upate kazi au biashara na kukosa kabisa ipi bora?
Acha hiyo 18% ikatwe,watoto wengi wanahitaji kusoma
 
Umenifungua macho. Ni kama kufunga ndoa na shetani! Lo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…