Blackberry vs Simu nyingine

Sana sana ni hiyo BlackBerry messenger tu, but its no match to Iphone....
 
Mkuu unafahamu sababu nchi za Uarabuni kutaka kukataa kuzitumia hizo simu? Just Google it utajua naongelea kitu gani.

Soma vizuri post yangu, nimeelezea kwanini Uarabuni wanaibana BB, ni kwasababu ni TOO secure, kinyume na wewe unavyodai.
 
Kwa kuongezea tu ni kuwa watu walikuwa wanapenda BB kupitia application ya BBM (Black Berry Messaging) Sasa Iphone nao wamekuja na iOS 5 ambayo ina service kama hiyo iMessage ni service ambayo unaweza kutuma unlimited message bure kupitia WI-FI au 3G na itatumika katika iPad, iPhone na iPod
http://www.google.com/search?q=ipho...&tbo=u&ei=PKrvTYD9CY-OvQO_l9CPCQ&ved=0CDYQqAI

Hizo BB Messenger na iMessenger zote bomu, siku hizi kuna App kibao ambazo ni cross platform, mambo ya kuweza kuongea na watumiaji wa iPhone au wa BB peke yao yamepitwa na wakati, checki WhatsApp Messenger, unachat na iPhone, Android, Nokia, BB etc.
 
Blackberry ni kipi hasa ilicho zizidi simu nyingine?
Kaka BB ni mahususi kwa shughuli za kiofisi /kibiashara hasa linapokuja suala la BES na BIS hakuana simu itakayoifkia kwa sasa hasa kwenye mambo ya emails,usiri wa data kwa washindani wa kibiashra,BB imeundwa si kwa ajili ya kujifurahisha kama zilivyo I Phone,Nokia,HTC,SE
hazina radio,hata mambo ya video/music downloads si kwake hasa.pia kwa ku text kutumia Qwerty BB ni nzuri sana.Katiak simu zote kwa mambo ya kazi napenda BB ,i.e push email yake haina gogoro
 
Mi nadhani wabongo wengi tunanuanua BB kama fashion tu. kama unavyoona serikali inavyonunua mashangingi kwa safari za masaki tu posta.

BB ni corporate phone for corporate users . Sasa how many BB owner In Tanzania can call themselves corporate user???? kama watu wangejua concept nzima ya design na reason behind BB watagundua kuw ajap wanaitumia haikuwa Idea ya desinger iwe hivyo
hapo kaka umeongopa BB si kwa corporate user too hata mimi kalagabaho naitumia kwa BIS na inanisaidia sana kufanya kazi zangu za kijasiriamali ,ndio inaniletea ugali mezani kaka,simu zingine ni kwa ajili ya kupigia ,kupokea na kucheza music BB inasaidia sana kwa kazi kati ya smart phones kwani kwa huu mgao atleast betri inakaa na unaweza kutuma document faster ,hata laptop naanza kuisahau kidogo,kwangu mii BB ni kifaa cha kazi na si cha ulimbwende
 
wat eva the case wabongo wengi tuna bb coz of show off.wakati hana uwezo wa kununua bundle na haimasidi katika maisha yake .tujifunze kutumia simu kwa manufaa yetu na kazi zetu
mh aheri ya dotnta aliyenunua hummer ya kukodisha kwenye harusi anadai kanunua milioni 100,so kila mtu ana matumizi yake na sio show off wajemeni
 
Hili suala ni gumu kwa vile ni BB v Simu nyingine, ingetajwa simu maalum na BB fulani ingekuwa rahisi kujadili, laikini tukijadili kama maada ilivyowekwa BB zina mambo 3 makubwa, na moja linatia mashaka, la kwanza ni ni BBM na la pili ni keyboard na la tatu ni usalama, hili la tatu ndio linatia mashaka, ingawa BB inasemekana kuwa na encryption ya hali ya juu, wapo wenye kudhani kwamba Majasusi wa Marekani wanao uwezo wa kusoma kila kitu kwenye BB na ndio maana Waarabu walijaribu kuzigomea.

