Blackberry vs Simu nyingine

Mi nadhani wabongo wengi tunanuanua BB kama fashion tu. kama unavyoona serikali inavyonunua mashangingi kwa safari za masaki tu posta.

BB ni corporate phone for corporate users . Sasa how many BB owner In Tanzania can call themselves corporate user???? kama watu wangejua concept nzima ya design na reason behind BB watagundua kuw ajap wanaitumia haikuwa Idea ya desinger iwe hivyo


hahaa ndo sie ma corporate sasa tupo bize na BB zetu hapa samaki samaki....teeeh
 
Mkuu unaongea kinyume kabisa, BB ndo most secure mobile phone kama unataka privacy ndo maana zinatumika na makampuni mengi kutunza corporate secrets, nchi zinaibania for the same reason kwa sababu wanausalama hawawezi kusoma msg za watu, hili ni tatizo hata terrorists wa Mumbai walikuwa wanatumia BB na iliwasaidia kuficha mawasiliano.

Kampuni za zote za simu (provider) zinaweza kusoma msg zako, kwa sababu encryption iko kati yako na kampuni, tofauti na BB ambayo unaweza kufanya encryption end to end yaani kati yako na unayeongea nae kitu ambacho kinawanyima hata BB kusoma msg zako.

mkuu ww ndio naona upo kinyume kwani usalama wa bb aukusaidii ww mana kila k2 kipo kwenye server yao na wanauwezo wa kujua nyendo zako zote maongezi unayoongea,msg nk zipo juu sana kiulinzi kiasi kwamba ww kama unatumia unakuwa kama upo kwenye nyumba ya kioo
 
Mkuu tatizo si kuwepo kwa App, tatizo ni vipi App imekubalika, BBM inatamba kwa sababu ina watumiaji wengi, si masuala ya cross platform wala nini. La pili mkuu ni masuala ya vipi app hiyo infanya kazi sidhani kiufanisi unaweza kufananisha WhatsApp na iMessage au BBM.
 
Mayasa nijuze zaidi kuhusu kitu cha galaxy kuna mtu kanambia hajaniconvice bado, kaisifia galaxy mnoo!

Ni kweli kwa sasa Samsung Galxy S2 ndio simu bora Duniani kwa mengi tu, lakini mimi sina haja ya kueleza hawa jamaa wa Gajetek wamemaliza kazi yote: http://www.gajetek.com/2011/05/simu-kumi-bora.html Nadhani ukimaliza kusoma makala hii utakubaliana na wale watoa maoni kuwa Galaxy 2 ni namba moja
 
Mkuu tatizo si kuwepo kwa App, tatizo ni vipi App imekubalika, BBM inatamba kwa sababu ina watumiaji wengi, si masuala ya cross platform wala nini. La pili mkuu ni masuala ya vipi app hiyo infanya kazi sidhani kiufanisi unaweza kufananisha What's up na iMessage au BBM.
BB haina watumiaji wengi kama unavyofikiri RIM wana only 16% ya soko la smartphone, maana yake hauwezi kuonngea na asilimia 84% ya watu ukiwa unatumia BB messenger au iMessenger.

Ni feature gani ambayo umeikosa WhatsApp ambayo ipo BB Messenger? Ufanisi wake ni mzuri sana very straight forward, hakuna hata haja ya kucreate account, inafanya kazi staight out of the box hakuna hata haja ya kuingiza "pin" ya mtu, mtu yoyote ambayo yupo kwenye addressbook yako aliyeinstall WhatsApp anatokea automatically! INATISHA!!.. Apple wanataka waturudishe nyuma na iMessenger yao, sisi haturudi!!
 
mkuu ww ndio naona upo kinyume kwani usalama wa bb aukusaidii ww mana kila k2 kipo kwenye server yao na wanauwezo wa kujua nyendo zako zote maongezi unayoongea,msg nk zipo juu sana kiulinzi kiasi kwamba ww kama unatumia unakuwa kama upo kwenye nyumba ya kioo

Sio kweli, kwenye BB wewe ndo unacontrol keys za encyption, yaani key zinazotumika kuifunga na kuinfungua msg, hata RIM hawawezi kusoma msg zako kama unatumia keys zako mwenyewe. Hili ndo tatizo lililopelekea kutaka kufungiwa India na sehemu zengine, vyombo vya usalama vinataka kusoma msg za watu na kwenye BB inakuwa ngumu.

