Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

Hivi kwani kesi nyingi bongo zinachukua siku nyingi? hebu fikiria hii ya kutoka NOV to Jan 25...Hivi ndio kesi nyingi mahakim wachache au mahakam chache? Nionavyo mahakim wanafanya kazi masaa 2-3 a day...labda md mwingine wanakwenda kubukua...kweli kazi zipo nyingi...na Karume kwa kujua mtindo wa mahakam za Bongo ndio maana anashangaa kwann kesi imewekwa mbali kiasi hicho...mie nilichojifunza ktk Kesi hii ni Mambo ya KIKE...angalikuwa hakim mtu mume asingefanya vile...hopefully itasolved within bila gazeti kujua...
 
Kuna Taarifa kuwa Rais wa Chama Cha Wanasheria Nchini (TLS),Ndg Joaquine De-Mello Leo Alhamis - 22/11/07, amemwandikia barua Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Mh.Sivangilwa Mwangesi na kumtaka afanye Uchunguzi Dhidi ya Wakili Fatma Karume,kutokana na tabia ya wakili huyo ya Ubishi na kutokuwa na Heshima ktk maeneo ya Mahakama,imeelezwa kwamba si mara moja Wakili Fatma amekataa Mahakimu ktk kesi zake,na mara nyingine amekuwa anathubutu kupanga tarehe za kesi bila kujali utaratibu wa Mahakama,Wakili huyo ameweza kuwathalilisha Mahakimu kwa kuwatishia kuwaharibia na kuwafukuza kazi.

Malalamiko ya Msingi yaliwakilishwa TLS na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Mh. Addy Lyamuya,Mh. Hakimu huyo alisema ktk barua yake kwamba "Tabia ya Wakili Karume haiwezi kuachwa iendelee" ktk kuelezea malalamiko hayo ametaja majina ya watu kadhaa kama mashahidi.Waliotajwa kwenye Waraka wa Mh. Lyamuya ni Jerome Msemwa,Jabir Mkongo,Juma Magota na Derick Ngoro na wote kwa wakati Tofauti wamekubali kutoa ushahidi wao.

Kwa mujibu wa Ndg De-Mello TLS inasubiri Taarifa na Uchunguzi wa Mh.Mwangesi ili Chama kichukue hatua za kinidhamu dhidi ya Mwanachama wake, Wakili Karume.
 
Huyu Hakimu Fatma Autiwe Kufnya Sheri Kwa Muda Kwenye Mahakama Zinazotaka Ustaarabu...kama Anataka Mambo Yta Kutaka Kuonekana Royal Family Au Untouchables ..akafanye Sheria Kule Unguja ..amabako Wamezoea Kunyenyekea Watu....kwanza Hata Huyo Babu Yake Hakuwahi Kuheshimu Sheria ..alizoea Ubabe...so Bado Wana Hizo Chembechembe...
Kaka Yake Fatma Kwa Jina Abeid Aliwahi Kutiwa Mkongoto Na Askari Mmoja Kutoka Bara Aliyekuwa Kule Baada Ya Kumuoneshea Alama Ya Dole La Kati....yule Askari Hakuangalia Akamtia Adabu.....
 
Wabongo bwana... uchunguzi utakamilika, hela itatembea, mashaidi watapatiwa kitu kidogo.

Mambo poa. Tunaendelea....

Kuna maswaliiiiii?
 
Kishoka what kind of principles are you talking about our "BANANA REPUBLIC's" judicial system; a corrupted system; i pray if i was on such a position of karume's daughter, i cud have done the same! kos no principles! do you believe that these guys and gals (mahakama judges) are counting far away dates because they are occupied? No, is only that they cannot solicit bribe from karume's daughter! OUr judicial system is equally as rotten as karume daughter! A little case like this can take 5 years why?

IO, (and Nyani for that case!)

Principles are there written through constitution, laws of the land and oath taken by those who are to given mandate to administer the law.

What happend in this case, is not absence of laws to protect the magistrate (principle) but fear of backlash from wakubwa. Had it been another noname lawyer, he/she would have been fined and spent a night in jail.

So it is not about Banana Republic having no laws, but Banana Republic where rich, famous and political connection is above law.

If the reputation is that Miss. Karume is famously known to bully the court administrators, then the problem is not the principles that govern our court and judicial system rather is the executors of these laws and principles. I am sure that each lawyer is registered and has to abide to certain rules and conducts.

