Black Dahlia: Kifo cha kikatili zaidi kuwahi kutokea katika nchi ya Marekani

Jamii Intelligence imekuwa Story teller forum so sad!..
At the same time there are some constructive posts in que waiting for moderation in here!..
 
Asubuhi moja ya Januari 15, 1947, mama mmoja akiwa na mwanae katika misele ya hapa na pale jijini Los Angeles alikutana uso kwa uso na mwili wa binadamu ambao ulikua umetenganishwa katika sehemu mbili yan kiunoni.
Mwili ulikuwa mita chache tu kutoka barabarani.Kwa jinsi mauaji hayo yalivyokua ya kutisha mama yule alishindwa kabisa kuamin kama alichokua anakishuhudia mbele yake ulikua ni mwili wa binadamu,aliamin kua ule ulikua ni moja kati ya midoli inayotumika katika maduka kwa ajili ya kuuzia nguo.Kilichomshangaza zaidi ni kuwa hakukuwa na hata tone la damu hali iliyomaanisha kuwa mauaji yale yalikua yamefanyika katika eneo lingine na mwili kuja kutupwa katika eneo hilo.

Baada ya uchunguzi wa kina kufanyika chini ya shirika la FBI jijini Los Angeles iligundulika kua mwili ule ulikua ni wa mwanamke.Ilitambulika kua mwanamke huyo alikua na umri wa miaka 22 na alifahamika kwa jina la Elizabeth Short-baadaye, aliitwa "Black Dahlia" na waandishi wa habari kwa sababu ya nguo zake za rangi nyeusi na filamu ya Blue Dahlia wakati huo.

FBI walifanikiwa kuutambua mwili huo kupitia alama za vidole ambazo zilipatikana katika kumbukumbu za FBI.Alama hizo za vidole zilimuhusisha Elizabeth short katika sehemu mbili.

Sehemu ya kwanza ilionesha kwamba Elizabeth Short alikuwa ameomba kazi kama karani msaidizi katika kambi ya jeshi ijulikanayo kwa jina la Cooke huko California mnamo Januari 1943;

Sehemu ya pili Elizabeth short alitambuliwa kwa sababu alikuwa amekamatwa na polisi wa Santa Barbara kwa kosa la kutumia pombe katika umri mdogo ambao hauruhusiwi kisheria kibongobongo tunasema alikua bado chini ya miaka 18 hii ilitokea miezi saba baada ya kua ameomba nafasi ya kazi katika kambi ya jeshi.

Nazani wengi wenu mtakua bado mna maswali nini kiliendelea baada ya upererezi wa kina kuanza ni watu gan walikamatwa na kwa vipi kwa shirika kubwa la upererezi kama FBI lishindwe kumkamata mtekelezaji wa mauaji hayo ya kinyama.Siku nyingine tutaenda kumwangalia mtu ambae anazaniwa kuwa ndie alitekeleza mauaji hayo pia mtu huyu anazaniwa kuwa ndiye Zodiac killer.
Upererezi = upelelezi
 
Hatuhitaji umalizie.. Unaleta story kama muvi za bongo ili uwe na part 2 wakat unaweza maliza.
 
Back
Top Bottom