Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza afariki kwa kujinyonga baada ya kunyang’anywa simu na kaka yake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza aliyekuwa anasoma Shule ya Sekondari Sarungi, Wilayani Rorya amejinyonga kwa kamba ya katani chumbani kwake kwake baada ya kudaiwa kutokea mzozo na kaka yake

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime, Mark Njera amesema “Binti huyo mwenye umri wa miaka 15 alichukua uamuzi baada ya kunyang’anywa simu na kaka yake waliyokuwa wakiigombania, baada ya kitendo hicho alikasirika na kwenda chumbani kwake akachukua kamba ya katani na kufunga kwenye kenchi kisha kujinyonga.”

Chanzo: AZAM TV
 
Nguvu iliyopitiliza katika kuyaelekea mambo inatesa na kuhumiza .

At her age 15 mtoto anakuwa tayari ni hisia ndo zinamfanyia maamuzi na sio akili , hivyo ni muhimu kuifanya hekima kutawala zaidi ili kuondoa madhara negative.

Rip
 
Inawezekana kweli ila kuna muda mmaamuzi ya mtu ya akushangaza kama vile kuna msukumo ndani yake. We wadhani ndio kitu cha kwanza kunya ganywa hicho
 
Inawezekana kweli ila kuna muda mmaamuzi ya mtu ya akushangaza kama vile kuna msukumo ndani yake. We wadhani ndio kitu cha kwanza kunya ganywa hicho

Unapomlea mtoto unabidi kujua akifika katika Adolescent stage anakuwa anafanya mambo mengi bila kuwa logically

Hivyo lazima uwe makini katika kumlea kwa utulivu.

Hivyo hiyo hatua inahitaji ufahamu mzuri kuhusu mtoto
 
Back
Top Bottom