If Miss. Karume is abusive of her pledge to respect the courts, then she deserve suspension from the governing body such as Tanzania Lawyers association, in addition to fines from the court system.

However, the question becomes, what sort of influence does Miss. Karume has to be bold enough to do what she desire with no respect to rules and principles of conduct?

What she told Lyamuya was a threat and degrading. She clearly showed Wananchi that she is above the law and she is not bind to follow the proper protocol. If I were the Chief Justice I would have had Miss. Karume CENSORED and FINED, even suspend her license for abusing a court officer.

That is why I stated that we have principles, however people are fearful of executing their jobs effectivelly for fear of being fired or get demoted and sent to Malampaka!

What Mwanakijiji is standing for as Kada and Nyani are questioning him is foundation of principles for any job. be Mwalimu, Mjakazi, Kuli or Mbunge. Never ever bow to any degradation just simply because fulani ni Mkubwa!

Ndio maana nimesema, mnamhoji mtu mwenye msimamo kufuata sheria, ni sawa na kulea uozo wa wanaotumia mabavu!
 
Hivi hapa wa kulaumiwa nani? mimi ningekuwa ni bosi wa yule hakimu ningemrudisha shuleni akapigwe msasa maana hajui kazi yake, na wala hawezi kuwa jasiri ingawa amepewa uwezo na serikali, yuko pale kuhakikisha haki inatendeka .Sasa yeye kushindwa kukemea kile kitendo cha wakili ni wazi hakimu hawezi kazi yake, sasa tunategemea huyu hakimu atakuwa na authority yoyote na uwezo wa kuhakikisha haki inatendeka na washtakiwa wanapewa haki zao au adhabu zinazowastahili?

Wengine tulisoma na watoto wa vizito kishenzi, lakini headmaster wetu alikuwa haelewi nani mlalahoi nani mtoto wa mkubwa, ukileta ujinga hata kama baba yako mwinyi ulikuwa unapata vibao na suspension juu na wala sikuwahi kusikia mtu amemgusa huyo headmaster kwanza heshima alipewa vile vile.

Huyo hakimu kilaza huyo, wamchape viboko kabisa. Na mimi ningekuwa hakimu bongo ningemchapisha viboko huyo sijui wakili sijui fatma karume mimi sielewi.

Pedro,

You read my mind on this when I responded to Kada. may be I should have used Kiswahili kama ulivyotumia hapa, labda Nyani asingekuja mbogo kudai nami nina kikorosho!

Ulichosema ni dhati. UJASIRI, huo haupo ndio maana I stated people protecting rotten mentality that fear famous and supremacy!
 
Pedro,

You read my mind on this when I responded to Kada. may be I should have used Kiswahili kama ulivyotumia hapa, labda Nyani asingekuja mbogo kudai nami nina kikorosho!
Ulichosema ni dhati. UJASIRI, huo haupo ndio maana I stated people protecting rotten mentality that fear famous and supremacy!

Sasa hiyo ni dharau! What are you trying to insinuate here...that I don't know/ understand the English language that well..? Alrighty then...

My (and perhaps Kada's) question was simple and straighforward that needed a little bit of clarification and that should have been it (at least as far as I'm concerned)
 
True,
Huu ushahidi ni wa upande mmoja ila i hope b'dae tutaweza kumsikia Fatma Karume's side!!
Lets wait n see before we make our decision on this!
 
Ndugu zangu wana JF tusimsakame ndugu yetu aliyesema kuwa mawakili ni maofisa wa mahakama!! Aliyoyasema ni ukweli mtupu. Kwa mujibu wa sheria ya mawakili inayoitwa Advocates Act mawakili ni maofisa wa mahakama kuu na hivyo automatically wanakuwa maofisa wa mahakama zote za chini. Kifungu hikki nimewawekea hapa chini ili mkisome na kuelimishwa!!!

ADVOCATES ACT (CAP 341)
Section 66: Any person duly admitted as an advocate shall be an officer of the High Court and shall be subject to the jurisdiction thereof.
 
True,
Huu ushahidi ni wa upande mmoja ila i hope b'dae tutaweza kumsikia Fatma Karume's side!!
Lets wait n see before we make our decision on this!

