Binti yake Raila Odinga aiomba msamaha Tanzania

Binti yake Raila Odinga aiomba msamaha Tanzania

INA MANA KWENYE ULE MKUTANO HAKUKUWA NA MUWAKILISHI KUTOKA TANZANIA???? KAMA ALIKUWEPO ALICHUKUA HATUA GANI NA KAMA HAKUWEPO MUWAKILISHI KWANINI ILIHALI KENYA ILITOA MUWAKILISHI????

HAPA NATAKA KUSEMA KUWA WAKENYA WANAFANYA YOTE HAYA KUTOKANA NA UZEMBE WETU.....
Inawekana Tz haikuwa Na mwakilishi, angekuwepo pengine angekanusha na pengine alikuwapo lkn alikuwa hajui, tumelala sana aisee hadi aibu
 
Nimemsikilia msemaji wa serikali akilizungumzia hili suala na ndio nimegundua kuwa bado tuko mbali sana katika haya masuala. Sitaki kukubaliana na kauli ya rais wa zamani wa Kenya kuwa Mwalimu alikuwa 'anatawala maiti' maana inaumiza sana ila itatuumiza zaidi pale tutakapoigundua kuwa ilikuwa na kaukweli fulani.
Hivi ingelikuwa kwenye mtihani na huyu binti akajaza hili jibu mnadhani angalipata hizo marks!? Sasa ni kwa nini tusijiaminishe tu kuwa 'elimu ya Kenya ni mbovu' mpaka wanaopewa nafasi ya kuongea UN hawajui hata historia/jiografia ya nchi yao achilia dunia! Sina uhakika kama wengi tulifuatilia jinsi South Africa walivyotumia ubia wa ATC kujinufaisha kwa kuiaminisha dunia kuwa ukitaka kufika Ngorongoro, Serengeti, Zanzibar, Kilimanjaro nk utapelekwa na SAA. Na wanaendelea kufaidi huo 'uongo' hata baada ya mkataba kuvunjika!
Kilicho wazi ni kuwa watetezi wa nchi ni wananchi na sio wanasiasa na huyo binti katika kiwango chake anajaribu hata kushawishi watu kwa uongo ili nchi yake ijulikane. Ndio maana hata wacheza mpira wengi wa Afrika Magharibi wanazamia kwa pasipoti bandia kuingia Ulaya lakini wakishapata mafanikio wanajipambanua kulingana na nchi wanazotoka.
Sisi tutabakia kuwashutumu Wakenya badala ya kushutumu mambo yanayotudumaza kama mazuio feki ya uchaguzi wa meya kutoka mahakamani.
Isikilize hii clip:

Umesema maneno mazuri saaana ila umekosea sehemu moja, umekosea pale ulipompinga Rais wa zamani wa Kenya kuwa Watanzania ni maiti, tumsubiri Yesu aje atufufue, si umeona wakenya wa wameamka!?
 
Tuna Rasilimali nyingi saaaana, na bado tunapiga kelele kwamba mtu kutangaza bonde lipo Kenya, tunapiga kelele utadhani hilo bonde limehamishwa physically.
Tuna Milima, mabonde, Mito, Bahari, Bandari, Madini, Gas, Ardhi nzuri n.k na bado masikini. Kwanini tusionekane sisi matahira.
Ile kesi ya ziwa Nyassa ingelekwa kwa Mungu, huenda Mungu angeamua lile ziwa na Gas yote ipelekwe Malawi ili iwasaidie na sio Tanzania.
Tulishaambiwa watz ni maiti zinazotembea Na kwa matendo yetu tunathibitisha hilo,
 
Kwani kenyata si yupo Arusha kwenye mkutano?
 
Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.

''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly).

''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.

''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado
Jaguar : Nisemeje,nawaombeni radhi Watanzania.

Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na kenya

'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram.

Tamko lake kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko Tanzania lilihusiana na mada ya siku hiyo
Jaguar : cha ubinadamu'' alisema bi Odinga

Olduvai ndiko kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)

Bi Rosemary aliomba radhi baada ya kuzomewa na maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook Instagram na Twitter wakidai aliwapotosha hadhira yake na haswa ulimwengu kwa kusema eti Olduvai ipo Kenya.

Mbunge Zitto Kabwe alikuwa amechangia mada kwa kusema kuwa Tanzania sharti izinadi vivutio vyake vya kitalii ilikuzima dhana potovu.

Aidha alidai kuwa watu wanafikiria kuwa mlima kilimanjaro uko Kenya ilahali ukweli halisi upo Tanzania sawa na mwanamuziki nyota Diamond Platnumz ambaye ni Mtanzania.

