Bodaboda ni kazi ya ku take risk sana

Bodaboda ni kazi ya ku take risk sana

juzi pale bunju dawasco boda boda kapigiwa honi na gari akataka atoke pembeni kumbe bara bara pembeni ina zile cabistone.ngao ya pikipiki ikapiga akarudishwa barabarani.karudisha namba mapema tu.alafu bado kijana na ana mke
Very risk job, na ukiongezea na elimu yao ndogo ya usalama barabarani, na ukiongeza na madereva wazembe tatizo linakuwa kubwa sana. Nilikuwa na mgonjwa wangu pale MOI mwaka juzi, nikakuta mama mmoja ana miezi 6 hapo MOI baada ya kupata ajali ya bodaboda. Anaelezea kwamba alitoka zake mkoani,Tabora, akashuka Mbezi Magufuli stend akachukua bodaboda. Kwenye hiyo boda akawa yeye, mtoto mgongoni, na mabeji yake. Wakiwa barabara boda akaamua kupita katikati ya Lori kubwa na Lori lingine lililobeba konteina. Bwana wee kabla hajamaliza hiyo ovateki yake katikati ya hayo malori 2 ile lori yenye konteina ikawa kama imeyumba, boda kwa kupaniki akayumba na kwenda kujibamiza pembeni kwa lori lingine, wakaanguka. Yule mama akajikuta katupwa uvunguni kwa lori la konteina, gonga kichwa na kutoteza fahamu. Hakujua kilichoendelea mpaka anazinduka yuko hospital, kavunjika mguu, majeraha kichwani nk. Mtoto wake alivunjika mkono tuu na boda alifariki pale pale. Yaani ni kazi hatarishi sana, na pale MOI walikuwa wengi kweli kweli.
 
Umeona hapo hapo ni uzembe wa dereva , kama uko makini umepitia mafunzo darasan huwez fanya hivyo

Kuna jamaa hapo juu kasema vifo vya boda vinasababishwa na wenyewe sio risk ya kazi Bali uduanzi wao
 
Back
Top Bottom