Boda Boda - SUNLAG

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
Wana JF

Ni duka gani (DAR) naweza kupata pikipiki za SUNLAG kwa bei nzuri, nimeelezwa pikipiki hizi zinadumu kidogo. Kuna aina nyingine ambazo zina sifa nzuri na bei zake ni poa.
 
Wana JF mliopo DAR vipi? hata window shopping huwa hamfanyi atleast kujua bei za SUNLAG?
 
Kama unaishi Dar, tembelea mtaa wa Swahili( mtaa ambao magari ya Mwenge na Kawe yanaingia Kariakoo kutoka huko Mwenge, ) pale pana maduka mengi ya pikipiki, au uje mtaa wa Sikukuu pia pana wauzaji wengi wa hizo pikipiki bei inarange between 1m na zaidi kidogo ( kama huujia mtaa wa Sikukuu teremkia kitio Cha Bakhresa hapo mtaa wa Msimbazi kata mtaa wa kwanza kushoto kuna maduka lukuki ya pikipiki
 
Wana JF

Ni duka gani (DAR) naweza kupata pikipiki za SUNLAG kwa bei nzuri, nimeelezwa pikipiki hizi zinadumu kidogo. Kuna aina nyingine ambazo zina sifa nzuri na bei zake ni poa.

Nakushauri waone Saba General pale msimbazi au lumumba
 
Kama unaishi Dar, tembelea mtaa wa Swahili( mtaa ambao magari ya Mwenge na Kawe yanaingia Kariakoo kutoka huko Mwenge, ) pale pana maduka mengi ya pikipiki, au uje mtaa wa Sikukuu pia pana wauzaji wengi wa hizo pikipiki bei inarange between 1m na zaidi kidogo ( kama huujia mtaa wa Sikukuu teremkia kitio Cha Bakhresa hapo mtaa wa Msimbazi kata mtaa wa kwanza kushoto kuna maduka lukuki ya pikipiki

Asante Mkuu, japokuwa kwa sasa nipo nje ya DAR. Nitapita hii mitaa katika siku za karibuni.
 
Labda nikushauri hivi, sun LG, za sasa sio kamzile zilizokuwa toleo la miakamiwiliiliyopita, sasa hivi wanauza tu jina lakini pikipiki hizi za sasa hazina uimara mzuri sana. Tafuta majina mengine ya pikipiki kama SUKIDA ni nzuri mimi niayo, zinapatika alog uhuru road mita kama 150 kama unatoka mnazi mmja. Nilinunuaga 1.3 m, wakati Sun lg kwa sasa ni tsh 1.8. see price difference? lg wanuza jina tu kwasasa lakini sio ngumu sana.
 
Asante Sana Mkuu, haya ndiyo mambo niliyokuwa nategemea hapa JF.
 
Mgombezi!
hiyo piki piki unataka kuitumia wapi?kwa biashara au matumizi ya usafiri wako binafsi. kama ni binafsi nakushauri ununue piki piki za india,hasa make ya Bajaj boxter ni imara na madhubuti.
kama ulivyoshauriwa hapo juu,usinunue SanLG za sasa ni feki-feki, meaning hizo za mwanzo ni standard ya feki,ila za toleo la sasa ni Feki ya feki za mwanzo(i hope umepata picha)

2,ushauri wa pili kama ni wewe mwenyewe na unataka kutumia in DAr.nenda ukate BIMA ya miguu yako na shughuli zako,just incase kwani Muhimbili-moi sasa wameamua kutoa huduma feki kwa wanaopata ajali za pikipiki
 
Nimecheka sana hapo kwenye red!

Asante kwa usahuri wako mkuu; pikipiki hii nataka kufanya biashara ya BODA BODA kijijini kwetu, lakini zaidi ya hapo itaweza kunisaidia kufanya mizunguko ya huko kijijini ninapokwenda shamba.
 
Wana JF

Ni duka gani (DAR) naweza kupata pikipiki za SUNLAG kwa bei nzuri, nimeelezwa pikipiki hizi zinadumu kidogo. Kuna aina nyingine ambazo zina sifa nzuri na bei zake ni poa.

Nenda pale AKIBA utawaona wachina wenyewe.

Lakini kumbuka kuna SUNLG na SANLG na maduka yanapakana hapo hapo kwa wachina.
 
Asante Mkuu; ndiyo maana niliogopa kwenda kichwa kichwa maana hizi bidhaa za kichina usipokuwa makini unaweza kuuziwa made in KARIAKOO.
 
Kweli mkuu alafu hizo SUNLG na SANLG moja ya kuchakachuliwa na bei zipo tofauti moja bei juu ingine bei chini.
 
mimi sijui kwa DSM zinapatikana wapi ila nina project ya bodaboda mkoa ninapoishi hivyo nina uzoefu sana na hiyo biashara. Kuna SUNLG na SANLG ila ambazo ni nzuri ni SUNLG na mpk sasa ndio pkpk imara ktk soko ukilinganisha na nyingine kwani mara ya mwisho nimenunua mbili mwezi wa 4 na ziko vizuri tu kiuimara.

