Biteko afuta likizo zote za Watumishi wa TANESCO

Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.

Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.

Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini.

Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo.

“Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliwa na changamoto ya umeme.

Hakuna likizo tena kuanzia sasa hivi kwenda mbele kwa mtu yeyote anayefanya kazi Tanesco. Nilivyosema Tanesco hamtalala wakati huu wa mgawo nilikuwa naaminisha, haiwezekani tuko kwenye changamoto halafu kuna wengine wanataka kulala.

Sisi wenyewe tunazunguka kila mahali kuhakikisha wananchi wanapata umeme. Katika hili tutachukua hatua kwa aliyeidhinisha likizo n ahata huyo aliyeomba likizo wakati huu ametoa wapi ujasiri,” amesema Dk Biteko.
Mbona ni vitu viwili tofauti au mm ndio sijamuelewa wazir?
 
Political gimmick kuendelea kuwazuga wajinga.

Hao wafanyakazi hawana uwezo wa kuondoa tatizo kuu la ufisadi na hujuma zinazofanya TANESCO ishindwe kutoa umeme wa uhakika.

Labda watasaidia katika kuendeleza propaganda zisisoisha.
 
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.

Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.

Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini.

Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo.

“Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliwa na changamoto ya umeme.

Hakuna likizo tena kuanzia sasa hivi kwenda mbele kwa mtu yeyote anayefanya kazi Tanesco. Nilivyosema Tanesco hamtalala wakati huu wa mgawo nilikuwa naaminisha, haiwezekani tuko kwenye changamoto halafu kuna wengine wanataka kulala.

Sisi wenyewe tunazunguka kila mahali kuhakikisha wananchi wanapata umeme. Katika hili tutachukua hatua kwa aliyeidhinisha likizo n ahata huyo aliyeomba likizo wakati huu ametoa wapi ujasiri,” amesema Dk Biteko.
Hawa watawala wetu ni watu wa ajabu sana. Hivi anajua ni kwa nini kunakuwaga na likizo?
 
Anataka kuleta usukuma gang kwenye mambo yenye kanuni zake.

Likizo sio hiari ya mwajiri ni stahiki ya kisheria ya muajiriwa. Asilete mambo ya udikteta uliopitwa na wakati.

Hata wakijazana wafanyakazi wote ndio umeme utawaka??
 
Hajui la kufanya bila likizo hakuna ufanisi
Yaani watu wengine ni kama ubongo wote umeondolewa. Huyu juha anajua maana ya likizo? Likizo zipo kisheria na siyo hisani ya watawala. Mtu asikosa nafasi ya kwenda likizo ufanisi unapungua na hata yeye anakuwa kwenye mgomo baridi.
 
Ujinga tu.
Badala wawe creative kutafuta permanent solutions wao kazi yao kutafuta cheap popularity tu.

Sasa ukizuia likizo ndo umeondoa tatizo la umeme nchini?
 
Ila viongozi wetu ukiwatazama na suti zao na magari na ulinzi unawaona wana akili na wa maana sana, Sasa njoo kwenye arguments na reasons zao za maamuzi utacheka ufe,

Sasa tatizo la umeme kama wanavyosema hao wenye mamlaka ni kuonhezeka kwa matumizi na ubovu wa mitambo ya kufua umeme, this means suluhu ni kuonheza uzalishaji wa umeme ili kukidhi mahitaji kwa kununua mitambo ya kufua umeme

Hivyo kwa yote hayo the only solution ni pesa na kupatikana mwa mitambo kama sababu zao ndizo uhalisia,

Sasa swali kwa biteko, likizo zinaathiri vp suluhu hizo za umeme?

Tanesco si taasisi? Kwamba akitoka bwana kasuku basi kazi haziendi?

POLE SANA TANZANIA
 
na imani kubwa na shirika la umeme

nishati itakua ya kutosha haijawahi kutokea chini ya mama akiongozwa na ilani ya chama cha mapinduzi
 
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.

Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.

Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini.

Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo.

“Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliwa na changamoto ya umeme.

Hakuna likizo tena kuanzia sasa hivi kwenda mbele kwa mtu yeyote anayefanya kazi Tanesco. Nilivyosema Tanesco hamtalala wakati huu wa mgawo nilikuwa naaminisha, haiwezekani tuko kwenye changamoto halafu kuna wengine wanataka kulala.

Sisi wenyewe tunazunguka kila mahali kuhakikisha wananchi wanapata umeme. Katika hili tutachukua hatua kwa aliyeidhinisha likizo n ahata huyo aliyeomba likizo wakati huu ametoa wapi ujasiri,” amesema Dk Biteko.
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Vipi kina mama wajawazito wanaotakiwa kwenda kujifungua?

Sikiliza Biteko, hiyo Tanesco ni usanii mtupu umejaa hapo, huu mgao ni dili tu za wajanja wafanye biashara zao, uliza ni kina hao ili uongee nao huu mchezo wa mgao uishe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Angejua hizo likizo wengine wanamalengonazo kwa maendeleo ya familia zao asingeropoka ujinga ndiyo atafanya khali izidi kuwa mbaya
 
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.

Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.

Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini.

Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo.

“Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliwa na changamoto ya umeme.

Hakuna likizo tena kuanzia sasa hivi kwenda mbele kwa mtu yeyote anayefanya kazi Tanesco. Nilivyosema Tanesco hamtalala wakati huu wa mgawo nilikuwa naaminisha, haiwezekani tuko kwenye changamoto halafu kuna wengine wanataka kulala.

Sisi wenyewe tunazunguka kila mahali kuhakikisha wananchi wanapata umeme. Katika hili tutachukua hatua kwa aliyeidhinisha likizo n ahata huyo aliyeomba likizo wakati huu ametoa wapi ujasiri,” amesema Dk Biteko.
Anataka aonekane na yeye kafanya kazi....Ila kufuta likizo sio suluhisho
 
Back
Top Bottom