Dmussa mimi naungana na wewe kwamba tusiwe watu wakukimbilia kutoa hukumu kabla ya kusikiliza upande wa pili yaani wa Wakili Fatma.
Vilevile nadhani wengi wa wachangiaji hawamtendei haki Wakili Fatma kwa kuhusisha suala lake na siasa au familia yake. Kama tunapigania uadilifu basi uanzie kwa wana-JF kwanza. Si vema tukamwona Wakili ana hatia wakati hatujapata maelezo ya kina toka pande husika.
 
WAKILI FATMA KARUME AZUNGUMZA KUHUSU KERO ZA MAHAKAMA YA KISUTU

BINTI wa Rais, Amani Abeid Karume, ambaye ni wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, anayedaiwa kufanya fujo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam juzi, ameibuka na kueleza kusikitishwa kwake na madai hayo huku yeye mwenyewe akitoa tuhuma nzito za rushwa dhidi ya mahakimu wa mahakama hiyo.
Fatma alitoa tuhuma hizo wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima jana jioni wakati alipotakiwa kueleza kile kilichotokea katika mahakama hiyo juzi na uamuzi wake, baada ya Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) kutoa tamko la kusikitishwa na tukio hilo na kutaka uchunguzi ufanyike.

Wakili huyo, alisema baadhi ya mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wanajihusisha na vitendo vya rushwa, jambo aliloeleza kuwa alikuwa tayari ameshalitolea malalamiko yake rasmi katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Akizungumzia matokeo ya mzozo wake huo wa juzi, Fatma alisema alikuwa tayari kukabiliana na hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu tu ya kupigania haki anayoamini alidhulumiwa katika misingi isiyofaa.

"Niko tayari hata kufutwa uwakili. Natetea haki yangu ambayo naamini nilinyang'anywa, nimeingia kufanya kazi hii kwa sababu ya kutetea wananchi, hivyo siwezi kuona nikidhulumiwa nikanyamaza kimya. Enzi za utumwa zilishapitwa na wakati, ni bora nikalime nazi kuliko kupoteza haki yangu," alisema Fatma kwa kujiamini.

Alisema hata kama yeye ni mtoto wa rais, bado anayo haki ya kudai kile anachodhani anadhulumiwa, kwani naye ni mtu kama walivyo watu wengine, na kimsingi akakataa suala lake kuhusishwa na urais wa baba yake.

Kuhusu kuwapo kwa rushwa, binti huyo wa Rais wa Zanzibar alisema anao ushahidi wa kutosha unaomuonyesha mmoja wa mahakimu waandamizi wa mahakama hiyo akiomba rushwa kutoka kwa mteja wake, Sadiq Walji.

"Ninao ushahidi wa uhakika hakimu (alimtaja jina), aliomba rushwa (akataja kiasi cha fedha zilizoombwa na hakimu huyo)…tena alimfuata mteja wangu katika Hoteli ya Sea Cliff Agosti 26 mwaka huu, na alimpatia fedha na akamrekodi bila ya yeye kujua 'tape recorder' (kinasa sauti). Hili ushahidi wa sauti yake tulishauwasilisha Takukuru na wamelifanyia uchunguzi kwa muda mrefu.

"Nasema hivi, Mahakama ya Kisutu inanuka rushwa. Inahusisha mahakimu na waendesha mashitaka. Rushwa imetawala pale, tena huyo hakimu kesho (leo) anapelekewa barua yake…mimi siyo mwehu hata kidogo, nasema hili kwa uhakika na serikali na watu wote wajue kuwa Mahakama ya Kisutu pana rushwa kila mahali," alisisitiza wakili huyo wa kujitegemea.

Akizungumzia madai ya kufanya fujo ndani ya mahakama wakati kesi inaendelea, wakili Karume aliyefika kwa ajili ya kumuwakilisha Walji, kwenye kesi namba 60/2006 ya madai ya mtoto wa miaka miwili iliyokuwa ikisikilizwa mbele ya Hakimu Mwandamizi, Addy Lyamuya, alisema hakimu huyo alimkosea, hali iliyosababisha malumbano.

Alisema, Hakimu Lyamuya alitaka kuipanga kesi hiyo tarehe za mbali bila sababu za msingi, jambo ambalo wakili Karume alipingana nalo kwa kuwa Hakimu Adolf Mahay, alikwishatoa uamuzi Agosti mwaka huu kuwa mtoto huyo wa mteja wake anayeishi kwa Saeeda Hassam , awe akiruhusiwa kila Ijumaa kwenda kwa baba yake na kurudishwa kwa mama yake Jumapili.

Fatma alisema licha ya uamuzi huo, mama wa mtoto huyo alikuwa akikaidi amri hiyo, hali ambayo ilimfanya yeye awasilishe ombi la kutaka mwanamke huyo achukuliwe hatua za kisheria kwa kosa la kuidharau amri halali ya mahakama hiyo.

"Licha ya kumuomba hakimu aipange leo, alikataa na kunijibu kwa ukali na akanionyeshea kwa ishara kwamba mimi ni mwendawazimu….nikamuuliza, madaraka hayo nani kampa ya kunionyeshea kwa ishara mimi ni mwendawazimu? Akaanza kuniambia nisimpangie kazi…nikashikwa na hasira na kutoka mahala nilipokuwa nimesimama na kumwambia zama za utumwa zilishapita katika nchi yetu, hivyo siwezi kukubali kuona navunjiwa heshima nikanyamaza kimya na nikamweleza kabisa nakwenda kumshitaki kwa wakubwa wake wa kazi.

Alisema baada ya kumweleza maneno hayo, hakimu alikwenda kumshitaki kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangesi na pia alikwenda kumshitaki kwa Jaji Kiongozi Amir Manento lakini hata hivyo alisema malalamiko yake hakuwa ameyapeleka kwa viongozi hao kwa maandishi.

"Licha ya kumweleza yote haya, hakimu hakutaka kunisikiliza na badala yake akanionyeshea kwa ishara kwamba, mimi ni mwendawazimu….ndipo nilipomweleza kwamba hawezi kazi na kwamba naenda kumshitaki kwa wakubwa wake wa kazi," alisema Karume.

Fatma alisema pia kuwa, juzi asubuhi alikwenda kumshitaki Lyamuya kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangesi, pia alikwenda kumshitaki kwa Jaji Kiongozi, Amir Manento, lakini hata hivyo alisema malalamiko yake hakuwa ameyapeleka kwa viongozi hao kwa maandishi.

"Habari zilizoandikwa jana kwakweli zimeniumiza sana…kwani Lyamuya aliniita mimi mwendawazimu na mbaya zaidi, Mahayi anasema kwamba alijitoa kwenye kesi ninayoitetea kwa sababu nilimfokea. Haya mambo si ya kweli," alisema Fatma katika mahojiano jana.

Katika tukio la juzi, Fatma alikuwa akituhumiwa kutoa maneno makali dhidi ya Hakimu Lyamuya, hali iliyodaiwa kusababisha hakimu huyo ajitoe kuendelea kusikiliza kesi inayomhusu mwanasheria huyo.

Tukio hilo la aina yake lilitokea katika chumba cha mahakama, wakati hakimu huyo alipotaka kuanza kusikiliza kesi ya madai namba 60/2006 ambayo ilianza kujadiliwa na hakimu huyo juzi hiyo kwa mara ya kwanza, tangu apewe jalada hilo.

Katika kesi hiyo, Fatma anamwakilisha Sadiq Walji, ambaye ni mdaiwa katika kesi hiyo ya madai ya mtoto. Mdai katika kesi hiyo namba 60/2006 ni Saeeda Hassam.

Kabla Hakimu Lyamuya kuanza kusikiliza kesi hiyo, Wakili Fatma, aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi kesho, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo.

Kutokana na hali hiyo, hakimu alimtaka karani wake kuangalia kwenye kitabu cha kumbukumbu (diary) kama siku hiyo itafaa kusikilizwa kwa shauri hilo. Hata hivyo, karani alimweleza hakimu kuwa siku hiyo zimepangwa kesi nyingi za kusikilizwa, labda waipange Januari 13, mwakani.

Kwa mujibu wa taarifa za juzi, Hakimu Lyamuya alikubaliana na maelezo ya karani wake na kumweleza wakili huyo kwamba kesi hiyo itasikilizwa tarehe hiyo.

Baada ya hakimu kupanga tarehe hiyo, Wakili Fatma anadaiwa kuwa alianza kufoka kwa sauti ya juu akitaka mahakama isikilize kesi hiyo jana jambo ambalo Hakimu Lyamuya alilikataa kwa kueleza kuwa hakuwa na nafasi.

Wakili huyo aliendelea kuomba mahakama kupanga kesi hiyo Januari 2 mwakani, ombi ambalo hakimu huyo alilikataa na kumweleza tarehe hiyo mahakimu watakuwa mapumziko, ndipo wakili huyo alipoanza kutoa kauli kali dhidi ya hakimu huyo.

"Kwanza wewe hujui kazi na ni mara yako ya kwanza kuniona mimi… hunijui ni nani, sasa nitakuonyesha… nitaandika barua kwa wakubwa wako wa kazi na kuwaeleza kwamba hujui kazi," alidaiwa kusema Fatma hiyo juzi.

Kutokana na tafrani hiyo, mahakama ilishindwa kuendelea kusikiliza shauri hilo wala kulipangia tarehe na badala yake jalada la kesi lilirudishwa kwa uongozi wa mahakama hiyo, ili limpangie hakimu mwingine kusikiliza kesi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tafrani hiyo juzi, Hakimu Lyamuya, alisema ameshangazwa na vitendo vya utovu wa maadili vilivyoonyeshwa na wakili huyo na kueleza hajafikiria kuchukua uamuzi wa kumfungulia kesi.

kutoka; Tanzania Daima. 23.11.07
 
IO, (and Nyani for that case!)

Principles are there written through constitution, laws of the land and oath taken by those who are to given mandate to administer the law.

What happend in this case, is not absence of laws to protect the magistrate (principle) but fear of backlash from wakubwa. Had it been another noname lawyer, he/she would have been fined and spent a night in jail.

So it is not about Banana Republic having no laws, but Banana Republic where rich, famous and political connection is above law.

If the reputation is that Miss. Karume is famously known to bully the court administrators, then the problem is not the principles that govern our court and judicial system rather is the executors of these laws and principles. I am sure that each lawyer is registered and has to abide to certain rules and conducts.

If Miss. Karume is abusive of her pledge to respect the courts, then she deserve suspension from the governing body such as Tanzania Lawyers association, in addition to fines from the court system.

However, the question becomes, what sort of influence does Miss. Karume has to be bold enough to do what she desire with no respect to rules and principles of conduct?

What she told Lyamuya was a threat and degrading. She clearly showed Wananchi that she is above the law and she is not bind to follow the proper protocol. If I were the Chief Justice I would have had Miss. Karume CENSORED and FINED, even suspend her license for abusing a court officer.

That is why I stated that we have principles, however people are fearful of executing their jobs effectivelly for fear of being fired or get demoted and sent to Malampaka!

What Mwanakijiji is standing for as Kada and Nyani are questioning him is foundation of principles for any job. be Mwalimu, Mjakazi, Kuli or Mbunge. Never ever bow to any degradation just simply because fulani ni Mkubwa!

Ndio maana nimesema, mnamhoji mtu mwenye msimamo kufuata sheria, ni sawa na kulea uozo wa wanaotumia mabavu!

Nadhani umefika wakati wa wachangiaji kuacha kuandika habari za kufikirika, je unaweza kutuambia unamfahamu vipi Wakili Fatma? je ni mtu wa namna gani?
 
Wakili Fatma kazungumza kwa kirefu sana na redio Clouds FM.
Kaweka wazi mambo mengi. Nimesikiliza sehemu tu, kwa waliopata nafasi ya kusikiliza mahojiano yote wanaweza kutuhabarisha zaidi.
 
Hakika nakubaliana na binti Karume Mheshimiwa hakimu Lyamuya hajui kazi hawezi hata kutumia sheria zinazomlinda yeye na mahakama kumuadabisha mtu anayedharau mahakama au sheri hiyo hakuna kama ipo inatumiwa kwa akina nani? au wakili binti Rais yuko juu ya uwezo wa mahakama ya kisutu? kama hivyo ndivyo basi kesi hiyo ihamishiwe mahakama kuu tukapime na ubavu wa waheshimiwa MAJAJI na huko akipandisha mzuka asiamuliwe aachwe amnase vibao jaji kumfundisha kazi. hata tamthilia ya the long wait inonyesha uwezo wa mahakama kumbe kisutu NYAU ukioroma inakimbilia jikoni kutafuta mashahidi

KAUSHA mi naona ungekaush tu. hii kali halafu eti kuna watu humu wanamtetea. sisi hatujui kama kulikuwa na ishu ambazo kimsingi ndo zilizopelekea amfokee hakimu. kwa macho ya kawaida kama jamii kilichoonekana ni dharau yake kwa mahakama na hakimu. kama kulikuwa na ishu za haki angefata utaratibu au hata kumshtaki huyo hakimu kama angetaka lakini sivyo alivyofanya. halafu tufikirie tu kikawaida kama angekuwa ni wakili wa kawaida, mtoto wa nobody kutoka bunchari huko, you already know what would have happened. Anyway hata huyu hakimu naye hata kujua haki yake kama hakimu, anaogopa mafisadi. hivi kama angemuweka lupango wangemfanyaje.? ningekuwa mimi ningemtupa ndani na kuiweka hadharani kwenye media kutest zali.
 
Kuelewa lugha ni kitu muhimu, ukiangalia kwenye kiingereza neno Officer linatafsiriwa kama 'a person holding a position of authority'. Tukirudi kwenye mada yetu kwenye legal profession:



Kwa maana hiyo kuwa ofisa wa mahakama kuu hakumpi uhuru au uwezo wa kuwa na authority kwa jaji na maendeleo ya taratibu za kimahakama. Yeye anakuwa msemaji na authority yake inaishia kwenye kutetea mteja wake na siyo vinginevyo. Vile vile ni lazima afuate taratibu zilizowekwa kama inavyoonyesha hapo juu. Uofisa wake hauna mamlaka yoyote katika utendaji na uendeshaji wa shughuli za mahakama.

Je, unakubali kuwa mawakili ni maofisa wa mahakama?
 
Wakili Fatma kahojiwa leo na CLOUDS FM.

Alichozungumzia ni kwamba hakimu wa kwanza alitakiwa kutoa court order kwa baba wa mtoto ili aweze kumuona mtoto wake once a week. wakili alidai rushwa kwa mara tatu mfululizo ndio atoe hiyo court order kama nilimuelewa vizuri.

Mara ya mwisho hakimu alimpigia huyu mteja wa wakili Fatma ili wakutane sea cleaf na kumuomba rushwa. mteja wa bi Fatma alimlikodi na mazungumzo tumeyasikia live Cloud's asubuhi hii.

Baada ya hapo Wakili Fatuma aliyapeleka malalamiko yake PCCB pamoja na tape recorder aliyolikodiwa hakimu (Sikumbuki jina lake) na hakimu akajitoa kwenye hiyo kesi.

Kesi ikakabidhiwa kwa Hakimu mwingine naye alijitoa siku ya kwanza tu ya kuanza kusikilizwa kesi baada ya wakili Fatma kumwambia wakili wa upande wa pili kuchelewa kufika na alipofika akatoa shukurani kwa wakili Fatma na binti akamwambia usinishukuru mimi kwani nilikusubiri kwa dakika 20 tu na kutaka kesi ianze ila hakimu ndio alisema hawezi kuendesha kesi bila ya wewe. HAPO HAPO HAKIMU AKASEMA NIMEJITOA KWENYE HII KESI.

kesi ikakabidhiwa kwa Hakimu mwingine. Ambaye ndio huyu ambaye mtafaruku ulitokea.

Inavyoonekana ni kwamba MAHAKIMU waliamua kususia hii kesi baada ya Huyu binti Fatma Karume kuamua kuwalipoti kwa ajili ya kuomba/ na kupokea rushwa.
 
jamani kama nilivyosema awali wakili ni ofisa wa mahakama kuu kwa hiyo hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi hawezi kumwadhibu kwa namana yoyote ile. yeye anachoweza kufanya ni kupeleka malalamiko kwa hakimu mkazi mwandamizi ili awasilishe malalamiko yake kwenye kamati maalumu ya malalamiko. ndiyo maana hakimu lyamuya alitafuta mashahidi wake na kusema wako tayari kutoa ushahidi wakati muafaka ukifika!!

kamati hiyo ina majukumu haya

ADVOCATES ACT (CAP 341)
section 13. Powers of Committee
(1) The Committee shall have jurisdiction to hear and determine–
(a) any application by an advocate to procure the removal of his name from the Roll;
(b) any application by any person to remove the name of any advocate from the Roll; or
(c) any allegation of misconduct made against any advocate by any person.

(2) Where an application or allegation of misconduct is made under paragraph (b) or paragraph (c) of subsection (1), the Committee shall have power to require the advocate in respect of whom such application is made, or in respect of whom such allegation is made, to show cause why his name should not be removed from the Roll of advocates or to answer the allegation made, as the case may be:
Provided that where, in the opinion of the Committee, an application under paragraph (b) of subsection (1), or an allegation under paragraph (c) of that subsection does not disclose a prima facie case, the Committee may refuse such application or may dismiss the allegation without requiring the advocate to whom the application or allegation relates to show cause why his name should not be removed from the Roll or to answer the allegation, as the case may be.

(3) On the hearing of an application under paragraph (b) of subsection (1) or any allegation under paragraph (c) of that subsection–

(a) the Committee shall give the advocate to whom the application relates or against whom the allegation is made an opportunity to appear and be heard by it, and for that purpose shall, not less than seven days before the date fixed for the hearing, inform him of such date and of the particulars of the application or allegation, furnish to him a copy of any affidavit made in respect of the application or allegation, and notify him of the time and place when and where he may inspect and make a copy of any other document in the possession of the Committee which it deems relevant to the application or allegation;

(b) the Committee may in the course of the hearing, hear such witnesses and receive such documentary evidence as in its opinion may assist it in coming to a conclusion as to the truth or otherwise of any allegation made against the advocate.

(4) Upon the conclusion of a hearing subsection (3) the Committee may, if it is satisfied of the truth of the allegations upon which an application under paragraph (b) of subsection (1) is founded or of any allegation of misconduct made against the advocate–

(a) direct that the name of the advocate be removed from the Roll;

(b) admonish the advocate; or

(c) suspend the advocate from practising for such period as the Committee may direct.

(5) In any proceedings under this section the Committee shall have power to make any such order as to payment by any party of any costs or witness expenses as it may think fit, and any such order shall be deemed to be an order of the High Court and may be enforced in like manner.

(6) If in the course of any hearing before the Committee after the whole or any part of the evidence has been heard and recorded, there is for any reason a change of the members of the Committee, the Committee may act on the evidence so recorded before such change, or partly recorded before and partly recorded after such change, as the case may be, or the Committee may re-summon the witnesses and recommence the hearing:
Provided that the advocate whose misconduct is the subject matter of the proceedings may, when the Committee resumes its proceedings after such change, demand that all the witnesses or any of them be re-summoned and reheard and shall be informed of such right by the Committee when it so resumes its proceedings.
 
Ninafikiri Fatma alichemsha, nionavyo mimi ni kwamba kuna kila dalili kuwa mtoto wa mkubwa ndio kumefanya awe jeuri namna hiyo. Pamoja na kwamba alikuwa na haki katika kuuliza hayo aliyouliza,lakini kitendo cha kutoka na kumfata hakimu alipo na kumfokea na maneno ya aibu, kinatia hasira sana, ukizingatia kuwa Fatma mwenyewe ni wakili hivyo tunaamini sheria anazijua labda kama uwakili aliupata kwa kuonga. Nafikiri angefutiwa kazi ya uwakili kwa muda kama adhabu aliyopoewa Masumbuko Lamwai. Lakini kama wenzangu walivyosema, Fatma kwa kuwa ni mtoto wa mkubwa yataisha haya kimya kimya kimya......kama kesi ya ditopile.
 
Mimi nasubiri kwa hamu magazeti ya kesho kwani na uhakika Fatma Karume hawezi kukaa kimya.
Alafu namtafuta Mwafrika wa Kike jamani, maana yeye ndiyo alikuwa anapenda quotation "well behaved women never make history!"
Haha! huyu dada is definitely not well behaved lakini kaweka historia!😀

Asubuhi ya leo huyo bibie alikuwa Clouds fm akielezea yaliyojitokeza.
Kwanza kabisa anasema mambo yaliyoripotiwa sivyo yalivyokuwa, kwani waandishi waliitwa na wakapewa hadithi hiyo na wakili wa utetezi; kwa hisia zake ni kuwa wakili huyo na hakimu wana lao jambo.
 
Back
Top Bottom