Pia sio kweli kuwa wanaweza kujua maongezi yako, voice haipiti kwenye server za RIM, inapita kwenye provider wako Voda, Tigo etc.
Pia kumbuka kuwa kila provider naweza kusoma msg zako kama hutumii encryption yako mwenyewe Voda wanaweza, Tigo wanaweza.
 
mi penda sana iphone
:mwaaah::mwaaah:ipad sio simu lakini mimi penda sana hiyo pia..

Blackberry kwa maoni yangu I think it's a perfect phone in the Corporate world. It's a very secure phone when it comes to sensitive government/ corporate information or data. Hata Obama ndio maana FBI/CIA na secret service wamemruhusu kuendelea kuitumia sababu iko very secure.
I can even log on and access my pc while I'm driving on my way to the office.
Personally kwa matumizi yangu binafsi naizimia sana iphone esp iphone4. Lakini kwa matumizi ya kikazi nadhani bBackberry haina mpinzani ukilinganisha na hayo matoy mengine
 
to me htc is another story.the killer features to me is ms outlook and msoffice integration.if you real want a smartphone htc is the answer.
 
Jamani hivi ni kweli tunaweza kushindana na teknolojia ya simu kiasi kwamba kila toleo jipya la simu uwe nalo?
 
ma corporate samaki samaki? Wacha vidampa sie tukatulie Kempiski

hahaaaa Kempinski wahudumu wamezidi viingeredha bana ...we tunaongea nao mpaka midogo inauma ..Mambo samaki samaki mpaka kihehe twende kazi....
 
Mkuu tatizo si kuwepo kwa App, tatizo ni vipi App imekubalika, BBM inatamba kwa sababu ina watumiaji wengi, si masuala ya cross platform wala nini. La pili mkuu ni masuala ya vipi app hiyo infanya kazi sidhani kiufanisi unaweza kufananisha What's up na iMessage au BBM.
BBM inabagua sana kwa nini usitumie MXit ambayo inakubaliana na smartphone nyingi na ukiangalia functionality is the same.My mxit ID: Mystro10
 
Mkuu tatizo si kuwepo kwa App, tatizo ni vipi App imekubalika, BBM inatamba kwa sababu ina watumiaji wengi, si masuala ya cross platform wala nini. La pili mkuu ni masuala ya vipi app hiyo infanya kazi sidhani kiufanisi unaweza kufananisha What's up na iMessage au BBM.
BBM inabagua sana kwa nini usitumie MXit ambayo inakubaliana na smartphone nyingi na ukiangalia functionality is the same.My mxit ID: Mystro10
 
Sio kweli, kwenye BB wewe ndo unacontrol keys za encyption, yaani key zinazotumika kuifunga na kuinfungua msg, hata RIM hawawezi kusoma msg zako kama unatumia keys zako mwenyewe. Hili ndo tatizo lililopelekea kutaka kufungiwa India na sehemu zengine, vyombo vya usalama vinataka kusoma msg za watu na kwenye BB inakuwa ngumu. Pia sio kweli kuwa wanaweza kujua maongezi yako, voice haipiti kwenye server za RIM, inapita kwenye provider wako Voda, Tigo etc. Pia kumbuka kuwa kila provider naweza kusoma msg zako kama hutumii encryption yako mwenyewe Voda wanaweza, Tigo wanaweza.
SPOT ON huo ndio ukweli MKuu, lakini kuna watu watabishi tu.