====================
Good evening! I have just been reminded of an incident which occurred while attending the IYLA conference in New York, 7 months ago. There was a Freudian slip. Apparently, our brothers and sisters from Tanzania are alarmed that I have grabbed their Olduvai Gorge. In Kenya, we equally have a beautiful prehistoric site named Olorgesailie along the way to Magadi. So, poleni sana my Tanzanian brothers and sisters, your Olduvai Gorge is safe. That being said, I would like to share the entire speech. It highlighted my efforts, which mainly focus on bringing people together. Have a fabulous evening and stay blessed


My take: Binafsi naamini bado kuna watanzania wenyewe wanaamini mlima Kilimanjaro Olduvai gorge ziko kenya kwakuwa Serikali ya Tanzania haikuwahi kufanya juhudi zozote kutangaza vivutio vyake ,unlike kenya tunaona matangazo ya kenya airways na jiji la mombasa BBC na CNN, Kenya inatumia uzembe wa Tanzania kujinufaisha na sidhani kama ni kosa kwani kuna mtu yuko tayari afe na njaa ilhali chakula anakiona?

Nguvu inayotumiwa na Watanzania kutangaza vivutio vyenu ni ndogo mnooo ukilinganisha na kenya,soon tutasema mikumi iko kenya, halafu tutaappologize kimyakimya huku tayari ulimwengu ukiamini mikumi iko Kenya.

Nisieleweke vibaya jamani ila soon tukipata platform ya kuaddres kimataifa hatutakata tamaa kusema Mikumi iko Kenya manake najua hizi nafasi Watanzania hawazipatagi sijui kwanini tunazipataga sie tuu

Thank u

falcon mombasa


Kenya is bulldozing us in tourism and advertise all what we have as theirs,we Tanzanians are quite and take it easy,,,,,,It isn't acceptable we need to do aggressive advertising of our national parks etc
 
Mimi nitakubali ombi la msamaha huo kama atatumia jukwaa hilo hilo alilotumia kupotosha kurekebisha upotoshwaji huo. Vinginevyo...bado namuonda 'adui' namba moja juu ya rasilimali yetu ya Olduvai Gorge.
 
Sasa wewe mikoa ya Arusha ndiko kunapatikana hivyo vivutio
Na Nyie CDM mnaishikiria mikoa hiyo
Mmefanya lipi kuitangaza!!
Kazi yenu ni kwenda ulaya Na totoz kwa kisingizio cha kutangaza utalii, huo utalii mnoenda kuufanya Na totoz ni wa aina gani magamba nyie
 
Sasa wewe mikoa ya Arusha ndiko kunapatikana hivyo vivutio
Na Nyie CDM mnaishikiria mikoa hiyo
Mmefanya lipi kuitangaza!!
Arusha ndio inapewa fungu la kutangaza utalii wa nchi? Tuliposema tunataka nchi iendeshwe kwa majimbo tuliona mabali tulijua serikali dhaifu ya ccm imeshindwa kuongoza nchi, lakini kwa ulafi wenu mkakataa na kusema nchi haiendeshwi hivyo, leo unatoka wapi kuhoji mkoa kuendesha shughuli za wizara? wapeni kazi ya kutangaza vivutio ASKARI maana wamegeuzwa mazombie wa ccm.
 
Inakera sana hawa jamaa inabidi waelezwe haya mambo ya kutaja vivutio na vitu vingine kuwa vipo kwao si mara ya kwanza, itafikia wakati Watanzania tutashindwa kuvumilia. Kwanza hapo hajaomba msamaha anatakiwa aite waandishi wa habari na afute kauli yake kwa sababu alikusudia kutamka hayo.
 
Kuomba msamaha kwenye instagram bado anatudhalilisha sana. Haiwezekani ametamtamka officially alafu anakuja kuomba msamaha rejareja. Alitakiwa kwenye moja ya mikutano kama hii ya east africa aombe msamaha huku baadhi ya hao waandishi wa habari walio kuwepo kwenye mkutano huo wakiwepo
Naunga mkono hoja mkuu angoja mkutano mwingine aombe radhi hiyo haitoshi kabisa
 
Mambo kama haya Ukawa wanachangia kwa kuhamasisha wananchi waandamane badala ya kufanya shughuli za kimaendeleo
 
Haya yote yanatokana Na uongozi mbovu wa serikali ya CCM, badala ya kufanya vya maana wako bize Na upinzani, chama na serikali vya ovyo sana kuwahi tokea duniani
Wewe umefanya nini? Kama si kukalia umbeya tu hapa jf. Nyumbu bwana bure kabisa. Jiulize wewe kwanza.
 
kama ameomba msamaa basi nimemsamahe kwa sharti kwamba aolewe na mtoto wa magufuri kwa kuwa anaipenda sana tanzania eheee heee
 
Ukweli huu hapa wajameni.
 

Attachments

  • OLDUVAI GORGE.png
    OLDUVAI GORGE.png
    261.5 KB · Views: 32
Wewe umefanya nini? Kama si kukalia umbeya tu hapa jf. Nyumbu bwana bure kabisa. Jiulize wewe kwanza.
Taratibu acha hasira, kupitia hili tunawataka msimame kwenye nafasi nzenu, mnatia aibu hadi tuliambiwa maiti zinazotembea, mbaya sana
 
Back
Top Bottom