Siyo mikopo yote ya Serikali ni mibaya

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Nashangazwa sana na watu ambao wana lalama kila siku kuhusu mikopo ya serikali bila kuelewa aina ya mikopo hiyo.

Inasikitisha Watanzania tuna uvivu sana wa kufuatilia mambo badala yake tunapinga na kushabikia vitu bila kujua.

Nilishangaa kuna watu walishangilia Magufuli kukopa mkopo mbaya wa $1.5B kwa asilimia 8% miaka 6 kutoka kwa Exim bank halafu watu hao hao wanampinga Raisi Samia kwa kukopa $1.3B kwa asilimia 3% kwa miaka 20.

Sasa kuna mawili kwanza inawezekana watu hawaelewi wanapinga nini au kushangilia nini au wanasubiri serikali ndiyo iwalishe maneno! Nakumbuka wakati wa Magufuli hata kuongelea hili waliona kama ni uchochezi!

Mfano huo hapo Juu Mkopo wa Raisi samia ni $87,380,420 kwa mwaka au Tsh Billion 200,974,966 kwa (Exachange rate ya $1-Tsh 2300 wakati wa magufuli ni $324,473,079. kwa mwaka au Tsh 746,288,082,490 kwa miaka 6.

Pamoja na kwamba mkopo wa Magu ni wa muda mfupi bado ni pesa nyingi sana ambayo itazuia pesa za uwekezaji ambazo ni muhimu kukuza uchumi. Uchumi wetu unataka uwekezaji zaidi hasa kwenye miundo mbinu hivyo sio vizuri kutumia pesa zote au nyingi kwenye miradi ambayo haiongezi kipato. Tunahitaji kuongeza kilimo, utalii, viwanda.

Tuchukuwe muda kujua mikopo kabla ya kupinga au kushangilia mikopo ya nchi.

Nilisha shauri mbinu za kurekebisha mikopo

Napenda nitoe mawazo yangu kwenye mikopo ya serikali. Nitaelezea kwa mtiririko wa utekelezaji ili niwasaidie Serikali badala ya kulalamika na kupigiana madongo
  • Mikopo yote ya serikali bila kujali awamu iangaliwe kwa kujua muda wa kulipa mikopo na riba za mikopo.
  • Group 1: Mikopo yote yenye riba ndogo na miaka mingi ya kulipa. Hii ndiyo mikopo mizuri. Mfano kama una mkopo wa 5% kwa miaka 20 huu ni mkopo mzuri.
  • Group 2. Mikopo ya pili ni mikopo yenye riba ndogo lakini muda mfupi. Hii nayo ni mizuri lakini muda ndiyo tatizo.
  • Group 3. Mikopo yanye riba ya juu ambayo ni zaidi ya 10% lakini muda mfupi. Hapa tatizo kubwa ni riba na huu ni mkopo mbaya.
  • Group 4. Mikopo yenye riba ya juu zaidi ya 10% na ya muda mrefu. Hii ndiyo mikopo mibaya kuliko yote.
Serikali fanyeni hizi;
  • Mikopo Group 3 fanyeni mpango kama mnaweza kujadili malipo kwa njia ya refinance. Hii ni kama kutafuta wawekezaji/bank ambayo inaweza kulipa hili deni na kukupa muda zaidi wa kulipa na riba nafuu. Inavyotokea ni kwamba hii bank au watoa mikopo wanalipa mkopo wote na lile deni linakuwa mkopo mpya nafuu na wa muda mrefu. Kama ni mkopo wa serikali chukueni hii mikopo na mpeni Raisi aweze kuongea na hiyo serikali husika. Wizara inatakiwa kumpa Raisi kitu ambacho kimekamilika ili akaongee nao. Mfano kama ni mkopo wa serikali ya Japan raisi anaweza kuongea na waziri mkuu wa Japan lakini ni lazima kwanza wizara ifanye kazi yake na kuwa na data zote za mikopo kwbla ya kupeleka kwa Raisi. Tatizo hakuna ubunifu na watendaji wa wizara wanabaki tu na utekelezaji badala ya kuwa wabunifu
  • Mikopo Group 4. Hii mikopo yote inabili kila mmoja uangaliwe upya na kutafuta njia zote za ku refinance. Hii ni kutafuta mkopo wa nafuu wa kulipa huu mkopo mbaya halafu mkopo mpya unakuwa wa muda mrefu zaidi na riba ya chini. Kama ni mikopo ya nchi muhusisheni Raisi!
HAKUNA MKOPO MZURI KWA SERIKALI WA MIAKA MITANO
  • Nimesikitiswa sana na wale wasomi wanao jaribu kuaminisha Watanzania kwamba kuna mikopo ya bank za biashara mizuri kwa serikali. Mikopo yenyewe mingi ni ya miaka 5 na riba zinakuwa 8%~10%. Hii mikopo sio mizuri kwa serikali hasa ukizingatia uwezo wetu. Serikali kwa ushauri wangu.

    1. Wasikope chini ya miaka 10.
    2. Riba ya mkopo isizidi ukuaji wa uchumi mfano Tanzania ukuaji wa uchumi ni 5%~ 7% hivyo riba iwe hapo katikati . Kama mkopo ni kwa dollar isizidi 5% kwasababu mfumuko wa bei wetu unakuaga 2% zaidi ya USA.

    Mwigulu acha mikopo ya riba ya juu na muda mfupi hii inaongeza payment amount za mwezi na mwaka na kusababisha pesa nyingi kwenda kwenye mikopo.

What Is a Refinance?​

A refinance, or "refi" for short, refers to the process of revising and replacing the terms of an existing credit agreement, usually as it relates to a loan or mortgage. When a business or an individual decides to refinance a credit obligation, they effectively seek to make favorable changes to their interest rate, payment schedule, and/or other terms outlined in their contract. If approved, the borrower gets a new contract that takes the place of the original agreement.

Borrowers often choose to refinance when the interest-rate environment changes substantially, causing potential savings on debt payments from a new agreement.

Mwigulu Nchemba

Niongezee hili serikali mikopo ni mizuri kama inatumika vizuri. Mikopo inatakiwa kutumika kwenye miradi ya kuongeza kipato na sio kutumika kujikimu na kulipa mishahara ya wafanyakazi. Hivyo wekezeni kwenye sehemu kuwawezesha wafanyabiashara kujenga viwanda na wakima kuongeza uzalishaji na sio kutumia pesa za mikopo kwa ruzuku au mishahara.
 
Taifa letu ni taifa masikini hivyo kukopa ni jambo lisilo epukika mkuu hili Watanzania wote inabidi walitambua wazi kabisa.

Mleta uzi hakuna anayepinga serikali kukopa hilo na wewe litambue wazi sio kuleta lawama tu watu wanacho uliza hizo pesa za mikopo zinazo chukuliwa kila uchweo zinakwenda kufanya shughuli gani hili swali hata waziri kashindwa kujibu Kama una majibu tupe.

"Katiba mpya ni takwa la umma"
 
mikopo ni mizuri kama inatumika vizuri. Mikopo inatakiwa kutumika kwenye miradi ya kuongeza kipato na sio kutumika kujikimu na kulipa mishahara ya wafanyakazi.
Kamundu, maelezo yako yote kuhusu mikopo na faida zake ni sawa kabisa ila kwa serikali yetu tatizo liko hapo kwenye hicho kipengele.
 
Taifa letu ni taifa masikini hivyo kukopa ni jambo lisilo epukika mkuu hili Watanzania wote inabidi walitambua wazi kabisa.

Mleta uzi hakuna anayepinga serikali kukopa hilo na wewe litambue wazi sio kuleta lawama tu watu wanacho uliza hizo pesa za mikopo zinazo chukuliwa kila uchweo zinakwenda kufanya shughuli gani hili swali hata waziri kashindwa kujibu Kama una majibu tupe.

"Katiba mpya ni takwa la umma"
Tunahitaji kuwa na mifumo wazi itayotuambia kila senti inayokopwa inaenda wapi na huko ilipoenda imetumika kama ilivyokusudiwa.

Hofu yetu ni kulipa deni ambalo walinufaika wachache
 
Back
Top Bottom