Na ukisoma kwa makini majibu humu kuhusu BB hutakuta wengi wako windowscentric (yaani wanabase zaidi katika windows network operating systems au tuite microsoft; chunguza terms zinazo tumika humu). Ukweli wa mambo ni kwamba siyo kila kitu lazima kipitie kwenye servers, mtu yeyote mwenye huelewa wa mahesabu na combinational logic (specifically exclusive or) zinazotumika katika encryption, anaweza ku-encrypt data zake ziwe za sauti, MSg, video na picha na kuzituma, cha muhimu hapa ni kutumia bits nyingi kidogo kufanikisha hilo kwa ajili ya usalama vile vile na kuhakikisha mwenzako unaye mtumia file hizo unampatia KEY ya kuweza kungamua ulicho mtumia; hakuna SERVER au firewall yoyote duniani inayoweza kujuwa kinacho endelea between end users. Kumbuka kwamba OS nyingi zinazo tumiwa na mobile phone manufacturers zimetokana na juhudi za OPEN SOURCE community kuanzia Android, Symbian na zinazo tumiwa na RIM and what have you. Kwa hiyo watu wa RIM wakisema kwamba hata wenyewe hawajuhi kinachotumwa na clients wao ni kweli.
 
[h=3]Simu: Kumi Bora (Sehemu 1)[/h]

1. Samsung Galaxy S 2
Samsung Galaxy SII
Kinachoifanya simu hii kuwa kileleni kwenye chati ni ubora wa vianisho halisi vyake, ina kasi na nguvu na pia ni simu nyebamba kuliko zote Duniani ambapo imeipiku iPhone 4 katika sifa hii. Ina kamera nzuri, yenye kutoa picha safi mno na uwezo wa kurekodi video za HD, vifuatavyo ni vianisho halisi vyake:-



Video: Full HD 1080p na megapiksel, ukiwa na simu hii basi huhitaji kamkoda wala kamera, simu nyingi kamera zake ni maskhara tu, lakini Galaxy S2 si hivyo ni kamera ya kweli yenye uwezo wa hali ya juu. Bila ya kutia chumvi unaweza hata kurekodi harusi iwapo utapata mwangaza wa kutosha.




Prosesa: Dual Core 1.2 Ghz aina ya snapdragon, hii ni prosesa yenye nguvu za kuendesha hata laptop wacha kijisimu, ina kasi kiasi kupindukia kasi inayohitajika kwenye simu.

Skrini: 4.3 Super Amoled Plus, hii inaifanya simu hii kuwa na skrini inayon’gara sana. Unaweza kutazama kwa pembe (angle) ya chini kabisa na kuona kwa vizuri na bila ya matatizo.

Kamera: megapiksel nane yenye flashi inaifanya simu hii kuwa na kamera yenye ufanisi kuliko zote kwenye simu, zipo simu zinazofanana na simu hii kwenye piksel hizi lakini mpaka sasa hakuna zaidi yake.

Umbile: Ikiwa na wembamba wa milimita 8.49 inaifanya simu hii kuwa ni simu nyembamba kuliko zote Duniani. Vile vile simu hii ina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kwa sauti ikitumia teknolojia ya Google ya kutambua sauti (voice recognition) na pia inatumia Android Gingerbread 2.3 ambayo ni toleo jipya la OS ya Android kwenye simu.

Simu hii imekamata kilele katika chati ya simu mwezi huu kwa kuipiku iPhone 4, je simu hii itaweza kubaki kileleni itakapotolewa iPhone 5 baina ya mwezi wa Juni na Septemba mwaka huu? Hatuna jibu, ni vyema tu tusubiri.