Kikubwa cha kuzingatia ni kumpata dereva mzuri na mwaminifu ambaye anajua matunzo ya chombo chake maana nyingi uwa zinaharibika kutokana na mapepe ya madereva wengi ni vijana wasio na uchungu na mali ya mtu wala kuwa na future na kazi yake.

Ni vizuri upate dereva ambaye ametulia na haswa mtu mwenye familia ambaye atajali chombo chako na kuheshimu kazi ili atunze familia yake.

Kizuri ktk hii biashara ni kwamba haihitaji supervision sana kama biashara nyingine na ukiwa na pkpk nyingi kama tano na kuendelea utapata kipato kizuri tu ila ukiwa na moja au mbili ni kizunguzungu lakini nakushauri ufanye hiyo business pia uzikatie namba nyeupe za biashara na kulipa kodi zote za TRA kuepuka kamata kamata

Kuhusu bei:
SUNLG ni 1.8
SANLG ni 1.6

ongeza kama laki 3 hapo za malipo ya load licence, kofia, bima, mapato TRA na gharama za namba nyeupe
 
Kweli wewe ni FUNZA DUME!, asante sana kwa kunishirikisha uzoefu kwani nami nataka kuanzisha hii project huko kijijini kwetu.
 
Wana JF

Ni duka gani (DAR) naweza kupata pikipiki za SUNLAG kwa bei nzuri, nimeelezwa pikipiki hizi zinadumu kidogo. Kuna aina nyingine ambazo zina sifa nzuri na bei zake ni poa.
Kama ni kwa biashara zitafaaa kwani bei rahisi... Tshs..1.4 m unapata. kama ni kwa matumizi binafsi nakushauri utumi pikpik za familia ya BAJAJ.. ni nzuri, nyembamba(kama wapta ktk foleni), na zina dumu sana.
 
Wana JF

Ni duka gani (DAR) naweza kupata pikipiki za SUNLAG kwa bei nzuri, nimeelezwa pikipiki hizi zinadumu kidogo. Kuna aina nyingine ambazo zina sifa nzuri na bei zake ni poa.

NAPANDISHIA HAPOHAPO.. Hivi bishara ya kukodi byke ikoje... changamoto zake ni zipihasa... niijuayo ukiondoa kununua vifaa feki... madrevea waamini ndio tabu kubwa kuwapata...
 
Hii biashara mwanzoni ilikuwa ina faida sana, ila kwa siku hizi TRA wameziwekea kodi ya mapato ambayo ukipiga hesabu unakuta faida si kubwa sana kama ukiwa na moja.

Kwa mfano kwa sasa pikipiki nzuri inauzwa Tshs 1.8 M ukiongeza na kodi, bima, namba, road licence n.k inafikia kama Tshs. 2.1 hapo hiyo laki tatu inajirudia kila mwaka (kodi ya mapato, bima na road licence)

Na pia mapato yake kama unapokea kila wiki ni Tshs 42,000/= hapo ina maana 7000/= kwa siku moja ila kwa wiki unamwachia dereva siku moja kama mshahara wake ambapo service na matengenezo madogo chini ya 3000/= anafanya dereva kwa gharama zake.

sasa mwaka uwa una wiki 52 so take 52 x 42,000 = 2,184,000/= kwa mwaka hapo sijapiga hesabu za matengenezo makubwa ambayo yakitokea unaletewa tajiri ambayo nayo yanapunguza sana kipato. Pia kuna vitu kama kuisha matairi, shock ups, taa kuvunjika, betri kwisha nguvu bila kusahau ajali ndogo ndogo n.k

Hivyo ukitaka ilipe inatakiwa ukae nayo zaidi ya miaka miwili ambapo pikipiki inakuwa imechoka sana na gharama za matengenezo ni kubwa.

Vitu fake pia vipo ila kama ukiwa makini unaweza kupata bidhaa original ila kama unapenda vitu cheap au ukiwa unamwachia dereva tu atengeneze bila wewe kufuatilia anaweza kukuwekea vitu fake ili ale cha juu

Sasa ili hii biashara ilipe na uifurahie inabidi ufanye kifuatacho ambacho mimi uwa nakifanya; ingia mkataba na dereva wa pikipiki wa maandishi kuwa akuletee tshs 3.5 M kwa mwaka mmoja na nusu kisha unamwachia pikipiki inakuwa yake. Hiyo inamwezesha kufanya kazi kwa bidii na kwa kuwa wanapata ziada nyingi atajitahidi akusanye ili alipe hiyo hela kwa muda mfupi pikipiki iwe yake. Pia ataitunza sana kwani itakuwa ni mali yake.

Hiyo mbinu hapo juu ndio imenifanya mpk leo niendelee na hiyo biashara na kila pkpk nimeifungulia daftari na nimefungua akaunti. Ila nakutahadharisha kuna madereva wanaweza kukutia kizunguzungu mpk unaweza kupiga mtu makofi.

