Bodi ya Mikopo haina majina ya waliochukua mikopo

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Insemekana bodi ya mikopo imepoteza baadhi ya majina ya walio faidika na mikopo. Ndio maana inahaha na kutoa vitisho watu wajipeleke au waajiri wapeleke majina.

Ukijipeleka basi ndio wanaanzia hapo kujua unatakiwa kulipa kiasi gani. Kama wanayo wangekua wamesha Tangaza majina.
 
we chelewa uje kulipa kwa asilimia ambazo haukukubaliana nazo ktk fomu uliyo jaza.

kuna mtu kaanza kukatwa baada ya miaka kama minne kazini....
 
Insemekana bodi ya mikopo imepoteza baadhi ya majina ya walio faidika na mikopo. Ndio maana inahaha na kutoa vitisho watu wajipeleke au waajiri wapeleke majina.

Ukijipeleka basi ndio wanaanzia hapo kujua unatakiwa kulipa kiasi gani. Kama wanayo wangekua wamesha Tangaza majina.

Wewe jidanganye tu!

Watu wamemaliza madeni yao, hatimaye wanapumua.

Mwenzetu unapima upepo hapa.....!

Pole.
 
Huenda uko sahihi....lakini sikushauri kukwepa kupeleka jina bodi...

Ni vyema ujisalimishe sasa...kuliko kusubiri wakuvamie ulipo na adhabu juu...

Usijione mjanja kukwepa bodi.....

usipokatwa Leo....kesho watakukata kwenye pensheni yako....

Tafakari chukua hatua.....
 
Kwani mwajiriwa anaanza kukatwa akiwa na miaka mingapi kazini au MTU anatikiwa aanze kurejesha mikopo yake baada ya muda gani baada ya masomo??
 
Insemekana bodi ya mikopo imepoteza baadhi ya majina ya walio faidika na mikopo. Ndio maana inahaha na kutoa vitisho watu wajipeleke au waajiri wapeleke majina.

Ukijipeleka basi ndio wanaanzia hapo kujua unatakiwa kulipa kiasi gani. Kama wanayo wangekua wamesha Tangaza majina.
Na pia ukienda wanakuuliza na Rafiki yako aliyekua anachukua mkopo
 
Waalimu peke yao maskoni ndo huwa wanalipa sisi kada nyingine hata hawajui kuwa tulishakufaga au tupo ki ukweli nina miaka mitano tangu nimalize na sijalipa chochote mimi pamoja na mama yenu mdogo!
 
Insemekana bodi ya mikopo imepoteza baadhi ya majina ya walio faidika na mikopo. Ndio maana inahaha na kutoa vitisho watu wajipeleke au waajiri wapeleke majina.

Ukijipeleka basi ndio wanaanzia hapo kujua unatakiwa kulipa kiasi gani. Kama wanayo wangekua wamesha Tangaza majina.
Umekopeshwa.... lipa deni suala la majina halikuhusu na mbaya zaidi una shauri na wengine eti wasilipe !? Defaulter wahed!!! Fikra hizi ni mbaya mdau kwanza hujui watu wangapi wataathirika na thread km hii mbaya zaidi huna data ni majina mangapi yamepote pili vyuo vyote vinavyopokea fungu toka Loan Board vina backup data za watu waliolipiwa na Board hiyo sasa hapo utakwepaje?...
 
Kama ni kulipa tukipe wote toma mwaka 1961 baada ya uhuru
 
Sasa sie tunaolima toka tumegraduate watatupataje...kama tu tuliomba mtaji wakatunyima ambapo ingekuwa rahisi kutu monitor
 
Inakuaje Mwananchi akopeshwe Kodi yake? Kanuni ipi waliitumia kufanya tuliosoma 1993 kwenda nyuma iwe bure halafu watoto/ Wadogo wetu kuanzia 1994 kuja mbele wakopeshwe. Ubaguzi wa Umri ni mbaya kama wa dini na UKABILA.
 
p { margin-bottom: 0.1in; line-height: 120%; }

Kupoteza majina ya wadaiwa is quet total imposible na haiwezekani na ni jipu / wahusika wa uhifadhi wa kumbukumbu wabanwe,hili haliwezekani hii ni dili posibly walirejista majina hewa na fedha zikawa zinaingia mifukoni mwao ili baadae wa-misplace doc's

cc/
jpm.
 
***
KUPOTEZA MAJINA YA WADAIWA IS QUET TOTAL IMPOSIBLE NA HAIWEZEKANI NA NI JIPU / WAHUSIKA WA UHIFADHI WA KUMBUKUMBU WABANWE,HILI HALIWEZEKANI HII NI DILI POSIBLY WALIREJISTA MAJINA HEWA NA FEDHA ZIKAWA ZINAINGIA MIFUKONI MWAO ILI BAADAE WA-MISPLACE DOC's /
Kweli mkuu!!!,mamlaka husika zichunguze na kuchukua hatua stahiki.
 
Mfano nimejiajiri mwenyewe.., kuna haja au ulazima wa kulipa hako kamkopo.., mi silipi wala nini.., mbona wa muhimbili hawalipi
 
Naamini kauli yako mtoa mada kuna dada nafanyanae taasisi ya uma amesoma nje kwa hela ya wazazi wake lakini anaambiwa anadaiwa na bodi nafkiri hawanatakwimu sahihi za walio wakopesha hasa miaka ile bodi ndo wanaanzatoa mikopo
 
Sidhani Kama Kuna Vijana Watajisalimisha Wakati Hawana Cha Kulipa, Watajiteteaje Sasa?
 
Kuna ukweli katika hoja ya mtoa mada. Japo Bodi walikuwa Na mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu lakini ulikuwa hautumiki baada ya wafanyakazi wengi kuanza kutumia karatasi kwa kufanya kazi zao.

Mwaka wa masomo 2005/2006 hapo ndipo mkanganyiko mkubwa ulipoanza ulipotokea. Nadhani kuna haja ya Serikali kuu kuliangalia hili.

Maana sasa Bodi inamkaba kila mtu mwenye degree alipe deni wakati wengine wamesoma kwa pesa za wazazi ama ndugu zao.
 
Back
Top Bottom