kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Nijuavyo mimi bodaboda wengi hawana TV, ving'amuzi wala muda wa kuangalia TV au kusikiliza redio. Muda mwingi wanasikiliza muziki kwenye flash zao kwenye pikipiki ili kujaribu kuvutia wateja wapande bodaboda zao. Tangazo la rais kuhusu kung'oa matairi ya bodaboda zao huenda halikusikika kwao, hivyo sio vizuri watendaji kumchonganisha Rais na wananchi wake kwa kushindwa kutafsiri kauli zake.
Mimi nilidhani kuwa baada ya mh. Rais kutamka vile nyie watendaji mngejiongeza kwa kutoa elimu zaidi kwa waendesha bodaboda kuhusu utekelezaji wa kauli ya Rais na ubaya wa kupita kwenye barabara za UDART kabla ya kuanza kung'oa tairi za bodaboda fasta fasta huku mkipaza sauti kuwa mnatekeleza agizo la Rais.
Kusudio kuu la Rais pale halikuwa kung'oa tairi za bodaboda bali alitaka watendaji wakuu kuepusha ajali za barabarani kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizoko kwenye makablasha yetu. Kung'oa tairi la mkosaji ni kanuni au sheria namba gani ya usalama barabarani?
Ningekuwa mimi ndio mh. Magufuli ningewatumbua waliong'oa tairi za bodaboda za wapiga kura wake, maana wameshindwa kazi kwa kushindwa kujiongeza, kutafsiri na kuzuia ajali za barabarani kwa kutumia sheria na kanuni zilizopo za kuzuia makosa ya barabarani. over!