Bodaboda ni maisha, bodaboda ni uchumi

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
BODABODA ni jina maarufu lililozoeleka nchini Tanzania likimaanisha ni Dereva anayeendesha chombo cha moto aina ya Pikipiki, ambapo kwa siku za nyuma iliaminika ni usafiri ambao anaweza kutumia mtu binafsi, makampuni au taasisi kusambaza huduma zake sehemu mbalimbali.

Lakini sasa tunaongelea Maisha ya watu ambao wamejikwamua kiuchumi kwa kutumia pikipiki kama kitegauchumi cha kuingiza pesa ili kuweza kulipa ada za za watoto, kujenga, kumudu gharama za kila siku kwenye maisha na mahitaji mengine ya msingi.

Duniani kote hakuna Serikali ambayo imeondoa changamoto ya ajira kwa kuwaajiri watu wote waliopo nchini ili kuondokana na changamoto ya ajira bali hutengeneza mazingira yatakayowezesha wananchi wake wajikite katika kujiajiri kwa kuwawekea mazingira wezeshi.

Na utakubaliana na mimi kuwa sekta isiyo rasmi ndio imeajiri kundi kubwa la watu ulimwenguni kuliko serikalini sasa kwanini sisi Tanzania tuaminishwe hii ni laana??

Rais Samia tangu aingie Madarakani ameyaangalia kwa ukaribu makundi haya hususani BODABODA na hapa aliwapunguzia na kuondoa baadhi ya tozo na sasa barabarani wanalipa faini ya shilingi elfu kumi kutoka elfu thelathini, Mama Ntilie, wamachinga maana ndipo uchumi wa wengi umeegemea huko.

Nyinyi mnaokebehi kundi hili na kuwaona si chochote kuna mahala mnajisahau ndugu zenu wamenusurika kwa mengi kwa kutumia bodaboda kuwahi ambako wangechelewa pengine wasingekuwa hapo lakini kuna kina mama wanawahishwa Hospitali , wagonjwa na wengine bodaboda ndo usafiri wao kila siku, msijisahau Haya ndio maisha yetu ya kila siku.
 
Ila bodaboda wanaandamwa sana wakati wanatafuta maisha. Nawaza hapa kama kitu cha kulamba asali kwa Lema ili waondolewe mjini hakuna cha ziada. Wanataka kuwafukuza kijanja. .
 
Kila mmoja afanye yake wewe wapeleke watoto wako kwenye bodaboda. Lema achana nao na ikiwezekana futa kauli hiyo wafurahi!
 
Back
Top Bottom