Kama binadamu yeyote amejiwekea kautamadni ka kufanya besidei ni vizuri kabisa. Ni kwa visingizio hivyo mtu kama Lowasa, Fisadi wa mafisadi anaweza kuandaa sherehe kubwa sana ili kuendelea kujisafisha kwa maandalizi ya 2015. Ni aibu gani kwa viongozi wa dini kuendelea kumuunga mkono huyu bepari na fisadi!!!?? Ukweli ndiyo huu!!!
Viongozi wengi wa dini na makanisa hasa yale ambayo yanajiita ya kiroho wamejawa na tamaa sana. Wamekuwa wakiwakumbatia waumini wale ambao wanatoa sadaka na mafungu ya kumi bila kujali yametokana na nini!!! Wamekuwa wakifanya harambee na kuwaalika hawa wenye pesa hata kama ni mafisadi au majambazi huwa hawajali. Ni wazee wangapi wa kanisa ambao wamekuja kugundulika kuwa ni majambazi na pengine ni wafanya biashara wakubwa wa madawa ya kulenvya?? Wana EPA wangapi akiwemo Njake, Lukaza, Makubo (alisevu), na wengine wengi ambao wanavaa ngozi ya kondoo na kuwa mstari wa mbele kuchangia kaika makanisa na wanakalishwa pale mbele ya makanisa kwa kuwa pia wana uwezo wa kuvaa vizuri ili watu wavutiwe na kuona kuwa pengine kundi au kanisa hili linatoa watu shida maana wote wako sparkling!! Kumbe ni usanii wa viongozi wa dini/wachungaji???
Ngoja leo EDO afilisike uone kama kuna kiongozi wa dini atakuwa karibu yake!! Kwanza watajificha ili wasije wakakutana naye asije akawadai sadka yake na mafungu ya kumi. Enyi viongozi wa dini wa kileo, acheni unafiki.
Huko nyuma, mtu akigundulika kuwa hata alikuwa mlanguzi, jambazi, mwenye hawara, asiye na ndoa rasmi, etc alikuwa haruhusiwi kupata huduma za kanisa. Leo hii haya yamewekwa pembeni, wanapata huduma kama kawaida mpaka vikundi vya kwaya vyenye njaa ambavyo vikizindua albam utasikia mgeni rasmi Lowasa, mgeni rasmi hovyo kabisa, kisa wanataka waandiwe cheque!!
Na huyo Paroko wa kanisa katoliki alienda kufanya nini huko?? Wakatoliki hamko maskini kiasi hicho. Mhashamu Pengo na Kilaini mmulikeni huyu traitor!! Au askof mkuu Josephat Lebulu uko upande upi wa mafisadi??