meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,349
- 4,674
- Thread starter
- #21
huyu meningitis nafikiri ni mmoja wa aidha recent graduates au mtu ambaye hajawahi ajiriwa serikalini katika wizara ya afya. naamini haujui utendaji kazi wa huyu mama, kwa taarifa yako na wengineo huyu mama ni miongoni mwa best PS MOH has ever had in the recent years. amejitahidi kuweka mambo mengi sawa wizarani, ukiritimba umepungua na kazi nyingi ziko safi, ila naamini mapungufu yapo kwa kila mtu ila huyu mama wengi tunapenda abaki wizarani kwa taarifa yako
anatakiwa atambue kuwa mwishoni mwa mwaka jana zoezi kama hili lilifanyika, waajiriwa walikuwa posted,lakini kwa bahati mbaya, kuna watu wizarani walighushi saini ya katib mkuu mama nyoni na wakawapangia watu vituo vya kazi kwenye wilaya mbalimbali. kwa taarifa yako, mama nyoni alipojua hivi alikasirika sana na kuna watu pale wizarani wanachunguzwa juu ya sakata hilo, sasa wewe unataka leo akurupuke tu kupanga watu ilhali kuna wasiomtakia mema na kughushi saini yake?
jengine zamani watu walikuwa posted hovyohovyo, matokeo yake watu wakawa hawaendi kwenye zile wilaya na mikoa waliyopangiwa,hivyo wizara mwaka huu imewaambie muindicate halmashauri tatu mnazopenda kufanya kazi, sasa wewe unatakiwa ujue mahitaji ya watumishi katika kila halmashauri hayafanani, wengine wanahitajika sana na wengine wanahitaji wachache katika kada fulani kwa hiyo zoezi lazima liendeshwe kwa umakini, msije mkajikuta kila anayeomba mnapeleka kanda flani tu,
pia usisahau kuna wilaya zingine hazikupeleka vibali vya maombi ya kazi wizarani, kwa hiyo wewe mathalani ni medical doctor AU NURSE MWENYE DEGREE AU NI PHARMACIST unaomba nafasi wilaya ya korogwe lakini iwapo korogwe haikupeleka maombi wizarani kuwa inamhitaji MD AU RN mwenye degree au pharmacist bali inawataka CO au AMO au nurse mwenye diploma au pharmaceutical technician tu unafikiri nani atakupeleka wewe MD , BSCN au PHARMACIST kwenye wilaya hiyo? Ninachomaanisha usifikiri sometimes kuwa wilaya fulani ina uhaba wa wafanyakazi na ukaanza kulaumu wizara haipeleki watu kule, bali tatizo linaweza kuwa kwenye wilaya ileile kwani makatibu wa afya wanaweza wasipeleke maombi ipasavyo ya ikama ya watumishi wizarani au kada flani flani wasiziombe,
so unatakiwa uelewe mambo badala ya kuwa mtu wa kukurupukarupuka wala huelewi ishu za kiserikali
serikali haina ishu! ina sera,mipango na mikakati.kwa taarifa yako natambua na kufuatilia jinsi halmashauri zilivyoomba watumishi wa kada mbalimbali za afya.hivyo hata kwenye uombaji wangu nilifuata msingi huo.sina tabia ya kukurupuka kama wewe.malamiko haya si yangu tu bali even some of DMOs ambao wanahitaji watumishi hawa ambao hupatikana kwa nadra wanalalmikia hili.