Ukiwa na nyingi na ukitumia mfumo huyo hapo juu utaona faida kidogo ila kama ukitumia njia a kuchukua pesa bila mkataba utakuwa unawapa ajira madereva tu ila wewe mwenyewe hupati chochote na waliovuruga utaratibu ni TRA wameweka kodi ya mapato kubwa ambayo sio realistic ukitazama na kipato anachopata mwenye pkpk na kwa ufupi mimi niko mbioni kuachana na hii biashara.

NB: Hii biashara si nayoitegemea kuendeshea maisha, ninaifanya tu kama hobby yangu kufanya ujasiriamali
 
Mgombezi!
hiyo piki piki unataka kuitumia wapi?kwa biashara au matumizi ya usafiri wako binafsi. kama ni binafsi nakushauri ununue piki piki za india,hasa make ya Bajaj boxter ni imara na madhubuti.
kama ulivyoshauriwa hapo juu,usinunue SanLG za sasa ni feki-feki, meaning hizo za mwanzo ni standard ya feki,ila za toleo la sasa ni Feki ya feki za mwanzo(i hope umepata picha)

2,ushauri wa pili kama ni wewe mwenyewe na unataka kutumia in DAr.nenda ukate BIMA ya miguu yako na shughuli zako,just incase kwani Muhimbili-moi sasa wameamua kutoa huduma feki kwa wanaopata ajali za pikipiki
- Mkuu....Chonde Mkuu...... unaua bendi
 
Hii biashara mwanzoni ilikuwa ina faida sana, ila kwa siku hizi TRA wameziwekea kodi ya mapato ambayo ukipiga hesabu unakuta faida si kubwa sana kama ukiwa na moja.

Kwa mfano kwa sasa pikipiki nzuri inauzwa Tshs 1.8 M ukiongeza na kodi, bima, namba, road licence n.k inafikia kama Tshs. 2.1 hapo hiyo laki tatu inajirudia kila mwaka (kodi ya mapato, bima na road licence)

Na pia mapato yake kama unapokea kila wiki ni Tshs 42,000/= hapo ina maana 7000/= kwa siku moja ila kwa wiki unamwachia dereva siku moja kama mshahara wake ambapo service na matengenezo madogo chini ya 3000/= anafanya dereva kwa gharama zake.

sasa mwaka uwa una wiki 52 so take 52 x 42,000 = 2,184,000/= kwa mwaka hapo sijapiga hesabu za matengenezo makubwa ambayo yakitokea unaletewa tajiri ambayo nayo yanapunguza sana kipato. Pia kuna vitu kama kuisha matairi, shock ups, taa kuvunjika, betri kwisha nguvu bila kusahau ajali ndogo ndogo n.k

Hivyo ukitaka ilipe inatakiwa ukae nayo zaidi ya miaka miwili ambapo pikipiki inakuwa imechoka sana na gharama za matengenezo ni kubwa.

Vitu fake pia vipo ila kama ukiwa makini unaweza kupata bidhaa original ila kama unapenda vitu cheap au ukiwa unamwachia dereva tu atengeneze bila wewe kufuatilia anaweza kukuwekea vitu fake ili ale cha juu

Sasa ili hii biashara ilipe na uifurahie inabidi ufanye kifuatacho ambacho mimi uwa nakifanya; ingia mkataba na dereva wa pikipiki wa maandishi kuwa akuletee tshs 3.5 M kwa mwaka mmoja na nusu kisha unamwachia pikipiki inakuwa yake. Hiyo inamwezesha kufanya kazi kwa bidii na kwa kuwa wanapata ziada nyingi atajitahidi akusanye ili alipe hiyo hela kwa muda mfupi pikipiki iwe yake. Pia ataitunza sana kwani itakuwa ni mali yake.

Hiyo mbinu hapo juu ndio imenifanya mpk leo niendelee na hiyo biashara na kila pkpk nimeifungulia daftari na nimefungua akaunti. Ila nakutahadharisha kuna madereva wanaweza kukutia kizunguzungu mpk unaweza kupiga mtu makofi.

Ukiwa na nyingi na ukitumia mfumo huyo hapo juu utaona faida kidogo ila kama ukitumia njia a kuchukua pesa bila mkataba utakuwa unawapa ajira madereva tu ila wewe mwenyewe hupati chochote na waliovuruga utaratibu ni TRA wameweka kodi ya mapato kubwa ambayo sio realistic ukitazama na kipato anachopata mwenye pkpk na kwa ufupi mimi niko mbioni kuachana na hii biashara.

NB: Hii biashara si nayoitegemea kuendeshea maisha, ninaifanya tu kama hobby yangu kufanya ujasiriamali

Heshima mbele kwa ushauri wako... nakumbuka kilishaandikwa kiitu cha namna hii(RED) hapa JF. (Green) ndo mawazo yangu hasa..
 
Back
Top Bottom