Ndugu yangu hapo umekutana na maprofesa(matapeli). Binafsi nina experience na hawa matapeli. Mwaka juzi 2009 ilinitokea kwa kutumiwa email kutoka UK. Niliijibu kwa kutoa details walizohitaji,baada ya siku chache nikapata email kuwa mimi ni mshindi na nimepata euro 950,000. Nikapewa maelekezo ya namna ya kuipata zawadi ambapo nilitakiwa kwenda kulipia dola 450 au 350 au 250 kupata zawadi haraka itategemea umetoa dola ngapi.
Walitaka nitumie moneywire au moneygram au westernuniun. Wakasema malipo ni kwa ajili ya firmchamber law kuwalipa wanasheria. Nikawaambia kateni kwenye zawadi wakagoma! Nikawaambia mie sinashida na zawadi yenye masharti,kama hivyo wampe mwingine. Walikuwa wananisumbua sana kwa kunipigia simu,baada ya hapo nilikuwa nakata kila wakipiga.
Baada ya kuona response ni negative waliniacha hata email zikawa haziji.Walijidai wanatoka LG electronics. Niliamua kusachi kama kampuni hiyo inashindano la hivyo,nikakuta hakuna nikajua hawa ni mtapeli wa kimataifa. Kwakuwa umeshajua,nakushauli jaza hizo details ila usiwape account yoyote wala namba ya simu. Wakikujibu tujuze kila hatua.