Bodaboda wafundishwe maadili ya kazi

co fm

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,411
2,138
Habarini wanajamii,

Moja kati ya vitu ambavyo madereva bodaboda wanakosa licha ya kuwa wasaidizi wetu katika kutupeleka na kutuwahisha hapa na pale ila wanakosa maadili ya kazi.

Jumamosi asubuhi hapa tunapoishi nilisikia maneno watu wakizozana alikuwa ni mama Juma na baba Salehe, mama Juma alikuwa akimshutumu baba Salehe kuwa anamtangazia kwa bodaboda kuwa huwa anapelekwa kwa mparange (hii ni tafsida ila wakubwa wataelewa).

Hii ni kutokana na kwamba kuna bodaboda huwa anamtumia baba Salehe katika safari zake za kwenda kwenye mishe zake, sasa katika mazungumzo ndio akamwambia mama Juma huwa anaenda huko kwa mparange.

Basi yule bodaboda siku alivyompakia mama Juma si akamwambia fulani anasema hivi, mama Juma hakuamini bodaboda akamwambia nimpigie simu halafu umrekodi huku ukimuuliza basi boda boda yule akampigia simu baba Salehe huku wakimrekodi yeye ajui anarekodiwa si akathibitisha. Sasa mtiti wake ndio ulikuwa hapa jumamosi hatari sana.

My take: Boda boda wajifunze ethics za kazi zao sio kuchonganisha watu
 
Yeye Huyo Baba swalehe alijuaje mambo ya mama Juma?

Kama soon kwamba mama Juma alimpitisha baba swalehe hiyo njia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom