Binti wangu wa kazi ni mjamzito; nifanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti wangu wa kazi ni mjamzito; nifanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kaunga, Aug 23, 2012.

 1. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Karibia mwezi umeisha msichana wangu akilalamika juu ya kuumwa na tumbo. Kazi yangu inanifanya niwe on the road almost 25 days of the month; hivyo amekuwa akienda hospt mwenyewe. Kama majuma mawili yaliyopita, alinifuata chumbani huku akilia akisema anaumwa sana, akaniletea cheti cha hospt, nikakuta amepimwa vipimo vingi including VDRL which was non reactive, ila mkojo ulikuwa na a lot of pus cells. Aliandikiwa sindano (sikumbuki jina) kama 7 hivi lakini alichomwa 5 na wakambadilishia dawa na kumpa ma Doxy ambayo yalimshinda kwani si mlaji mzuri, kwa kuwa nilikuwa nasafiri; nikamwambia aache hizo dawa anisubiri mpaka nitakaporudi.

  Nimerudi juzi, jana nikampeleka govt hosp; majibu ya mkojo na vaginal swab yalikuwa okay, again VDRL was unreactive; walivyomwangalia uke (alikuwa analalamika ana vidonda) wamesema it is okay???; baadaye dr akaandika afanyiwe utra sound kuangalia pelvic infection, ndio natoka kwenye utra sound, matokeo ni kazygote ka 8 weeks.

  Sijaongea naye chochote, na honestly sijui cha kuongea naye. Ni binti ambaye nimekaa naye kwa miaka kama 4 hivi, kitu ambacho nina uhakika nacho ni kuwa siwezi lea mtoto wake; kwani kazi yangu sio friendly na parenthood. Kingine ninacho ogopa ni the fact kuwa ndani ya miezi hiyo miwili alikuwepo mdogo wangu wa kiume aliyekuja field; huenda walijioa ninavyokuwa safarini.

  Nishaurini ndugu zangu how do l first start councilling her, halafu namuulizaje kuhusu huyo aliyemmimba na mwisho ninamsaidiaje?

  New updates
  Wakati tunakula, ameanzisha maongezi yeye mwenyewe kwamba wali unamshinda. Nikapata nafasi ya kuanza kumuuliza kiutani (huwa ninamtania) kwamba ni nani mwenye bahati; akaguna. Kisha nikamuuliza huyo mtu ameshajua, akanod; nikamendelea kumprobe amesemaje, akainama huku machozi yakimlenga; nikamuuliza amekwambia muitoe? akasema ndio.
  Nikamuuliza kwanini, akasema hajajiandaa na kwamba anaishi kwao bado (ni dreva wa mtu binafsi).

  She is into deep thinking naye anawazia kuitoa, kisa hataweza kufanya kazi na hivyo ataishije. Baada ya kuongea naye sana, anasema mama wa huyo kijana ni nurse; nimemwambia nikirudi nitaongea naye, lkn bado ni mnyonge nafikiri akili yake kubwa iko kwenye kuutoa huo ujauzito. Ngoja niendelee kumcouncil, nipo naye hapa chumbani ananiuliza kwani akitoa atakufa.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  how old is she?
   
 3. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Weka picha kwanza tumwone
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Pole sana.

  Kosa ulilofanya ni kutompa 'induction' kuhusu maisha yako na matazamio yako kwake.
  Ongea nae, muulize nani muhusika. Kama ni mdogo wako angalia jinsi ya kumuwajibisha kama ni kwa kumtafutia kibarua ili aanze kulea familia. Lakini husisha wazazi wenu. Kama ni kijana wa mitaani, ongea na wazazi wa binti ili wakushauri uwasaidieje kuwajibisha mkwe wao mtarajali. Mchuma janga hula na wa kwao, binti arudi kijijini akaanze maisha ya utu uzima.

  Next time wifi yangu, ukipata maid hakikisha ana miaka 18+. Mpe somo kuhusu ukimwi, kubakwa na jinsi ya kujilinda (mfano ukaribishaji wa watoto wa kiume nyumbani wakatinwewe haupo ni recipe ya kubakwa na ukimdaka kazi hana). Mie humueleza maid hata mwenzi wangu ama ndugu yangunakikutaka niambie nitakulinda, na namaanisha. Napenda niwe boss rafiki, so any challenges unaweza kushare. Ila sumu ya nyumba hii ni mimba, ukidaka tuuu unarudi kwenu ukaanze kujitegemea kama kwa kilimo ama vipi. Hapo unakuwa na almanac yabkueleweka, yakitokea mnafanya reference. Namuhofia juu ya ukimwi zaidi kuliko mimba.
   
 5. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Binti wa kazi...daaaaah!!!
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Nafikiri kati ya 20 na 23
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ulimpata pata vipi?
  ni lazima umuulize pia anafikiria nini now that ni mjamzito
   
 8. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Pole sana, nilipatwa na tatizo kama hili, lakini mimi hakuumwa ila nilihisi kuwa hayuko sawa kwani alinenepa na alikuwa kila mlo mezani lazima kachumbali+ndimuuuu ziwepo. nilimpeleka hspt, nikamwambia daktari ninataka apimwe nini na kwasababu gani, kwani nami nilihisi bwanamdogo ndo amefanya kazi kwani nami muda mwingi nasafiri.
  alipogundua ni mimba alitikisika sana , so ni daktari ndo aliniita na kunishauri ...... lakini ni yafuatayo yalifanyika
  1. nilikuwa friendly , sikuonyesha kuwa ni kosa kubwa , so akawa huru
  2. nikamwuliza mimba ni ya nani, kama baaada ya sku 3 hivi, aliniambia kuwa nirafiki wa dogo wangu
  3. kwakuwa alikuwa health, wakati nagundua ilikuwa ni miezi 4, so nilikaa nae mpaka mwezi wa 7. niliongea na mama yake kwa simu, alikuwa mkali hakufurahia, lakini nikaongea na dada yake na shemeji yake ( mume wa dada). niliwaeleza jinsi ambavyo waki react huyu binti atapotea. walielewa. nilimrudisha kwa kumlipia nauli, nilimpa pesa kama laki na nusu na kiroba cha mchele. alifika kwao alijitungua, aliendelea kuwasiliana na mimi. na sasa ninaitwa babu kwani nina mjukuu wa miaka 7 sasa.ilikuwa ni ngumu kwangu kwani i was single. so majirani wanaona Hg mjamzito na baba mwenye nyumba ni jokeli.
  ila huyo mwenye kufanya hiyo kazi aliiingia mtini

  ninafahamu huwezi kulea mwanae, aidha sasa uhesabu kuwa hutamtumia tena kama mfanyakazi kwa hali hii. lakini ni vema ukatumia historia jinsi ulivyoishi nae ktk kumuongoza ktk hili
   
 9. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Binti yako wa kazi hujui umri wake? Wow.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  na mimi nilitaka uliza hivyo hivyo

  halafu how old nae huyo mdogo wako wa field...?
   
 11. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mdogo wangu mimi?
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ha ha haaa sorry
  mdogo wake Kaunga wa field
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Kuhusu kuongea naye, nimeongea naye saana tu. Na nilipanga nimuendeleze kielimu baada ya kunisimulia historia yake (baba yake alimwambia afeli mtihani kwa kuandika madudu kwenye mtihani wa darasa la saba; kama ulishasikia wazazi wa Kibondo wanavyofanya).

  Nina wasiwasi na mdogo (cousin) wangu, coz alishamsimulia niece wangu kwamba HG wangu alikuwa anampigia simu usiku wa manane hadi mdogo wangu akatofautiana na girlfriend wake. She (my maid) is very seductive, nilimchukua toka kwa kaka mmoja tunayefanya naye kazi baada ya kile alichokiita kutegwa na binti; ndio maana nahisi my cousin could not resist her, na ukizingatia ni kazuri!

  Wasi wasi wangu hatasema ukweli, na pia ninaanza kuwa na mashaka maana kesho tu nitasafiri; hakawii kutoroka baada ya kuniliza.
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Nilipewa na mkaka wa ofisini, baada ya kuona anaweza kumsaliti mchumbaye aliyekuwa shuleni (binti alikuwa anamtega kwa madai ya huyo kaka)
   
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  She is 22; nilichokuwa najua she is over 18
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Bwana mimi sijui, ila anaingia 3rd year
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  pole kaunga....

  Zungumza na huyo binti kwa upole na upendo akutajie mwenye mzigo ni nani....

  Ukishamjua (awe mdogo wako au mtu wa nje) uwasiliane nae kujua what next.....

  Anaweza kuendelea kukaa hapo mpaka mwezi wa 7 msaidie vyote vya muhimu arudi kwao kujifungua..... Au
  Kama mwenye mtoto ni mdogo wako then zungumza na wazazi na mhusika jinsi nduguyo atakavyomlea mtoto.....

  Then baada ya kujifungua unaweza kuangalia kama atarudi kufanya kazi au vipi....
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mdogo wako wa kiume how old is he?
  walibaki peke yao kwa siku ngapi?
   
 19. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Aisee nashukuru sana kwa ushauri na kushare experience yako. Je niongee naye leo au niache siku zipite kidogo?
   
 20. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Yaani kwa hiyo miezi 2 ambayo mdogo wangu alikuwepo, kama nimekaa sanan nyumbani ni siku zisizozidi 5, so muda wote walikuwa peke yao. Huyo cousin wangu anaingia 3rd year chuo, so he must be over 23
   
Loading...