Party la birthday lilikuwa la aina yake.
Nilikuwepo ila simu yangu ikashindwa kuwaunga live ili wana JF muone na "kujumuika nae."
Waliokuwepo ambao mimi nawafahamu ni KARAMAGI,MNDOLWA (DAWASCO),MKUU WA CHUO,TANZANIA MILITARY ACADEMY,mhubiri maarufu MWAKASEGE,FLORA MBASHA na kundi lake la nyimbo.
Waliotambulishwa na EL ni MAASKOFU WA ANGLIKANI KUTOKA ARUSHA,KILIMAJARO,MOROGORO NA MWAKILISHI WA ASKOFU MKUU ANGLIKANI TZ,PAROKO WA KANISA KATOLIKI MONDULI.
Vikundi vya kwaya mbali mbali kama RC UNGALIMITED etc.
Wengine niliowaona,ni watu ambao huwa nawaona kwenye misafara ya JK mikoani kama wanausalama(UWT)hawa walikuwa kama 10 na ndio waongozaji wa shughuli hii.
Shughuli ilianza saa 6 mchana na kuendelea na watu walikuwa wengi maana wananchi wote wa MÖNDULI walialikwa na hakuna utambulisho wa kuingia(kadi).
Baada ya mimi kuondoka around saa 11 jioni,naambiwa kufika saa moja ndo kama sherehe ilianza maana du,...........
Nimesahau kumtaja OLE NAIKO(CTI) nae alikuwepo.
Taarifa nilizopata,zinasema party la usiku lilikuwa babkubwa kwani kila aina ya kileo kilikuwepo,tofauti na mchana ambapo kulikuwa na vinywaji laini tu,pia naambiwa MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI WENGI PAMOJA NA WABUNGE WENGI WALIKUWEPO
NB.Wakati wa mchana,LOWASA HAKUMTAMBULISHI MWANASIASA YEYOTE AU MTU YOYOTE TOKA KUNDI LINGINE ZAIDI YA WACHUNGAJI NA MAASKOFU.