kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Nimeona orodha ya Taasisi sugu zinzodaiwa kutokupeleka majina ya waajiwa wao wanaodaiwa na bodi.Orodha ndogo niliyoiona ndiyo imenifanya nione hawa jamaa hawafikiri vizuri.
Kama wana sababu yoyote ya msingi wangeweza kuitafutia ufumbuzi mapema.Mfano iwapo wanakazi nyingi na wamezidiwa na kazi,wanashindwa nini kuwaomba wakuu wa wilaya wawasaidie kujua taasisi nyingi zilizomikoani zenye waajiriwa wanaodaiwa mikopo na hawajaanza kulipa?
mathalani zipo shule nyingi binafsi zenye waajiriwa wanaodaiwa mikopo,pia makampuni mfano wakandarasi wa ujenzi,hospitali za binafsi na mashirika ya dini,famasi zote Tanzania ni lazima ili zipewe kibali kuwe na mtu mwenye digrii anayedhamini na ziko zaidi ya 1000 tanzania nzima,baadhi ya NGOs zina waajiriwa wengi sana lakini sijaziona katika orodha na taasisi moja ninayofanya kazi wapo zaidi ya kumi na hawana mpango wa kulipa wala mwajiri hana mpango wa kupeleka majina.
Maoni yangu ni kwamba kama mmeshindwa kazi na mmeshindwa kuwa wabunifu,kwa nini msitumbuliwe wapewe kazi watu wengine ili walipe vizuri madeni yao?