'Binti Kiziwi' ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huko Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, July 15, 2013

MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda' wa biashara hiyo haramu, Ijumaa Wikienda lina mtiririko wote.

Hivi karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange' amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi' akiwa na kilo mia moja na hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda kortini mara moja Ijumaa iliyopita.

SANDRA.JPG

Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed 'Z-Anto', Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga'.

HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.

UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio.

Kwenye makazi ya mama yake, Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo amehama baada ya kufunga ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

IJUMAA WIKIENDA LAZIDI KUCHIMBA
Ijumaa Wikienda lilizidi kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo ambapo lilifanikiwa kumpata ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya naye mazungumzo kama ifuatavyo:

Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli?

Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini?

Wikienda: Kuna manenomaneno kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli?

Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi.

Wikienda: Ukweli ni upi?

Ndugu: Kwanza kabisa Binti Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong Kong, kwa sheria za kule mtu akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga' anahukumiwa jela tu.

"Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka."

Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu.

Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana.

==============
Previously (Feb 2013)


SOOOO.jpg


SIKU chache baada ya mrembo wa video ya wimbo wa Binti Kiziwi wa Ally Mohammed ‘Z. Anto', Sandra Khan ‘Binti Kiziwi' kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kunaswa na madawa ya kulevya nchini China, Jacqueline Patrick ‘Jack' ambaye ni modo kiwango Bongo, amesema anajua kila kitu kuhusu tukio la kukamatwa kwake, Amani linakuhabarisha.

Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum juzi, jijini Dar es Salaam kuhusu uvumi ulioenea kwamba yeye ndiye aliyemchoma Binti Kiziwi kwa polisi na kusababisha kudakwa kwake, alisema tuhuma hizo si za kweli bali ni mbinu za watu wanaotaka kumchafua.

"Ngoja nikuambie ukweli, siku Binti Kiziwi anakamatwa mimi nilikuwepo uwanja wa ndege na niliona kila kitu. Unajua mwanzo alianza kulalamikia tumbo kumsumbua ghafla, akachukuliwa na kupelekwa kupewa huduma ya kwanza.

"Akiwa huko kwenye matibabu alipigwa ultrasound ndipo alipogundulika kuwa kumbe alikuwa na vitu tumboni.

Katika hali kama hiyo unadhani ni mjinga gani anaweza kujitokeza na kudai huyo ni ndugu yake?"

"Mimi sijui chochote lakini nilichojua yule ni Binti Kiziwi na ni Mtanzania mwenzangu, tena staa kama mimi kwa hiyo sikuwa na sababu ya kumchoma ila ilivyogundulika hivyo nisingeweza kujitokeza maana na mimi pia ningetakiwa kuisaidia polisi kwenye uchunguzi.

"Kubwa kuliko yote, yeye ni ndugu yangu kabisa. Mama yake na mama yangu ni ndugu, nisingeweza kumchoma."


"Jambo la muhimu nililoamua kufanya ilikuwa ni kutoa taarifa kwa ndugu zake wengine ili waweze kumsaidia.

Nilifanya hivyo kwa wakati. Siku zote nimekuwa karibu naye, hata nikienda China huwa nakwenda kumtembelea gerezani," alisema Jack.
 

Sasa hadi VIZIWI wetu wanawekwa karibu na hao CARTEL? inasikitisha!!!
 
Kweli fedha fedheha! Yaani hawa PUNDA wanavyobeba hayo madawa ya kulevya ni kwa NJIA ya udhalilishaji mkubwa. Kwasababu hizo KETE au PIPI huingizwa kwenye UTUMBO MKUBWA (sio tumboni) kupitia MKUNDUNI (ANUS). Just imagine mtu unaingizia kete kupitia mkunduni kisa eti pesa. Ndiyo maana wabeba unga wengi wanapenda K.U.F.I.R.W.A wake kwa waume.
 
Kweli fedha fedheha! Yaani hawa PUNDA wanavyobeba hayo madawa ya kulevya ni kwa NJIA ya udhalilishaji mkubwa. Kwasababu hizo KETE au PIPI huingizwa kwenye UTUMBO MKUBWA (sio tumboni) kupitia MKUNDUNI (ANUS). Just imagine mtu unaingizia kete kupitia mkunduni kisa eti pesa. Ndiyo maana wabeba unga wengi wanapenda K.U.F.I.R.W.A wake kwa waume.

mkuu umenifuisha hapo hapo nimesikitika sana
 
Huyo ndg yake mwenyewe inaonekana ni teja kama siyo teja atakuwa punda kama siyo punda atakuwa kontena naishia hapo
 
Kweli fedha fedheha! Yaani hawa PUNDA wanavyobeba hayo madawa ya kulevya ni kwa NJIA ya udhalilishaji mkubwa. Kwasababu hizo KETE au PIPI huingizwa kwenye UTUMBO MKUBWA (sio tumboni) kupitia MKUNDUNI (ANUS). Just imagine mtu unaingizia kete kupitia mkunduni kisa eti pesa. Ndiyo maana wabeba unga wengi wanapenda K.U.F.I.R.W.A wake kwa waume.
Kiongozi ni kweli vijana wengi hawajui jinsi yanavyobebwa wanafikiri unameza km panadol!
Hata hivyo hizi habari za madawa zinasikitisha sana baba mkwe wangu amenyongwa uarabu mwezi uliopita na tumezika Tanga.
NB: Watanzania wenzangu maisha hayana shortcut fanyeni kazi acheni usitaduh na ubrazamen.
 
Vijana wengi TZ kwa sasa hawataki kufanya kazi pia wana tamaa ya kuendesha magari mazuri pasipo kufanya kazi.Mimi naomba waongezewe adhabu kali zaidi.
 

miaka mitano mbona kidogo
wanatakiwa wazeeke jela hao shenzzzzzy zao
kutuharibia vijana wetu!!
 
Hawa wasanii wa bongo ni janga lingine..pale uwanja wa ndege wanapitaje?? Na huyo kaka yake anaonekana nae ni walewale eti 'miaka mitano sii mingi atatoka tu' shame on you mnaharibu maisha ya watu kwa ujinga wenu wa.pu.mba.vu kabisa
 
Nadhani pia jk atakua anahusika na huu mtandao wa wauza madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom