Binti Apachikwa Mimba na Mwenziye!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,331
2,000
Yep! Hicho ndicho kichwa cha habari kwenye ippmedia.com cha habari ifuatayo:

Binti apachikwa mimba na mwenziye

2007-10-11 16:36:12
Na Janeth Kiure, Kibaha

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lupondo, Paulina Ciaga amefukuzwa shule baada ya kubainika kuwa amepewa ujauzito na mwanafunzi mwenzie wa kidato cha kwanza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Henry Salewi amesema mwanafunzi huyo alitimliwa shule jana mishale ya saa 7:00 mchana alipobainika kuwa na ujauzito a miezi sita.

Amesema Kamanda Salewi kuwa binti huyo alipohojiwa kuhusiana na mtu aliyempa ujauzito, akamtaja kijana Bakari Busoji ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule yao kuwa ndIye aliyempa ujauzito huo.

Kamanda Salewi akasema Polisi ilipomfuatilia mtuhumiwa huyo ailikuta ameshatoroka na kwenda kusiko julikana na hivyo anaendelea kusakwa na Jashi hilo.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Pwani linaashikilia Mbaraka Omary, 14, Jasta Antony, 27 na Thabit Khalfan, 27 kwa tuhuma za kukutwa wakiwa na gramu 15 za bangi.

Kamanda Salewi amesema watu hao walikamatwa jana mishale ya saa 2:30 katika uwanja wa mpira wa Nyundo wakati Polisi walipofanya msako katika eneo hilo.

Kamanda Salewi amesema Jeshi lake pia linamshikilia Benedict John aliyekamatwa akiawa na lita 10 za pombe haramu ya gongo.

Akasema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana mishale ya saa 4:00 asubuhi huko Kimanzichana wilayani Mkuranga akiwa na kiasi hicho cha gongo.

Pia Kamanda Salewi amesema mtuhumiwa mwingine RamadhaniNyawimba pia alikamatwa jana mishale ya 2:30 katika kijiji cha Tangisini akiwa na lita 60 za pombe haramu ya gongo.

Akasema watuhumiwa wote ni watumiaji na wauzaji wa pombe hiyo, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

Kamanda Salewi amesema watuhumiwa wote wataburuzwa mahakamani wakati wowote baada ya Polisi kukamilisha upelelezi wao.

SOURCE: Alasiri
 
Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,749
2,000
Yep! Hicho ndicho kichwa cha habari kwenye ippmedia.com cha habari ifuatayo:

Binti apachikwa mimba na mwenziye

2007-10-11 16:36:12
Na Janeth Kiure, Kibaha

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lupondo, Paulina Ciaga amefukuzwa shule baada ya kubainika kuwa amepewa ujauzito na mwanafunzi mwenzie wa kidato cha kwanza.

...hii kichwa cha habari bado ilikuwa kinanitatiza mpaka niliposoma na hapa;...
Amesema Kamanda Salewi kuwa binti huyo alipohojiwa kuhusiana na mtu aliyempa ujauzito, akamtaja kijana Bakari Busoji ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule yao kuwa ndIye aliyempa ujauzito huo.

...'mwenziwe' ni tungo tata, anaweza kuwa 'mwenziwe' kwa maana ya 'mwenziwe' kweli, dunia imebadilika, 'laana' imeingia mpaka katika jamii za kwetu.
 
Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,337
1,250
me too niliposoma amepachikwa mimba na mwenziye sijui mwenzake..nikajua ndio watu wameshaweza prove kuwa wana science na biology kwa ujumla ni waongo..as nilijua ni msichana mwenzake ndio kampa mimba....
 
Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
683
0
Duh sasa nawewe mwanakijiji ndio kichwa gani cha habari hicho? mimi nimefikiria nature imebadilika na sasa wasichana wanapachikana Mimba. Waandishi wetu ni wafani sana nakumbuka waliwahi kuandika kuwa POLISI MBEA WAFUNGUA TOVUTI YA KURIPOTI UHALIFU, kusoma ndani kumbe ni polisi wafungua e mail address ya polisimbeya@yahoo.com.

Jana nimesoma habari kuwa zaidi ya 60% ya majeruhi wanaolazwa MOI ni wakazi wa Dar. Sasa nikajiuliza hivi kweli kwani watu wa Mwanza, Kigoma, Mbeya, etc wanategemewa kulazwa MOI?
 
Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
449
250
hata miye ndiyo nikakurupuka nilidhani mjanja na yeye alijifanya demu (no pun intended)
Mwanakijiji mbona watu vunja mbavu?, ama ndo zilikuwa zako utotoni?
ngoja niendelee kucheka!

On serious`note, hata miye nilijiuliza swali hilo....Nadhani kiswahili safi ilitakiwa kiwe hivi; "mwanafunzi apewa mimba na mwanafunzi mwenzake (au mwenziye)" ...na siyo "Binti apachikwa mimba na mwenziye" Kwanza ni lugha ya kihuni sana, isiyo na heshima na tatu sentensi yenyewe ina maanisha kuwa huyo binti amepewa mimba na binti mwingine.
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
9,986
2,000
Duh sasa nawewe mwanakijiji ndio kichwa gani cha habari hicho? mimi nimefikiria nature imebadilika na sasa wasichana wanapachikana Mimba. Waandishi wetu ni wafani sana nakumbuka waliwahi kuandika kuwa POLISI MBEA WAFUNGUA TOVUTI YA KURIPOTI UHALIFU, kusoma ndani kumbe ni polisi wafungua e mail address ya polisimbeya@yahoo.com.

Jana nimesoma habari kuwa zaidi ya 60% ya majeruhi wanaolazwa MOI ni wakazi wa Dar. Sasa nikajiuliza hivi kweli kwani watu wa Mwanza, Kigoma, Mbeya, etc wanategemewa kulazwa MOI?

....wajameni mie bado nacheka kutokea jana kwikwikwi hahahahahaha
enewei hapo ndipo mfahamu kuwa hata taaluma ya habari imeingiliwa. ila ukitaka kucheka zaidi nenda nairobi ukasome headings za tabloids za kiswahili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom