Bodaboda wavamia ofisi ya Serikali ya Mtaa Tabata, wamchukua mwizi wa Bodaboda watokomea naye kusikojulikana

Kijana mmoja maarufu kwa jina la Bonge mkazi wa Mtaa wa Kichangani, Tabata Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, hajulikani alipo baada ya kubebwa na baadhi ya waendesha Bodaboda kwa madai kuwa amehusika na wizi wa pikipiki usiku wa kuamkia leo Agosti 3, 2023.

Tukio la wizi lilivyokuwa
Dada mmoja ambaye hajatambulika alimchukua Bodaboda kutoka Kinyerezi Sokoni (Mnadani) majira tano usiku, ampeleke Kichangani Darajani.

Baada ya kushuka abiria akatoa Tsh. 10,000, wakati dereva wa Bodaboda anatafuta chenji, ndipo wakatokea watu wawili na kumshambulia, katika purukushani dereva akitaka kuchmoa funguo wakampiga na kitu kizito usoni na kisha kumtupa kwenye mtaro.

Baada ya muda dereva Bodaboda akaenda kuomba msaada nyumba ya jirani ambapo wakatoa taarifa kwa Mjumbe wa Mtaa kisha kupelekwa katika moja ya zahanati ya Kinyerezi.

Usiku huohuo taarifa zikaanza kusambaa juu ya kilichotokea, ndipo mtu mmoja akasema amemuona Bonge akiwa anakokota pikipiki.

Wavamia nyumbani kwa Bonge
Inadaiwa Bonge ni mwizi maarufu maeneo hayo na kutokana na rekodi yake ya nyuma vijana wengi wa Bodaboda walikuwa na kisasi naye na walikuwa wakisubiri ‘ajichanye’.

Wakiongozana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichanganyi,….. wakafika nyumbani kwa Bonge ambaye baada ya kubanwa akakiri kuiba pikipiki husika, akaenda kuonesha alipoificha, kisha akachukuliwa kwenda kuhifadhiwa katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa, akiwa pamoja na kijana ambaye alijeruhiwa na kuporwa pikipiki.

Bodaboda wavamia
Ilipofika alfajiri, kundi la Bodaboda zaidi ya 30 wakavamia ofisi hiyo wakimtaka mtuhumiwa kwa kuwa ni kawaida yake kufanya matukio na kuachiwa.

Nguvu iliyotumika ikawazidi nguvu viongozi wa Serikali za Mtaa, wakafanikiwa kumtoa Bonge na kutokemea naye kusikojulikana huku mashuhuda wakidai walielekea njia ya Gongo la Mboto.

UPDATES....
Mwenyekiti Serikali ya Mtaa ya Kichangani, Leonard Nyukuli alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema "Nipo nje ya ofisi, kama unataka taarifa zaidi njoo ofisini utapata taarifa rasmi ya kiofisi."

MWILI WA BONGE WAPATIKANA
Mwanafamilia wa marehemu (jina linahifadhiwa) amesema mwili ulipatikana maeneo ya Vingunguti, juzi (Agosti 3), Mama Bonge tumezungumza naye amesema alipopata taarifa za tukio akajua siku ya mwanaye imefika hata kabla ya kuupata mwili, ni kama alishajiandaa kisaikolojia kutokana na matukio ya nyuma.”

Naye, Mwenyekiti wa Kichangani, Leonard Nyukuli amesema "Wananchi waache kujichukulia Sheria mkononi, mtuhumiwa alitoa ushirikiano akaonesha pikipiki, kuna watu waliotoka sehemu nyingine ndio wakafanya hayo waliyofanya, tuliita Polisi hawakufika kwa muda muafaka ndio yakajitokeza hayo."
Hii ya Viongozi kusema eti Wananchi wasijichukulie sheria mkononi hua ni kama formality tu na msemo wa kisiasa.

Wao wenyewe huibiwaga na mdomoni anasema tusichukue sheria wakati moyoni anasema "piga na ua kabisa umbwa huyo". Hata wao hawataki kusumbuka ma kesi kila siku.
 
wamekosea kumuua wezi wa pikipiki ni chain ndefu, kuna mwizi na kuna anayezinunua na kuzichinja spea na duka zinakopelekwa.
Sasa yule mnunuaji atatafuta mchongo kwa wezi wingine wizi utaendelea
Kweli, hii angeungiwa chain wadosi wawili watatu mtaani, na kuvamiwa na nyomi ya bodaboda, hii biashara ingekoma au walau kupungua.
 
Mwizi ni haki yake kuuawa
Mwizi yupi,wa bodaboda ya mil.2 au hata wale wanaoiba mabilioni?maana hawa wanaoiba mabilioni sijawahi kusikia wananchi wamechukua sheria mikononi ila ni kwa hawa wezi wa kuku na viatu...
 
Tofauti iliyopo huyu mwizi wa bodaboda haiishii tu kuiba bodaboda ukicheza hata wewe atakutoa uhai, Hana chembe ya huruma kabisa hata kama hiyo bodaboda ataiuza 200k lakini Yuko tayari akutoe uhai aichukue
 
Watu wengi hawajui hilo.
Unataka Pikipiki ya 2m,mtu anakupiga na shoka au hata chuma kizito.
Wameua Vijana wengi sana ambao pia wana Familia.
2M ni ya kuua mtu kwa Shoka tena mapema tu jioni.
Boda boda wengi siku ni vijana wana Diplom na Degree,kuna baadhi ya vijiwe wapo Elite sana.Wanataratibu ngumu hat huku Maofisini hakuna.

Hii ni kulinda maisha yao.

Hata huko kwenye Bajaj,na ndio maana wana Intel zote za wizi na kila aina ya ushenzi.
Hizi zimekuwa kazi kama kazi zingine.Ikumbukwe kama Boda na Bajaji zisingekuwepo vijana wengi wangekuwa wezi na mtaani huku kungekuwa kugumu sana.

Japo baadhi yao pia wamekuwa wezi tokana hulka zao na tabia.
 
Kijana mmoja maarufu kwa jina la Bonge mkazi wa Mtaa wa Kichangani, Tabata Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, hajulikani alipo baada ya kubebwa na baadhi ya waendesha Bodaboda kwa madai kuwa amehusika na wizi wa pikipiki usiku wa kuamkia leo Agosti 3, 2023.

Tukio la wizi lilivyokuwa
Dada mmoja ambaye hajatambulika alimchukua Bodaboda kutoka Kinyerezi Sokoni (Mnadani) majira tano usiku, ampeleke Kichangani Darajani.

Baada ya kushuka abiria akatoa Tsh. 10,000, wakati dereva wa Bodaboda anatafuta chenji, ndipo wakatokea watu wawili na kumshambulia, katika purukushani dereva akitaka kuchmoa funguo wakampiga na kitu kizito usoni na kisha kumtupa kwenye mtaro.

Baada ya muda dereva Bodaboda akaenda kuomba msaada nyumba ya jirani ambapo wakatoa taarifa kwa Mjumbe wa Mtaa kisha kupelekwa katika moja ya zahanati ya Kinyerezi.

Usiku huohuo taarifa zikaanza kusambaa juu ya kilichotokea, ndipo mtu mmoja akasema amemuona Bonge akiwa anakokota pikipiki.

Wavamia nyumbani kwa Bonge
Inadaiwa Bonge ni mwizi maarufu maeneo hayo na kutokana na rekodi yake ya nyuma vijana wengi wa Bodaboda walikuwa na kisasi naye na walikuwa wakisubiri ‘ajichanye’.

Wakiongozana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichanganyi,….. wakafika nyumbani kwa Bonge ambaye baada ya kubanwa akakiri kuiba pikipiki husika, akaenda kuonesha alipoificha, kisha akachukuliwa kwenda kuhifadhiwa katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa, akiwa pamoja na kijana ambaye alijeruhiwa na kuporwa pikipiki.

Bodaboda wavamia
Ilipofika alfajiri, kundi la Bodaboda zaidi ya 30 wakavamia ofisi hiyo wakimtaka mtuhumiwa kwa kuwa ni kawaida yake kufanya matukio na kuachiwa.

Nguvu iliyotumika ikawazidi nguvu viongozi wa Serikali za Mtaa, wakafanikiwa kumtoa Bonge na kutokemea naye kusikojulikana huku mashuhuda wakidai walielekea njia ya Gongo la Mboto.

UPDATES....
Mwenyekiti Serikali ya Mtaa ya Kichangani, Leonard Nyukuli alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema "Nipo nje ya ofisi, kama unataka taarifa zaidi njoo ofisini utapata taarifa rasmi ya kiofisi."

MWILI WA BONGE WAPATIKANA
Mwanafamilia wa marehemu (jina linahifadhiwa) amesema mwili ulipatikana maeneo ya Vingunguti, juzi (Agosti 3), Mama Bonge tumezungumza naye amesema alipopata taarifa za tukio akajua siku ya mwanaye imefika hata kabla ya kuupata mwili, ni kama alishajiandaa kisaikolojia kutokana na matukio ya nyuma.”

Naye, Mwenyekiti wa Kichangani, Leonard Nyukuli amesema "Wananchi waache kujichukulia Sheria mkononi, mtuhumiwa alitoa ushirikiano akaonesha pikipiki, kuna watu waliotoka sehemu nyingine ndio wakafanya hayo waliyofanya, tuliita Polisi hawakufika kwa muda muafaka ndio yakajitokeza hayo."
Polisi wamejirudi, wizi utapungua.
 
Mwizi sio wa kumchekea, haswa Hawa wa bodaboda, ni kuua Mara 1 kenge Hawa, wanaua vijana(bodaboda) kikatili mnoo
 
Watu wengi hawajui hilo.
Unataka Pikipiki ya 2m,mtu anakupiga na shoka au hata chuma kizito.
Wameua Vijana wengi sana ambao pia wana Familia.
2M ni ya kuua mtu kwa Shoka tena mapema tu jioni.
Boda boda wengi siku ni vijana wana Diplom na Degree,kuna baadhi ya vijiwe wapo Elite sana.Wanataratibu ngumu hat huku Maofisini hakuna.

Hii ni kulinda maisha yao.

Hata huko kwenye Bajaj,na ndio maana wana Intel zote za wizi na kila aina ya ushenzi.
Hizi zimekuwa kazi kama kazi zingine.Ikumbukwe kama Boda na Bajaji zisingekuwepo vijana wengi wangekuwa wezi na mtaani huku kungekuwa kugumu sana.

Japo baadhi yao pia wamekuwa wezi tokana hulka zao na tabia.
Kabisa
 
Back
Top Bottom