Binti aliyeitoa jasho familia kwa visa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti aliyeitoa jasho familia kwa visa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 7, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hii picha haihusiani na habari hii.....................

  Inaniumiza
  sana kuikumbuka, hasa kuisimulia, lakini nimeambiwa kuwa, kwa kusema jambo hili wazi, naweza kupata nafuu. Hata hivyo naamini nitapata thawabu kwa kuwasaidia wengine kujua tatizo na kuweza kuliepuka wakimudu. Mimi na mke wangu tulioana mwaka 1974 jijini Dar es salaam, mimi nikiwa na miaka 32 na yeye akiwa na miaka 24 wakati huo. Mke wangu ni mwenyeji wa Iringa na mimi ni mwenyeji wa Lushoto, mkoani Tanga. Tulikutana hapa Dar es salaam, mimi nikiwa mfanyabiashara naye akiwa amemaliza kozi ya ualimu daraja ‘A' akisubiri kwenda kufundisha.

  Tulianza uhusiano na alipopangiwa kituo cha kazi Kyela, nilimwambia asiende. Alisema ni lazima aende akaonje ualimu ambao aliusomea kwa miaka miwili. Alikwenda, lakini baada ya miezi sita alirudi akidai hawezi. Nilimwomba aache ualimu na kufanya biashara. Tulikubaliana. Tulioana wakati huohuo na kuanza maisha ya mke na mume. Tulikuwa tukiishi Mburahati wakati huo, ambapo baadae hata hivyo tulihamia Sinza. Tulikaa kwa miaka mitatu bila mke wangu kupata ujauzito. Ndugu walianza maneno na mke wangu alianza kubabaika. Nilimtuliza na kumwambia, angekuja tu kupata ujauzito.

  Hadi mwaka 1980 yaani miaka sita baadae, mke wangu alikuwa bado hajapata ujauzito. Ndugu zangu walianza kelele na vurugu za kila aina, wakidai nioe mke mwingine. Nilipuuzia maneno yao, ingawa yalianza kuniingia kidogokidogo. Mwaka 1981 niliwaza njia ambayo niliona ingesaidia kuondoa kero zote. Nilimwambia mke wangu afunge maguo tumboni na kuonekana kama ana ujauzito. Aliponiuliza sababu , nilimwambia afanye tu hivyo. Alibishabisha awali, lakini nilipomuuliza kama haniamini, aliamua kunikubalia ombi langu.

  Alipovaa maguo hayo na kuonekana kama mwenye ujauzito nilianza kutangaza kwamba mke wangu ni mjamzito. Nilitangaza kwa ndugu, jirani na hata kwa jamaa zangu wa karibu. Ilipofika miezi saba baada ya kutangaza hivyo nilimwambia mke wangu ni muda mzuri sasa wa kuaga kwamba anaenda kwao. Nilikuwa wakati wote huo nahangaika kutafuta namna ya nitakavyoweza kuwezesha kile nilichokuwa nimekibuni. Ni kweli aliondoka kwenda kwao. Wiki ile ile aliyoondoka, nilifanikiwa kupata nilichokuwa nataka.

  Nilikuwa nimezungumza na wahusika wengi sana wa maeneo mbalimbali ambao wangeweza kunipatia mtoto mchanga. Mama mmoja ambaye naomba nisimtaje jina alipata mtoto mchanga. Mtoto huyo alikuwa amezaliwa hospitalini {naomba nisiitaje} na mama yake akafariki. Hakutokea mtu kumdai mtoto, wala maiti ya mama yake na huyo mama alijifanya ni ndugu wa marehemu, mara tu alipofariki. Kwa kutumia fedha kidogo nilizokuwa nimempa aliruhusiwa kumchukua mtoto yule akamlee. Ukweli ni kwamba hakuna ndugu wa yule msichana aliyejitokeza hapo hospitalini………….

  Kwa kusindikizana na mama huyu, tulisafiri kwenda Iringa kwa mke wangu. Mke wangu hakuwa ameenda kuishi kijijini bali alikuwa akikaa hotelini, pale Iringa mjini. Tulipofika pale hotelini, nilimkabidhi mke wangu kachanga kale nakusema ni kake kuanzia wakati ule. Kalikuwa ni katoto ka kike kazuri. Kwa mara ya kwanza mke wangu alijua mpango wangu. Ilibidi niondoke na mke wangu kwenda naye kijijini kwao, ambapo tulipofika tuliwaambia alikuwa amejifungua njiani. Nilimwacha kule na kurudi Dar es salaam, kutangaza kwamba mke wangu amejifungua mtoto wa kike. Siwezi kusema furaha iliyokuwepo kwa ndugu zangu na wa mke wangu. Tukawa wanandoa wenye mtoto mmoja kwa njia hiyo.

  Mwaka 1987 ndipo tulipoanza kushangazwa na binti huyu, akiwa na miaka sita wakati huo. Kwanza, alikuwa ni binti mkatili sana, tangu akiwa mdogo tu wa miaka mitatu. Alikuwa anapenda sana kukwangua wengine tukiwemo sisi. alipoanza kuzungumza, alikuwa akizungumza maneno ya ajabu, lakini ya kutisha pia. Mara nyingi alikuwa akipenda sana kutaja kufa, kuumwa na nyoka, kupanda mlimani, kufukiwa gizani na mengine ya aina hiyo. Alikuwa akipenda sana kusikiliza kwa makini watu wanapokuwa wakizungumzia mambo ya uasi kuliko mambo mazuri. Hii tabia tuliigundua alipokuwa na miaka mitano.

  Akiwa na miaka sita, tukio la kwanza lililotushtua ni lile la kumwambia mama yake, hana adabu, alimwambia hivyo kufuatia kumwambia , akinywa chai awe anaondoa kikombe chake mezani na kukipeleka jikoni. Mama yake alimchapa. Kwa kawaida mtoto wa miaka sita akichapwa, mtu anategema akiona akilia. Huyu hakulia, bali alimwangalia tu mama yake vibaya na kuondoka. Siyo siri, niliogopa sana. Mwaka 1994 alipokuwa darasa la saba alifanya vituko vingi sana na tulihangaika sana kutafuta suluhu. Ili kupunguza maumivu, tuliamua kumpeleka shule ya sekondari ya bweni mikoani. Tulimpeleka. Lakini hata mwezi haukuisha alikuwa amerudishwa kutokana na kushindikana.

  Alikuwa na kila aina ya visa. Alikuwa akitukana waalimu, kupiga wanafunzi wenzie na kuanzisha vurugu za aina mbalimbali. Ajabu ni kwamba, ukiwa umekaa naye na kuzungumza naye, anakuwa mtoto mzuri na msikivu sana. Anaweza hata kulia, kujutia makosa yake. Lakini baada ya hapo ndio anakuwa ametiwa moto. Kwa mwaka mmoja wa kidato cha kwanza, tulimbadilisha shule kiasi cha sita. Alipoingia kidato cha pili ndio vurugu zikawa kubwa zaidi. Lakini sasa hapa akawa ameanza tabia za uhuni, yaani kushiriki ngono.

  Hali hii ya kupenda kushiriki mapenzi ilitukera sana na tulijua kwamba tumeshapoteza mtoto tayari. Lakini katikati ya tatizo hili, likazuka lingine. Hili ndilo lilikuwa kubwa zaidi. Alikuwa mara nyingi akidai kwamba ana hamu na mama yake. Tulipokuwa tukimwambia kwamba mama yake yupo hapo nyumbani, yaani mke wangu, alikuwa akisema hana uhakika sana kama hadanganywi. Kusikia hivyo, nilijua yule mama aliyenisaidia kumpata alikuwa amemwambia siri yote. Nilipomwendea na kumuuliza alisema asingeweza. Lakini alisema hata mama yake halisi na yule mtoto, kabla hajafa alikuwa akiropoka mambo mengi makubwa na ya kutisha. Ilibidi sasa niombe ushauri kwa watu mbalimbali, kuanzia kwa mashehe, mapadri, waganga na madaktari, lakini hakuna kilichobadilika.

  Kila mmoja alijaribu kumsaidia kwa namna yake lakini, bila mafanikio. Pamoja na Vituko vyake na kauli za kutisha, hasa hizo za kumtaka mama yake na kusema anahisi haambiwi kweli, bila kufafanua, alimaliza kidato cha nne mwaka 1999. Wakati huo alikuwa anaumwa
  sana hata hivyo. Tulijaribu kumsaidia sana kwa matibabu na kumtunza.

  Tulikuwa tunampenda sana pamoja na visa na vituko vyake. Mwaka 2000 alizidiwa sana na maradhi na tulilazimika kumfanyia vipimo zaidi na alibainika kwamba ameathirika kwa ukimwi. Hatukumpa matokeo ya vipimo hivi awali,lakini alitushangaza aliposema, 'mnanificha kitu gani, siogopi kama mnavyofikiria. Kwani mtu kwenda kuungana na mama yake kuna tatizo?' Kwa kuwa nilishamzoea kwa visa vingi lukuki, sikustuka sana, ingawa mke wangu alishtuka kupindukia.

  Mwaka 2001 alizidiwa kabisa na sasa alikuwa akikaa nyumbani tu. Siku moja mwezi wa Juni aliomba apewe jina la ukoo wa mama yake, kabla hajafa. Hapo tuliogopa vizuri sana kwa kweli na siwezi kuisahau siku hiyo. Tulimpa jina la ukoo wa kwa mke wangu, alikasirika sana na kusema anataka jina la ukoo wa kwao. Alisema akifa bila jina hilo, mambo yasiyopendeza yangetokea na kwamba asingepaswa kulaumiwa kwa hilo, kwani kazi tuliyofanya ingekuwa imepotea bure.

  Tuliogopa sana na ilibidi niende kwa yule mama aliyenifanyia mpango wa kumpata binti huyu na nilizungumza naye. Alisema, ingekuwa ni vigumu kwake kupata taarifa za yule mama yake. Lakini kwa bahati alikumbuka jina na ubini na kwamba, yule mama alimwambia alikuwa ametokea kijiji cha Puge, Nzega, Tabora. Alimwambia alifika Dar es salaam kwa kudanganywa na mtu ambaye alimleta Dar na kumtelekeza baada ya ujauzito.

  Nililazimika kusafiri hadi huko Puge, nilipofika hapo kijijini {Ni kijiji lakini ni
  kama kamji kadogo} nilidadisi na kupata taarifa kumhusu yule mama. Sikusema chochote, zaidi ya kurejea Dar es salaam. Nilivyoambiwa kule ni kwamba, yule mama wa mtoto wetu alikuwa apewe kitu walichoita Mkoba {Uganga bila shaka} ya bibi yake mzaa baba, lakini akakataa na kukimbilia kusikijulikana.

  Huku Dar es salaam alikuja mwenyewe na kukutana na huyo tapeli aliyempa ujauzito. Inaelezwa kwamba, bibi yake alikufa akiwa hajakabidhi mikoba ya uganga kwa yeyote. Hayo niliyaamini ingawa kabla ya tukio hili, kama ungenitajia jambo kama hilo, ningekutemea. Nilirudi Dar na nilipofika nyumbani, hali ya binti yetu ilikuwa mbaya sana. Nilimsalimia na kumwambia kwamba tunampa jina {Naomba nisilitaje}. Aliposikia jina hilo aliinua kichwa, jambo ambalo alikuwa hajawahi kulifanya tangu kuzidiwa kwake na ugonjwa.

  Halafu alirudisha kichwa kwenye mto na kufariki hapohapo. Naomba uniamini kwa faida yako, kwani hilo, lilitokea mbele ya macho yangu. Sioni faida ambayo mimi au wewe utaipata kwa uongo ambao nitaufanya katika suala hili. Mwaka huo huo akiwa na miaka 41 mke wangu alijifungua mtoto wa kike. Ilikuwa kama ajabu kwetu na mshangao huo hauwezi kututoka hata siku moja. Lakini hata kama atakuja mtu gani tukubali kuwa hakuna miujiza na nguvu za ajabu kwenye maisha, tutambishia hata kwa thamani ya damu yetu, kwa sababu tumeona kwa macho yetu.

  Mimi na mke wangu tumeumizwa sana na kilichotokea na hasa matukio ya yule binti yetu ambaye tulimlea kwa upendo. Tumekuwa tukijiuliza kilichotokea bila kupata jibu.
   
 2. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Duh.....ebana sijui ubarikiwe au uende kanisani kupata maombezi..sema hongera mzee hii stori inafaa kuwekwa kwe shuhuda za makanisani..
   
 3. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  duh, yaan mpaka mwili umenisisimka, dah ila nampongeza hy baba alikuwa na mapenz ya dhat kwa mke wake

  Wakati mwingine ndg, majiran marafiki na jamii kwa ujumla wanaweza kutufikisha kufanya maamuz ajab sana

  hope wengine wanajifunza ki2 kwenye story hii
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,073
  Trophy Points: 280
  Inatisha!
   
 5. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Duu Mtambuzi hii kitu imenistua sana!!! Kweli maishani kabla hujafa hujaijua sawasawa!!!!!

  Shukuru MUNGU kama binti yenu mliyepata anaendelea vizuri na shikeni sana MAISHA YAFUATAYO NJIA SAFI ZA MUNGU
   
 6. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi nitakuwa wa mwisho kuamini hii stori..lol!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haya bwana...................................!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii hainihusu mimi mkuu.................
   
 9. p

  pointers JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kweli hii ni changamoto kali sana kwenye maisha kwa kweli............unaweza ukapata kichaa bure
   
 10. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Interesting- And I'm speechless!
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Duu hii jaijakaa vizuri sana, Duniani kuna mambo
   
 12. K

  Katufu JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 433
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Hizo ni nguvu za giza ungepata akili ya kumpeleka kwa watumishi wa Mungu kama Kakobe na wengine matatizi yangeisha na sasa hivi ungekuwa na binti yako. Ila baadae ingebidi utubu na kumweleza ukweli
   
 13. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  I am glad haikuhusu wewe, naweza iamini kwani nimejifunza there is a lot going on kwenye hii ardhi. The fact kwamba hujashuhudia does not mean kuwa hayapo.

  Kuna issue imetokea recently hapa Kigoma,
  Anakuja mdada nyumbani kwako, na kujiintroduce as a distance relative na kukutajia maisha yako na ya watu wako wa karibu wote (anavaa uhusika kisawa sawa), anakaa siku kama mbili halafu anaondoka na mtoto wako wa kike less than 2 yrs. Baada ya muda (hadi miezi) unakuja mpata wilaya au mtaa mwingine kabisa unharmed.

  Amefanya hivyo kwa familia moja ninayo ifahamu, over the course ya kuhangaika wakakuta hiyo story kwa watu wengine kama 6 hivi (police kituo cha mjini Kigoma wanaifahamu). Huyo dada anajulikana kwao kama Kabula (jini Kabula), na inasemekana anawapeleka hao mabinti ziwani God knows nini kinafanyika huko.

  Kwa kweli mambo mengine yanatisha sana, usiombe kukutana nayo!
   
 14. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh kwa kweli huyo baba alinifurahisha sana kwa jinsi alivyokuwa na upendo na mkewe.
  Mh PIA YAWEZEKANA huyu baba alijijua yeye ndiye mwenye mapungufu so kumtema mkewe isingekuwa suluhisho na ndio maana alifight kufunika kombe.

  Mh now a new baby girl!
   
 15. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Makubwa haya tena!
   
 16. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  mwili wote umenisismka! hapo ndipo unaamini kuwa hakuna linalomshinda mungu baada ya mateso na tabu zote mlizopitia hatimae amewafuta machozi na jasho lenu..."kweli nani kama yeye aliye juu...sifa na shukrani apewe mungu"
   
 17. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  SnowBall naamini hii story ila nitakuwa wa mwisho baada yako kuamini kama ilimtokea Mtambuzi, nilishasikia ushuhuda huu kwenye redio fulani ya kidini mkoani Arusha
   
 18. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mtambuzi hii story nimewahi kuisoma kama sio marehem munga basi kwenye blog yako'hongera sana kwa kutunza kumbukumbu za marehem munga'na vile visa jinsi nilivyofedheheka unavyo?
   
 19. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi dunia hii iache kama ilivyo baba macho yetu huona pafupi sana sana nasikiaga huko njiani tunatembea ila tunapishana na watu tusiowaona du huwezi jua ila afadhali alikufa angefunua masiri yasiofunulika maana kimbembe kingerudi kwa yule dada du!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Triple G

  Triple G JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  mkuu inatisha sana.daah poleni sana.
   
Loading...