Bodaboda hawana Haki

Kama ulimwambia akukimbize chap Kariakoo ulitegemea nini? Ndio maana wanashauri na wewe kama abiria kuchukua tahadhari unapoona dereva wako anakiuka sheria
Abiria uchukue tahadhari gani mkiwa mko kwenye mwendo tayari? Kuna muda unapanda tu unamwambia twende taratibu, akishaona vipi sijui anasahau anavuta mafuta. Best way ni kutokupanda boda kabisa kwa wanaoweza japo kuna muda boda hazikwepeki.

Mimi napanda boda barabara za mtaani tu, main road hapana. Serikali Ifanye jambo vijana wa boda wataisha.
 
Sio DIT kabisa ni nyuma kidogo pale kwenye mataa ambapo kuna barabara ya kwenda Lumumba kama sijakosea.. Muda mwingine madereva wa mwendokasi wanadharau mataa.
Madereva wa mwendo kasi wanaheshimu taa na wapo makini njiani nishaona sehem tofauti wakipiga breki kupisha boda wanaoingia kimakosa mfano mzuri barabara ya msimbazi
 
...kwa hiyo ulitaka basi la mwendokasi liipishe boda?
 
Siku moja nimepanda bodaboda natoka Ubungo naenda Kimara , tuko njiani mbele kuna semi trailer mbili zinatembea mwendo wa kawaida ziko sambamba kwenye barabara la lane mbili. Yule dereva wa bodaboda si akaona uchocholo kati ya zile semi trailer mbili. Naona jamaa anaongeza speed anataka apite katikati ya yale maroli. Ikabidi nimvute shati nikamwambia aache ufala tutakufa vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…