Ukiondoa hili specs za BB zote zinachosha, kwa wapenda sceen kubwa sina cha kueleza na mengine mengi. Ila kuna makala moja imeandikwa kwa kiswahili ikiwa na kichwa cha habari kwa nini BB hazingii kwenye simu kumi bora ya simu, Gajetek - Gajet na Teknolojia: Kwa Nini Blackberry Haziingii Kwenye 10 Bora? ningeomba tuipitie ili tujue kuwa BB si simu za maana kwa upande wa Hardware specs na apps, vitu ambavyo kwa sasa ni muhimu zaidi katika simu yoyote. iMessage inaweza ikaua BBM.
 
Mh jamani acheni story kitu samsung galaxy S2. Utapenda jinsi android inavyofanya mambo. Yaani hata iphone 4 pale wanahangaika. Nimetulia nayo hapa naenjoy nasubiri nione iphone 5 itajibu nini.
 
Kwa Nini Blackberry Haziingii Kwenye 10 Bora?


Nembo ya Blackberry simu maarufu kutokana na BBM
Kumi bora mara nyingi huwa ni mtazamo binafsi wa mwandishi au kundi fulani, hata hivyo ukiangalia chati za simu kumi bora mbali mbali zenye kutofautiana, kuna kitu kimoja zinafanana, nacho ni hakuna simu za Blackbery. Kwenye makala hii tutajaribu kufanya uchambuzi wa kina juu ya sababu zinazopelekea simu hizo kutokuwemo kwenye chati.




Blackberry ni simu zilizopata umaarufu mkubwa na kutumiwa na wateja wengi Duniani. Simu hizo hutengenezwa na kampuni iliyopata mafanikio katika sekta hii ijulikanayo kama Research In Motion maarufu zaidi kwa ufupisho wake, RIM. Pamoja na umaarufu wa simu hizo ni mara chache sana kuona simu za Blackberry zinaingia kwenye chati ya simu 10 bora. Kwa mfano tangu mwaka 2010 hadi sasa ni Blackberry Torch pekee ndiyo iliyoingia katika chati hiyo ambao inatawaliwa na simu za Apple, HTC na Samsung. Hata Blackberry Torch ilikaa kwa muda mchache na kutolewa.
RIM, nembo ya kampuni inayotengeneza simu za
Blackberry, Research In Motion
Ubora wa Blackberry

BBM: Simu hizi zimejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na njia ya kutumiana ujumbe baina watumiaji wake ijulikanayo kama Blackberry Messenger (BBM) ambapo wateja hupeana Blackberry Pin (BBP) na kuweza kuwekana katika orodha ya wenye kutumiana ujumbe, vile vile mtumiaji anaweza kumuingiza mtumiaji mwenziwe katika BBM kwa ku-scan barcode yake iliyoko kwenye simu hizo. BBM imesababisha simu za RIM kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa vija wa rika kati ya miaka 15 - 40 ukizingatia kwamba tumo kwenye wakati ambao mitandao ya kijamii au kibashasha (social network) ni kivutio kikubwa.

QWERTY kibodi: Hii inaendena sana na BBM kwa vile wengi wa watumiaji wa Blackberry huwa ni waandishi zaidi kuliko wazungumzaji katika simu zao, kibodi huwasaidia kuandika kwa kasi na urahisi kutokana na ufanisi mkubwa uliotumika na RIM kuzibuni (design) kibodi hizo.

Usalama (Security): Vile vile simu hizo zina usalama wa hali ya juu kwani si rahisi kwa mapaparazi, wapelelezi au mahaka (hackers) kuweza kupata ujumbe kwa njia ya wizi kwa vile Blackberry inatumia mitandao yao wenyewe kama njia za kupeleka ujumbe. Hata imefikia baadhi ya serikali kutaka kupiga marufuku simu hizo kwani hata vyombo vya usalama vya nchi vilishindwa kupata kusoma BBM za watu wakihofia kwamba magaidi watatumia uchochoro huu kuweza kuwasiliana na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi zao. Hii imeplekea watu wenye usiri kuvutiwa sana na simu hizo ikiwa ni pamoja na wanasiasa, wasanii na ‘masupastaa pamoja na maselebriti’ wengine.

QNX OS: Blackberry inatumia OS zao wenyewe ambazo hutumia utaratibu wa QNX. OS hii ina uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi sambamba (multi tasking) kwa namna ya kipekee, pia ina ufanisi wa hali ya juu kwa namna inavyofanya kazi. Muhimu zaidi ni kwamba Blackberry OS haihitaji kifaa (hardware) chenye kasi sana kufanya kazi kwa kasi, kwani OS hii ni nyepesi (lightiweight) mno.

Maradhi (Addiction): Utafiti unaonesha kwamba watumiaji wengi (si wote) wa Blackberry wana maradhi na simu zao kwa kuzitumia zaidi kuliko watumiaji wa simu nyingine zozote. Ukianza kutumia simu hizi basi ni taabu kuziacha, hali hii inachangiwa zaidi na BBM ambapo wengi wanapoitumia utadhani akili zimewaruka huwa hawasikii wala hawasikilizi, hucheka pekee yao na hujihisi hawako wapweke. Kwa upande wa RIM hili ni zuri kwani inakuwa si rahisi kumpoteza mteja.
Sehemu ya juu ya Blackberry Pearl 3G, ikionesha kamera yake
Udhaifu wa Blackberry

Zifuatazo ndio sababu za msingi zinazozifanya simu za blackberry kutokuwemo katika chati ya simu bora Duniani pamoja na kuwa na ubora tulioueleza mwanzoni:-

Skrini: Kwa asili simu za Balckberry zina skrini ndogo ukifananisha na simu ambazo hutamba kwenye kumi bora. Simu zote zilizokuwa kwenye kumi bora kwa sasa zina ukubwa wa skrini baina ya inchi 3.5 na 4.3. Bila ya shaka kampuni ya RIM wanalifahamu hilo ndio maana wakajaribu kutengeneza simu kama vile Torch na Storm.

Ubora wa Skrini (Quality): Rizolushan (Resolution) ni za hali ya chini kwa mfano Blackberry curve ina rizolushan 320X240, hii husababisha simu za Blackberry kutokuwa na mvuto wala mng’aro kwenye skirni kama zilivyo simu ambazo zinakuwemo kwenye kumi bora. Itakuwa si sahihi kulinganisha iPhone 4 na Curve kwa hiyo hebu tuangalie iPhone 4 ambyo ndiyo simu inayoweka viwango na Torch. iPhone 4 ina rizolishan 960X640 na PPI (pixel per inch) 326. na BB Torch ina rizolushan 480X360 na PPI 187.5, kwa mapana na maferu tunaweza kusema kwamba hii ni aibu kwa RIM. Skrini huchukuliwa kuwa ni hali ya juu (high end) ikiwa na PPI 300 na ya hali ya chini (low quality) ikiwa na PPI 150 au pungufu. Hii itakupa picha ni vipi Blackberry wanabana matumizi katika masuala ya Skrini.

Bofa Skrini: Wakati simu za skrini za kugusa (touch screen) zinaingia na kupata umaarufu kuanzia miaka ya 2007 ilipotoka iPhone, RIM wakataka kujitofautisha na kutoa skrini za kubofa (click screen) badala ya kugusa, hii iliwaangusha vibaya kwani simu hizo hazikuweza kukubalika na wateja, athari yake katika makosa kama haya yamepelekea jina la Blackberry na RIM (brand name) kushuka thamani kwa 20%, (Chanzo WPP). Sasa linganisha na Apple watengezaji wa iPhone ambapo brand yao imekuwa kwa 84% (Chanzo WPP)

Umbile: Nadhani hata baadhi ya watumiaji wa Blackberry watakiri kwamba simu hizi hazina maumbile ya kuvutia ukilinganisha na simu za Samsung, Apple, LG, Sony Ercisson na HTC. Hii imechangiwa zaidi na utaratibu wa RIM kuwa ni muhimu kwao kuweka QWERTY kibodi. Iwapo RIM wanataka kutoa ushindani katika simu za hali ya juu basi hawana budi kuwafukuza kazi baadhi ya wabunifu wa maumbile (designers) wao na kuajiri wapya.

Vianisho Halisi (Specs): Hapa hatuna maelezo mengi tutalinganisha Blakberry bora kuliko zote kwa viainisho (Torch) na Samsung Galaxy Ace ambayo ndiyo ya mwisho katika kumi bora za mwezi huu:

Torch: CPU 624 MHz, Kamera 5 mp, Video VGA 24 fps, Betri masaa 5:40 (kuzungumza), RAM 512.

Ace: CPU 800 Mhz, Kamera 5MP, Video VGA 15 fps, Betri masaa 6:30 (kuzungumza) RAM 256.

Kwa hiyo Torch inaikaribia simu ya mwisho kabisa katika kumi bora, iwapo wanataka kuingia katika simu bora hawana budi kuwa na viainisho halisi bora zaidi ili kutoa ushindani wa kweli.

Blackberry App World: hii ni aibu ya pili kwa RIM, soko hili la apps lina apps zisizozidi 20,000 ambapo ni chini ya 10% ya appstore ya Apple yenye apps zaidi ya 200,000 na Android Market yenye apps zaidi ya 150,000. RIM wanalifahamu hili, katika kufanya juhudi za kuwahamasisha watengenezaji wa apps kuingia kwenye soko lao RIM wametoa ahadi ya kumpa zawadi yoyote atakayepeleka app yake kwenye soko lao na kupasishwa, ambapo zawadi yenyewe ni Blackberry Playbook tablet ya bure.

Ni matumaini ya washabiki wa Blackberry na wapenda gajet Ulimwenguni kuwa RIM wamepata funzo kubwa kwenye utengezaji wao wa Blackberry Playbook na udhaifu uliowazi wa simu za Blackaberry. Playbook ni tablet ambayo inatarajiwa kupata mafanikio kwa kuwa imetengenezwa kwa umahiri mkubwa.


Sisi katika Gajetek tunaamini kwamba simu ya Blackberry ijayo itaingia katika cha chati yetu ya simu na kukaa kwa muda mrefu. Hata hivyo RIM wafanye haraka kabla ya Blackberry haijageuka kuwa Crapberry.

Chanzo Gajetek - Gajet na Teknolojia: Kwa Nini Blackberry Haziingii Kwenye 10 Bora?

 
Historia ya hizo simu inasema kwamba zilitengenezwa kwa ajili ya kazi za kijasusi tu kwa mashirika ya kijasusi ya kimarekani baadaye ndio zikawewkwa sokoni zikaweza kutumiwa na watu wote so tatizo la hizo simu walivyobadili mfumo kutoka kwa mfumo wa kijasusi kwenda kwa mfumo wa simu za kawaida kuna vitu ambavyo walisahau kuvitoa kwenye bios ya hizo simu,hizi simu hazina siri kwenye server zao za Canada na USA operator anaweza kusoma msg zote za kwenye hizo simu kuanzia sms mms hadi email nakila kitu kilichomo kwenye hiyo simu so mwenye simu anakuwa hana usiri tena na mambo yake thats why last year baadhi ya nchi za Kiarabu zilipiga marufuku matumizi ya hizo simu. Ingawa nimeshawahi kuzitumia lakini wala hazikunifurahisha hata kidogo coz internet unanua bundle yake yenyewe ya bb inayojitegemea kwa wiki au kwa mwezi wakati ukitumia smartphone ya iphone unanua bundle ya kawaida tu na matumizi yake ni ya kawaida tu wakati hiyo iphone kwanza speed yake ya net ni kubwa zaidi ya bb na ina apps za kueleweka.
kwa Bwn Omary unanishawishi ninunue iphone, nadandia mada ya jamaa yangu. Ila hiyo iphone iwe ni type gani (ukitilia maanani price conscious) nzuri zaidi??????????
 
hapo kaka umeongopa BB si kwa corporate user too hata mimi kalagabaho naitumia kwa BIS na inanisaidia sana kufanya kazi zangu za kijasiriamali ,ndio inaniletea ugali mezani kaka,simu zingine ni kwa ajili ya kupigia ,kupokea na kucheza music BB inasaidia sana kwa kazi kati ya smart phones kwani kwa huu mgao atleast betri inakaa na unaweza kutuma document faster ,hata laptop naanza kuisahau kidogo,kwangu mii BB ni kifaa cha kazi na si cha ulimbwende

Basi wewe ni "coprprate user". Nikisema corporate user haina maana mpaka uwe kwenye corporate fulani au uwe ni CEO .No . Nina maanisha mahitaji na mtumizi.

Hope umenilewa na utakubalina nami . Ndo maana nikatoa mfano wa mawaziri wetu wa Tanzani Kutumia mashangingi from masaki to posta. Wanazo sababu lakini uizingatia mahitaji na matumizi yao hata Vitara zingewafaa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom