Ni vigumu kuelewa kiundani hii saga yote kwa mapana yake kama hujaishi US.
First and foremost, weusi sio spokesman wa weupe ili wawasemee weupe shida zao and vice versa. Kila mtu atajibeba pale atapoguswa.
Ni kweli weusi wanauana sana kwenye hoods zao ila muuaji akishikwa anapigwa miaka mingi sana jela ila mzungu akiua mweusi ni kama sio kosa, he can easily get away with it. Jiulize ni kwanini.
Wakati huo huo mweusi almost kosa lolote linaweza kukupeleka jela ila mizungu haiendi kwa kosa hilo hilo.
Kuna mapolisi weusi wengi tu ila hata siku moja hujawahi sikia police mweusi kaua mtu wa rangi yeyote for any traffic violation siku zote ni wazungu wanaua tena wanaua weusi, hapo utagundua kuna motive behind this all
Utakubaliana na mimi gov imeguswa sasa baada ya kuona police wanauwawa ila mwanzo walionyesha kutokujali mauaji ya weusi hata pale ushahidi wa video ulipoonyesha dhahiri
Pamoja na hayo yote hayaondoi fact kwamba wanugu yani weusi wa America ni watu aggressive sana, attitude balaa, wagumu kucomly na chochote na hawawapendi police kabisa. Ila hayo hayahalalishi kuondoa uhai wa mtu kirahisi rahisi kama ilivyo sasa
Sababu sasa pande zote mbili zimegungwa na kusikia ule uchungu naamini kitu kitafanyika kabla hali haijawa mbaya zaidi. That being said, sisapoti mauaji ya binadamu yeyote.