CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,257
- 12,877
asante kwa somo zuri! barikiwa mpendwa. . .
asante kwa somo zuri! barikiwa mpendwa. . .
Umerudisha passport ya jiran yetu?
Stori za kusadikika hizo, ama ndo utatumia ibadani jumapili? Mchungaji aruhusu mtu kufunga ndoa kutoka kwa waumini bila kuandikisha, kutangaza siku 21 kwa mujibu wa sheria na kufanya mafundisho ya ndoa?
Eti eeh? Nikisali Kanisa lako sadaka naenda kunywea supu!Hii ni habari ya kweli kabisa, kama wewe huamini kwamba ni ya kweli, endelea kutoamini.
Ntake radhi. Mi Nataka mifano iliyoenda shule.Du! yaani King'asti mtata aisee, mwenzio atakuwa ametumia kama mfano tu huo jama, lengo ilikuwa kumwaga neno kwa chini pale ........
charminglady, tofautisha mifano na parables. Afu anasisitiza ni ukweli. Last week nilikutana na mmama akanipa stori kuhusu my old prof. Ati alikataliwa na mume kanisani, padri Akaita anaetaka kumuoa ndo hadi Leo mumewe. Najua ni wivu tu, the lady is super intelligent and has done great things for this country. Niliishia tu kuwa polite na kusema she is a great and strong woman!King'asti huo ni mfano kama mifano alokuwa anaitumia Yesu kipindi kile. km we ni mkristo naamini ushawah kusikia ule mfano wa Yesu kuwa ni rahisi kwa ngamia kupenya katka tundu la sindano. hapo hajamaanisha kwel ngamia anaweza kupenya kwny tundu la sindano. na mifano hutusaidia sana kuelewa mengi ambayo ni vigumu kuelewa.
Haya ni mafundisho tu na siyo ukweli. Hakuna mchungaji atakayetoa ruksa hiyo ya ghafla kufungisha ndoa.
Hapo nimemuelewa ni kwamba tusikubali kudanganyika, na pia usimuamini hata rafiki yake kipenzi.
MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
Hii ni habari ya kweli kabisa, kama wewe huamini kwamba ni ya kweli, endelea kutoamini.
Mkuu una maana huyu ndugu ndiye Shigo?
Dada mmoja ambaye alikuwa anakaribia kufunga ndoa na mchumba wake, alikuwa na rafiki yake kipenzi ambaye alimshirikisha katika mambo mengi sana. Na wiki moja kabla ya ndoa, rafiki yake alimletea taarifa juu ya uaminifu hafifu wa mchumba wake. Ili kurahisisha naomba nirumie binti X kuwakilish rafiki wa bibi harusi mtarajiwa. Na taarifa zile zilimshitua sana yule bibi harusi mtarajiwa, basi akaamua kuomba ushauri wa nini cha kufanya toka kwa binti X. Binti X alimshauri kwa kumuambia kuwa amkatae siku ya harusi kama adhabu kwa mchumba wake. Siku zilijivuta, hatimaye siku ya harusi ikawadia, mchungaji alipoanza maswali kwa bibi harusi iwapo kweli binti anaridhia kuolewa, binti alijibu kama ifuatavyo simpendi huyo mwanamme, wazazi wangu ndio walionilazimisha kuolewa, kwa hiyo sipo tayari kuolewa. Mchungaji akamuuliza Bwan harusi, sasa tunafanya nini kama binti amekukataa?. Bwana harusi alisema, naomba kama kuna binti aliye tayari kufunga pingu za masha na mimi, ajitokeze maana leo ni siku yangu ya kuoa na zege haitalala. Mchungaji aliuliza kama kuna binti aliye tayari. Muda ulipita pasipo binti yeyote kujitokeza na hatimaye binti mmoja akanyanyuka na kusema yeye tuko tayari kumsaidi huyo kaka, kweli pale pale iabidi aliyekuwa bibi harusi avuliwe shela na harimaye binti aliyejitolea akavishwa shela na hatimaye ndoa ikaendelea kufungwa. Bibi harusi wa awali alipotazama vizuri nani aliyejitolea kuolewa, lahaula!!, alikuta ndiye yule rafiki yake yaani binti X. Aliyekuwa bibi harusi akapaza sauti na kusema nataka kufunga ndoa na mme wangu maana huyo aliyejitolea, ndiye aliyenidanganya nimkatae mpenzi wangu siku ya ndoa. Mchungaji akaamua kumuultiza Bwan harusi kuwa anamtaka yupi, naye akajibu anamtaka yule wa pili. Kwa hiyo bibi harusi original akawa amekosa kuolewa.
Ni vivyo katika upande wa mambo ya Mungu, kuna watu wanaondanganya watu ambao hatimaye wamedangantika. Ndiyo maana Mungu alitahadharisha katika kitabu cha Isaya 9:16 alionya kwa kusema haya Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia. Kumbe ukikubali kuongozwa na watu wapotoshao utakuwa umepotea na mauti ya milele yatakuwa yanakusubiri. Kuna watu akishasikia chochote kikitajwa na kiongozi wa dhehebu lake, basi anaamini, hata kama hayo ni maneno ya kupotosha. Nao wanatahadharishwa hivi katika Yeremia17:5-6, BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA, Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema, bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Mengi yapo ya kuandika lakini kwa sasa naomba kuishia hapo.
NAOMBA KUULIZA KUHUSIANA NA KIFUNGU HIKI:
''Yeremia17:5-6, BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA, Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema, bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu''
1.Tafsiri ya neno BWANA katika bible ni ipi ni Bwana Mungu ama Bwana Yesu?
2. Je? Yesu ni Mwanaadamu ama si Mwanaadamu?
3. Kuna watu ama kuna sehemu nimeona pameandikwa '' Gari hili linalindwa na damu ya Yesu'' hapa ikoje? kutokana na maandishi ya hapo juu?
Naomba kuelimishwa maana kuuliza si ujinga waungwana
anaonekana tu.labda iwe hii fani imevamiwa na watu wengine.
Ubarikiwe sana, lakini hayo maneno yako ambayo sikutarani yalopokwe na wewe sijayashangaa sana, maana ni sharti viumbe kama wewe wawepo duniani ili necha ibalansi. Ubarikiwe sana tena sana.