kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
- Thread starter
- #21
Tuone ni namna gani hawa watu watakavyoweza kupitiwa pia na mnyororo wa mzunguuko wa hela mifukoni mwao, bila hivyo watapita tu hata kama uking'oa matairi yao. Hata wao ni mashahidi wa wenzao walioburutwa na kufa kwenye njia hizo, kama ni kuacha basi wangeacha kwa kuona ajali zinazowapata wenzao. Ukweli vijana hao hawana cha kupoteza kwanza hata hizo pikipiki sio za kwao, kwao wao ni heri wafie barabarani kwa ajali kuliko kufia uvunguni mwa kitanda kwa njaa.isitoshe hili lilijulikana kabla hata njia zenyewe hazijazinduliwa. visingizio kwamba hawasikilizi au hawana redio/tv ni kiduchi sana. mbona mengine ya maandamano yanawafikia? wenzao waliogongwa kwa makosa ya kupitisha tukutuku zao hapo hawakupewa maonyo? yule abiria aliyeburutwa uvunguni mwa basi si aliponzwa na dereva asiyejua au aliyekaidi sheria? iweje leo tuendekeze na kulea makosa yatakayogharimu maisha ya wenzetu na vilema vya maisha ati ni kuogoapa sera ya 'wapiga kura' kwani wanaogongwa na kufa/kulemaa sio wapiga kura? tuweke itikadi kando tukemee na kupongeza inapobidi. mizaha na michezo michezo kwa uhai wa binadamu tuuepuke kabisa.