2. iPhone 4
iPhone 4 nyeupe
Simu hii imekuwa kilele kwa muda wa zaidi ya miezi kumi, kutokana na wingi wa simu na namna simu zinavyobadilika haraka si rahisi kwa simu kuwa kwenye chati kwa zaidi ya mwezi mmoja, hii inathibitisha namna ambavyo simu hii ilizitangulia simu nyingine kwa wakati ilipotolewa. Yavutayo ndio yanaifhanya simu huu kuwa ni miongoni mwa si bora:

OS: iOS 4.3.3 yenye ubora, ikitumia OS ambayo haipatikani kwenye simu yoyote nyingine, inaifanya iPhone kukosa ushindani wa karibu kwenye nukta hii. OS hii ni rahisi kuitumia na ina ufanisi bora.

Appstore: Hili ni duka la kununulia apps (program), lina apps zaidi ya laki mbili, ni kweli kabisa kama Apple wanavyodai kwenye tangazo la simu hii “kama huna iPhone basi huna iPhone” Karibu kila unachofikiria ambacho ungependa simu yako ifanye basi kuna app yake kwenye duka hili.

Skrini: Skrini yake ambayo inaitwa Retina inaukubwa wa inchi 3.5 na piksel kwa kila inchi (ppi) ni 320. Uwezo wa jicho kuona ni mwisho ppi 300 unapikamata kitu kiasi cha umbali wa sentimita 25 hivi. Hii maana yake ni kwamba macho yetu hayana uwezo wa kuona uzuri wa skrini ya iphone, yaani ni nzuri kuliko tunavyoiona.

SSD: Huhitaji kukunua SD kadi kwani haitumii teknolojia hiyo. Hata hivyo ina disk aina ya SSD (solid State Disk) yenye ukubwa baina ya 16GB na 32GB. Apple wanadai kwamba kadi za SD hupnguza kasi za simu.

iTunes: Mawasiliano baina ya simu hii na kompyuta hufanywa kwa kutumia program ya iTunes, hii hurahisisha kazi ya ku-backup simu na kuingiza mafaili kama vile muziki, vitabu (E Books), picha, video na apps na pia kuhamisha video, picha na apps zilizo kwenye i`phone kwenda kwenye kompyuta kwa ajili ya kutumia au kuhifadhi.

Umbile: Simu hii ina umbile la kipekee, ambapo ina kioo mbele na nyumba, ni ya pili kwa wembamba baada ya Samsung Galaxy S2 ambapo ina wembamba wa milimita 9.3 na ina kona za kiduara zinazoifanya kukamatika kuwe ni rahisi .

3. HTC Sensation

HTC Sensation


Huwezi kuzungumzia simu bora bila ya kuitaja HTC. Sensation kama jina lake ni simu ambayo ina ufanisi usiojificha.

Kuzima mlio: Simu hii kama zilivyo baadhi ya HTC, inapoita na ukaichukua na kuifunika kwa kuigeuza skrini kuelekea chini basi hunyamaza, ukiwa mkutanoni au darasani na umesahau kuitoa sauti basi hii teknolojia itakufaa sana wakati huo.

Vianisho halisi: Simu hii inafanana mambo mengi na Galaxy 2 ikiwa ni pamoja na Android Gingerbread , kamera yenye megapiksel nane, prosesa aina ya dula core yenye kasi ya 1.2 Ghz na ndio maana ipo karibu na juu kwenye chati hii.

Skrini: Ikiwa na ukubwa wa inchi 4.3 yenye mn’garo ulikithiri, uzuri skrini hii haitofautiani sana na skrini ya Samsung Galaxy S2.

HTC Sense: simu hii pia imevalishwa koti ya HTC Sense ambapo linaweza kukufanya usahau kama unatumia Android kwa namna koti hili lilivyo la kipekee. HTC Sense inaonyesha habari muhimu kwa urahisi ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, saa na tarehe katika mji uliopo, unaposafiri basi HTC Sense kwa kutumia sensa za GPS nayo hubadilika wenyewe kwa mujibu wa mji uliopo

HTC Sync: HTC sensation pia hutumia HTC Sync kuhamisha mafaili baina yake na kompyuta na hivyo kuifanya kazi hii kuwa ni rahisi kwa kiasi fulani tofauti na chukua na weka (drg and drop) inayotumika kwenye simu nyingine.


