Bodi ya Mikopo haina majina ya waliochukua mikopo

Bodi ya Mikopo haina majina ya waliochukua mikopo

Tunaomba hiyo link yenye orodha ya majina ilishawahi tolewa hapa nyuma.
 
Kama kuna mbunge yupo makini basi akipeleka hoja binafsi kuhusu suala hili atapata ujiko kweli...Mimi nina hakika hawa jamaa majina hawana au yalipotezwa kwa makusudi ili kuficha uovu.Mbona TRA kila siku wanatoa majina ya wadaiwa sugu kwa nini Bodi ya Mikopo isifanye hivyo.
 
Insemekana bodi ya mikopo imepoteza baadhi ya majina ya walio faidika na mikopo. Ndio maana inahaha na kutoa vitisho watu wajipeleke au waajiri wapeleke majina.

Ukijipeleka basi ndio wanaanzia hapo kujua unatakiwa kulipa kiasi gani. Kama wanayo wangekua wamesha Tangaza majina.
watangaze zawadi nono tuwapelekee majina ya wanaodaiwa bodi,watu wanajitamba maofisini wengi tu hawalipi mikopo ile
 
Kama umekopa mkopo mwingine 1/3 ya mshahara inatakiwa kubaki.Sasa kuna majamaa tumeajiriwa wote hawajaanza kuwakata kwa kuwa fomula iligoma(labda walipe private cash in hand) wakati mimi kama mwaka sasa wanakula chao.
 
Ila ni vyema ukarejesha ili na wengine wafaidike kama ulivyofaidika wewe
 
Warudishe kwanza pesa za Escrow, EPA na mimi ndo nitalipa mkopo wangu walionipa. Mimi milioni 10 tuu wananikereketa hivi, wakati EPA watu wamesepa na mabilion ya pesa hawashughulikiwi.

Yaani kiufupi hii pesa waliyonisomesha nayo bodi ni mgawo wangu katika madili yote machafu yaliyopigwa nchi hii. Na silipi Ng'oooooooo
 
mi nimeshawalipa kwa kodi nayokatwa kwenye mshahara wangu...

yaani pesa ya mlipa kodi useme unamdai.. shenz kabisa na siwalipi hata iweje
 
Inakuaje Mwananchi akopeshwe Kodi yake? Kanuni ipi waliitumia kufanya tuliosoma 1993 kwenda nyuma iwe bure halafu watoto/ Wadogo wetu kuanzia 1994 kuja mbele wakopeshwe. Ubaguzi wa Umri ni mbaya kama wa dini na UKABILA.
Tena waliosoma bure kabla ya mwaka 93 ndio wenye mpunga na mishahara mikubwa.
 
huwa naiamini sana JF kwa kupaza sauti za wananchi na zinavuma kila kona ya dunia hii mpaka walengwa inawafikia.sasa ngoja tuone majibu ya hiki kitendawili toka kwa wahusiku na watuwekee link yenye majina hapa...
wakikaa kimya ni kweli majina hawana ila wanasubiri HR na mtu kujisalimisha.
 
Lipa deni wadogo zako nao wasomeshwe. Kama tayari una ajira kwa nini usilipe?
 
Majina ya wadaiwa, vyuo na mwaka waliosomea, majina na anuani za wadhamini wao yawekwe kwenye website ya Bodi. Hii itawezesha waajili, wadhamini, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, TRA, Halimashauri za wilaya, Polisi, na vyombo vingine vya dola kuwakamata wahalifu hawa. Vinginevyo wahusika kwenye hiyo Bodi watumbuliwe. Hapa kazi tu, hakuna ujanjaujanja wa Bongo. Lazima kieleweke.
 
Sasa sie tunaolima toka tumegraduate watatupataje...kama tu tuliomba mtaji wakatunyima ambapo ingekuwa rahisi kutu monitor
utalimishwa kwa lazima ili kulipa deni!
 
Jipeleke utasulubiwa pekee yako wakati toka uhuru watu wanasoma bure. haa

Halafu wewe ndiye uliyekuwa mstari wa mbele kwenye msafara wa mgomo wa kudai mkopeshwe, ebu lipa hiyo pesa na watanzania wenzio wasomeshwe!
 
Kama ni kulipa tukipe wote toma mwaka 1961 baada ya uhuru
Kweli, woote twende, hadi wale waliokopa mabilioni ya JK. Mbona wao hawasumbuliwi? Au kwa vile walitukopesha sisi watoto wa wakulima ndo maana wanatukomalia? Na walioiba mali za umma nao waorodhoshwe waanze kurejesha. Hadi Polepole aliyeiba zile laki 6 za NGO nae arejeshe.
 
Back
Top Bottom