Umbile: Simu hii pia ina upana wa milimita 11 pana kwa milimita 2 tu ukifanannisha na iPhone bado inapendeza kwa kuiona na kuishika mkononi ni rahisi. Pia gamba lake limetengeneswa kwa namna ambayo HTC wenye we wanaiita ‘unibody’ yaani halina kufungwa msumari wala kuunganishwa unganishwa.

4. Motorola Atrix Laptop
Motorola Atrix
Simu hii ni moto kama ulivyo uhamasishaji wa Motorola ‘Moto’. Motorola wanastahiki kupengezwa kwa uvumbuzi wa kisasa walioufanya kwenye Atrix.
Dock: Doki hii hujulikana kama HD multimedia dock. Hichi kifaa ambacho unaiweka simu hii hukuwezesha kutumia internet ya simu kwenye kompyuta yako. Doki hii inakuwezesha kuunganisha simu hii na TV, kompyuta, skrini, mouse na keyboard kwa kutumia USB na HDMI.

Lapdock: Pia Atrix ina kifaa kijulikanacho kama Lapdock. Hii huigeuza Atrix kuwa laptop kamili. kila kilichomo kwenye simu inapokwa simu hii kwenye lapdock huwa kinaweza kupatikana kwenye lapdock ikiwa ni pamoja na mtandao wa simu, mafaili ya picha, muziki au video yaliyopo kwenye simu. Pia lapdock hii inauwezo ya kuonesha HD.

Lapdock na Atrix ikiwa imepachikwa
Vianisho halisi: Simu hii pia ni Android ambayo ilipotoka ilitumia toleo la Froyo 2.2 lakini kwa sasa unaweza kuiboresha na kuweka Android 2.3 Gingerbread. ina kamera yenye megapiksel 5.

Fingerprint: Simu hii ina usalama mkubwa. Ina teknolojia ya fingerprint inayokuwezesha kuitia loki na hivyo ni aliyeifunga tu kwa kutumia vidole ndiye utakaeweza kuifungua. Huna haja ya kukumbuka neno lasiri (password) wala kuwa na wasi wasi wa mtu wa karibu yako kuweza kujua neno la siri unalotumia

Hivyo badala ya kununua laptop na Simu waweza kununua Motorola Atrix na lapdock yake, ikiwa unataka kutumia kwa ajili ya kujifurahisha kwa video, muziki na picha basi dock maalum kwa shughuli hii (entertainment dock) hakitkufanya ujihisi kwamba umepungukiwa.

Sehemu ya pili ya makala hii tutazielezea simu zenye kushika nafasi ya sita hadi ya kumi nazo ni:

Sony Ericsson Xperia Arc

Google Nexus S

LG Optimus 2X

HTC Desire S

HTC Incredible S

Samsung Galaxy S
 
Sio kweli, kwenye BB wewe ndo unacontrol keys za encyption, yaani key zinazotumika kuifunga na kuinfungua msg, hata RIM hawawezi kusoma msg zako kama unatumia keys zako mwenyewe. Hili ndo tatizo lililopelekea kutaka kufungiwa India na sehemu zengine, vyombo vya usalama vinataka kusoma msg za watu na kwenye BB inakuwa ngumu. Pia sio kweli kuwa wanaweza kujua maongezi yako, voice haipiti kwenye server za RIM, inapita kwenye provider wako Voda, Tigo etc. Pia kumbuka kuwa kila provider naweza kusoma msg zako kama hutumii encryption yako mwenyewe Voda wanaweza, Tigo wanaweza.
SPOT ON huo ndio ukweli MKuu, lakini kuna watu watabishi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom