Binti aliyeitoa jasho familia kwa visa

I am glad haikuhusu wewe, naweza iamini kwani nimejifunza there is a lot going on kwenye hii ardhi. The fact kwamba hujashuhudia does not mean kuwa hayapo.

Kuna issue imetokea recently hapa Kigoma,
Anakuja mdada nyumbani kwako, na kujiintroduce as a distance relative na kukutajia maisha yako na ya watu wako wa karibu wote (anavaa uhusika kisawa sawa), anakaa siku kama mbili halafu anaondoka na mtoto wako wa kike less than 2 yrs. Baada ya muda (hadi miezi) unakuja mpata wilaya au mtaa mwingine kabisa unharmed.

Amefanya hivyo kwa familia moja ninayo ifahamu, over the course ya kuhangaika wakakuta hiyo story kwa watu wengine kama 6 hivi (police kituo cha mjini Kigoma wanaifahamu). Huyo dada anajulikana kwao kama Kabula (jini Kabula), na inasemekana anawapeleka hao mabinti ziwani God knows nini kinafanyika huko.

Kwa kweli mambo mengine yanatisha sana, usiombe kukutana nayo!
watakuwa wanaenda kuwa initiated na mambo ya nguvu za giza....endelea kuchunguza tabia zake za sasa na hali ya maisha ya familia yake lazima kutakuwa na mabadiliko makubwa.
Yapo mengi mabaya dunia hii....salama ni ndani ya Yesu tu.
 
Mh kwa kweli huyo baba alinifurahisha sana kwa jinsi alivyokuwa na upendo na mkewe.
Mh PIA YAWEZEKANA huyu baba alijijua yeye ndiye mwenye mapungufu so kumtema mkewe isingekuwa suluhisho na ndio maana alifight kufunika kombe.

Mh now a new baby girl!

Hamna bana kuna watu wana mapenzi ya kweli me nimeona watu wamekaa ten years ndo wanapata mtoto na mwanaume anakuwa mwaminifu.Mara nyingi ndugu ndo wanaletaga chokochoko
 
watakuwa wanaenda kuwa initiated na mambo ya nguvu za giza....endelea kuchunguza tabia zake za sasa na hali ya maisha ya familia yake lazima kutakuwa na mabadiliko makubwa.
Yapo mengi mabaya dunia hii....salama ni ndani ya Yesu tu.

Yaani my heart goes to the little girls, tatizo hiyo familia ninaowafahamu ni waislamu hivyo ni ngumu wao kkimbilia kwa Yesu ingawa nimewashauri.
 
Unajua nini Matambuzi! yawezekana hii ni kweli, ila kinachoweka ugumu sisi kuamini ni kwamba, wewe Mtambuzi ni mmoja wa wakale wa stori za namna hii hapa jukwaani,sasa inakuwa vigumu kuamini hii sio sehemu ya zile za ubunifu wako!!
 
Mara nyingi san mambo kama haya husaidia kutujulisha kuwa pamoja na sayansi kushindwa kuthibitisha nguvu hizi,haimaanishi kuwa hazipo!
 
I am glad haikuhusu wewe, naweza iamini kwani nimejifunza there is a lot going on kwenye hii ardhi. The fact kwamba hujashuhudia does not mean kuwa hayapo.

Kuna issue imetokea recently hapa Kigoma,
Anakuja mdada nyumbani kwako, na kujiintroduce as a distance relative na kukutajia maisha yako na ya watu wako wa karibu wote (anavaa uhusika kisawa sawa), anakaa siku kama mbili halafu anaondoka na mtoto wako wa kike less than 2 yrs. Baada ya muda (hadi miezi) unakuja mpata wilaya au mtaa mwingine kabisa unharmed.

Amefanya hivyo kwa familia moja ninayo ifahamu, over the course ya kuhangaika wakakuta hiyo story kwa watu wengine kama 6 hivi (police kituo cha mjini Kigoma wanaifahamu). Huyo dada anajulikana kwao kama Kabula (jini Kabula), na inasemekana anawapeleka hao mabinti ziwani God knows nini kinafanyika huko.

Kwa kweli mambo mengine yanatisha sana, usiombe kukutana nayo!

the same story imtokea mtaani kwetu a 3 yrs boy alikuwa na mama yake ndani, mama kaingia bafuni kuoga geti kafunga mtoto kafungua na kutoka kibaya zaid ilikuwa jion so mama kutoka bafuni mtoto hayupo, tulihangaika kutafuta pasi mafanikio after 4 daysza fasting tena kwa mnyororo like no one was eating anything for 4 days among those people ambao walikuwa wanafunga huku wengine tukihangaika kutuma matangazo kwenye ma tv redio na hata misikitini na makanisani the last day ya fasting ndipo mtoto alipokutwa kituo cha polis mbagala from where i live is about 90 km. mtoto kafikaje no one knows. tuliona tangazo kwenye jiji letu mtoto enock anawatafuta wazaziwake hatukuamni aisee.

kumbe bwana kuna binti huwa anazunguka mtaani ambaye ukimuona unaona kama ni mtu unayemjua na huwa wanaenda nao huko majimatitu what they do there no body knows. ooh god help our kids.
 
dah, imenisikitisha sana story hii. Swali langu ni kuwa huyu mtoto hapo pichani ndio huyo aliyekuja kufariki au imewekwa tu !??
tema_girl_ghana.jpg

Inaniumiza sana kuikumbuka, hasa kuisimulia, lakini nimeambiwa kuwa, kwa kusema jambo hili wazi, naweza kupata nafuu. Hata hivyo naamini nitapata thawabu kwa kuwasaidia wengine kujua tatizo na kuweza kuliepuka wakimudu. Mimi na mke wangu tulioana mwaka 1974 jijini Dar es salaam, mimi nikiwa na miaka 32 na yeye akiwa na miaka 24 wakati huo. Mke wangu ni mwenyeji wa Iringa na mimi ni mwenyeji wa Lushoto, mkoani Tanga. Tulikutana hapa Dar es salaam, mimi nikiwa mfanyabiashara naye akiwa amemaliza kozi ya ualimu daraja ‘A’ akisubiri kwenda kufundisha.

Tulianza uhusiano na alipopangiwa kituo cha kazi Kyela, nilimwambia asiende. Alisema ni lazima aende akaonje ualimu ambao aliusomea kwa miaka miwili. Alikwenda, lakini baada ya miezi sita alirudi akidai hawezi. Nilimwomba aache ualimu na kufanya biashara. Tulikubaliana. Tulioana wakati huohuo na kuanza maisha ya mke na mume. Tulikuwa tukiishi Mburahati wakati huo, ambapo baadae hata hivyo tulihamia Sinza. Tulikaa kwa miaka mitatu bila mke wangu kupata ujauzito. Ndugu walianza maneno na mke wangu alianza kubabaika. Nilimtuliza na kumwambia, angekuja tu kupata ujauzito.

Hadi mwaka 1980 yaani miaka sita baadae, mke wangu alikuwa bado hajapata ujauzito. Ndugu zangu walianza kelele na vurugu za kila aina, wakidai nioe mke mwingine. Nilipuuzia maneno yao, ingawa yalianza kuniingia kidogokidogo. Mwaka 1981 niliwaza njia ambayo niliona ingesaidia kuondoa kero zote. Nilimwambia mke wangu afunge maguo tumboni na kuonekana kama ana ujauzito. Aliponiuliza sababu , nilimwambia afanye tu hivyo. Alibishabisha awali, lakini nilipomuuliza kama haniamini, aliamua kunikubalia ombi langu.

Alipovaa maguo hayo na kuonekana kama mwenye ujauzito nilianza kutangaza kwamba mke wangu ni mjamzito. Nilitangaza kwa ndugu, jirani na hata kwa jamaa zangu wa karibu. Ilipofika miezi saba baada ya kutangaza hivyo nilimwambia mke wangu ni muda mzuri sasa wa kuaga kwamba anaenda kwao. Nilikuwa wakati wote huo nahangaika kutafuta namna ya nitakavyoweza kuwezesha kile nilichokuwa nimekibuni. Ni kweli aliondoka kwenda kwao. Wiki ile ile aliyoondoka, nilifanikiwa kupata nilichokuwa nataka.

Nilikuwa nimezungumza na wahusika wengi sana wa maeneo mbalimbali ambao wangeweza kunipatia mtoto mchanga. Mama mmoja ambaye naomba nisimtaje jina alipata mtoto mchanga. Mtoto huyo alikuwa amezaliwa hospitalini {naomba nisiitaje} na mama yake akafariki. Hakutokea mtu kumdai mtoto, wala maiti ya mama yake na huyo mama alijifanya ni ndugu wa marehemu, mara tu alipofariki. Kwa kutumia fedha kidogo nilizokuwa nimempa aliruhusiwa kumchukua mtoto yule akamlee. Ukweli ni kwamba hakuna ndugu wa yule msichana aliyejitokeza hapo hospitalini………….

Kwa kusindikizana na mama huyu, tulisafiri kwenda Iringa kwa mke wangu. Mke wangu hakuwa ameenda kuishi kijijini bali alikuwa akikaa hotelini, pale Iringa mjini. Tulipofika pale hotelini, nilimkabidhi mke wangu kachanga kale nakusema ni kake kuanzia wakati ule. Kalikuwa ni katoto ka kike kazuri. Kwa mara ya kwanza mke wangu alijua mpango wangu. Ilibidi niondoke na mke wangu kwenda naye kijijini kwao, ambapo tulipofika tuliwaambia alikuwa amejifungua njiani. Nilimwacha kule na kurudi Dar es salaam, kutangaza kwamba mke wangu amejifungua mtoto wa kike. Siwezi kusema furaha iliyokuwepo kwa ndugu zangu na wa mke wangu. Tukawa wanandoa wenye mtoto mmoja kwa njia hiyo.

Mwaka 1987 ndipo tulipoanza kushangazwa na binti huyu, akiwa na miaka sita wakati huo. Kwanza, alikuwa ni binti mkatili sana, tangu akiwa mdogo tu wa miaka mitatu. Alikuwa anapenda sana kukwangua wengine tukiwemo sisi. alipoanza kuzungumza, alikuwa akizungumza maneno ya ajabu, lakini ya kutisha pia. Mara nyingi alikuwa akipenda sana kutaja kufa, kuumwa na nyoka, kupanda mlimani, kufukiwa gizani na mengine ya aina hiyo. Alikuwa akipenda sana kusikiliza kwa makini watu wanapokuwa wakizungumzia mambo ya uasi kuliko mambo mazuri. Hii tabia tuliigundua alipokuwa na miaka mitano.

Akiwa na miaka sita, tukio la kwanza lililotushtua ni lile la kumwambia mama yake, hana adabu, alimwambia hivyo kufuatia kumwambia , akinywa chai awe anaondoa kikombe chake mezani na kukipeleka jikoni. Mama yake alimchapa. Kwa kawaida mtoto wa miaka sita akichapwa, mtu anategema akiona akilia. Huyu hakulia, bali alimwangalia tu mama yake vibaya na kuondoka. Siyo siri, niliogopa sana. Mwaka 1994 alipokuwa darasa la saba alifanya vituko vingi sana na tulihangaika sana kutafuta suluhu. Ili kupunguza maumivu, tuliamua kumpeleka shule ya sekondari ya bweni mikoani. Tulimpeleka. Lakini hata mwezi haukuisha alikuwa amerudishwa kutokana na kushindikana.

Alikuwa na kila aina ya visa. Alikuwa akitukana waalimu, kupiga wanafunzi wenzie na kuanzisha vurugu za aina mbalimbali. Ajabu ni kwamba, ukiwa umekaa naye na kuzungumza naye, anakuwa mtoto mzuri na msikivu sana. Anaweza hata kulia, kujutia makosa yake. Lakini baada ya hapo ndio anakuwa ametiwa moto. Kwa mwaka mmoja wa kidato cha kwanza, tulimbadilisha shule kiasi cha sita. Alipoingia kidato cha pili ndio vurugu zikawa kubwa zaidi. Lakini sasa hapa akawa ameanza tabia za uhuni, yaani kushiriki ngono.

Hali hii ya kupenda kushiriki mapenzi ilitukera sana na tulijua kwamba tumeshapoteza mtoto tayari. Lakini katikati ya tatizo hili, likazuka lingine. Hili ndilo lilikuwa kubwa zaidi. Alikuwa mara nyingi akidai kwamba ana hamu na mama yake. Tulipokuwa tukimwambia kwamba mama yake yupo hapo nyumbani, yaani mke wangu, alikuwa akisema hana uhakika sana kama hadanganywi. Kusikia hivyo, nilijua yule mama aliyenisaidia kumpata alikuwa amemwambia siri yote. Nilipomwendea na kumuuliza alisema asingeweza. Lakini alisema hata mama yake halisi na yule mtoto, kabla hajafa alikuwa akiropoka mambo mengi makubwa na ya kutisha. Ilibidi sasa niombe ushauri kwa watu mbalimbali, kuanzia kwa mashehe, mapadri, waganga na madaktari, lakini hakuna kilichobadilika.

Kila mmoja alijaribu kumsaidia kwa namna yake lakini, bila mafanikio. Pamoja na Vituko vyake na kauli za kutisha, hasa hizo za kumtaka mama yake na kusema anahisi haambiwi kweli, bila kufafanua, alimaliza kidato cha nne mwaka 1999. Wakati huo alikuwa anaumwa
sana hata hivyo. Tulijaribu kumsaidia sana kwa matibabu na kumtunza.

Tulikuwa tunampenda sana pamoja na visa na vituko vyake. Mwaka 2000 alizidiwa sana na maradhi na tulilazimika kumfanyia vipimo zaidi na alibainika kwamba ameathirika kwa ukimwi. Hatukumpa matokeo ya vipimo hivi awali,lakini alitushangaza aliposema, 'mnanificha kitu gani, siogopi kama mnavyofikiria. Kwani mtu kwenda kuungana na mama yake kuna tatizo?' Kwa kuwa nilishamzoea kwa visa vingi lukuki, sikustuka sana, ingawa mke wangu alishtuka kupindukia.

Mwaka 2001 alizidiwa kabisa na sasa alikuwa akikaa nyumbani tu. Siku moja mwezi wa Juni aliomba apewe jina la ukoo wa mama yake, kabla hajafa. Hapo tuliogopa vizuri sana kwa kweli na siwezi kuisahau siku hiyo. Tulimpa jina la ukoo wa kwa mke wangu, alikasirika sana na kusema anataka jina la ukoo wa kwao. Alisema akifa bila jina hilo, mambo yasiyopendeza yangetokea na kwamba asingepaswa kulaumiwa kwa hilo, kwani kazi tuliyofanya ingekuwa imepotea bure.

Tuliogopa sana na ilibidi niende kwa yule mama aliyenifanyia mpango wa kumpata binti huyu na nilizungumza naye. Alisema, ingekuwa ni vigumu kwake kupata taarifa za yule mama yake. Lakini kwa bahati alikumbuka jina na ubini na kwamba, yule mama alimwambia alikuwa ametokea kijiji cha Puge, Nzega, Tabora. Alimwambia alifika Dar es salaam kwa kudanganywa na mtu ambaye alimleta Dar na kumtelekeza baada ya ujauzito.

Nililazimika kusafiri hadi huko Puge, nilipofika hapo kijijini {Ni kijiji lakini ni
kama kamji kadogo} nilidadisi na kupata taarifa kumhusu yule mama. Sikusema chochote, zaidi ya kurejea Dar es salaam. Nilivyoambiwa kule ni kwamba, yule mama wa mtoto wetu alikuwa apewe kitu walichoita Mkoba {Uganga bila shaka} ya bibi yake mzaa baba, lakini akakataa na kukimbilia kusikijulikana.

Huku Dar es salaam alikuja mwenyewe na kukutana na huyo tapeli aliyempa ujauzito. Inaelezwa kwamba, bibi yake alikufa akiwa hajakabidhi mikoba ya uganga kwa yeyote. Hayo niliyaamini ingawa kabla ya tukio hili, kama ungenitajia jambo kama hilo, ningekutemea. Nilirudi Dar na nilipofika nyumbani, hali ya binti yetu ilikuwa mbaya sana. Nilimsalimia na kumwambia kwamba tunampa jina {Naomba nisilitaje}. Aliposikia jina hilo aliinua kichwa, jambo ambalo alikuwa hajawahi kulifanya tangu kuzidiwa kwake na ugonjwa.

Halafu alirudisha kichwa kwenye mto na kufariki hapohapo. Naomba uniamini kwa faida yako, kwani hilo, lilitokea mbele ya macho yangu. Sioni faida ambayo mimi au wewe utaipata kwa uongo ambao nitaufanya katika suala hili. Mwaka huo huo akiwa na miaka 41 mke wangu alijifungua mtoto wa kike. Ilikuwa kama ajabu kwetu na mshangao huo hauwezi kututoka hata siku moja. Lakini hata kama atakuja mtu gani tukubali kuwa hakuna miujiza na nguvu za ajabu kwenye maisha, tutambishia hata kwa thamani ya damu yetu, kwa sababu tumeona kwa macho yetu.

Mimi na mke wangu tumeumizwa sana na kilichotokea na hasa matukio ya yule binti yetu ambaye tulimlea kwa upendo. Tumekuwa tukijiuliza kilichotokea bila kupata jibu.
 
stori yako inasisimua kwa kweli ila hapa kwenye umri wa mkeo kujifungua ndo nina shaka napo...ulisema mmekutana na kuwa pamoja mwaka 1974...kipindi hicho wewe una miaka 32 na mkeo 24... sasa tokea 1974 mpaka 2001 mkeo alipojifungua nafikiri ni miaka 51 alikuwa nayo na si 41, na pia huyo bi mkubwa kujifungua katika umri huo hapo ndipo kwenye miujiza ya kweli...
 
I am glad haikuhusu wewe,
naweza iamini kwani nimejifunza there is a lot going on kwenye hii
ardhi. The fact kwamba hujashuhudia does not mean kuwa hayapo.

Kuna issue imetokea recently hapa Kigoma,
Anakuja mdada nyumbani kwako, na kujiintroduce as a distance relative na
kukutajia maisha yako na ya watu wako wa karibu wote (anavaa uhusika
kisawa sawa), anakaa siku kama mbili halafu anaondoka na mtoto wako wa
kike less than 2 yrs. Baada ya muda (hadi miezi) unakuja mpata wilaya au
mtaa mwingine kabisa unharmed.

Amefanya hivyo kwa familia moja ninayo ifahamu, over the course ya
kuhangaika wakakuta hiyo story kwa watu wengine kama 6 hivi (police
kituo cha mjini Kigoma wanaifahamu). Huyo dada anajulikana kwao kama
Kabula (jini Kabula), na inasemekana anawapeleka hao mabinti ziwani God
knows nini kinafanyika huko.

Kwa kweli mambo mengine yanatisha sana, usiombe kukutana nayo!

Mh! Hayo sasa mauzauza.
 
sad story kwa kweli
Kaunga umenikumbusha kigoma enzi zangu za kuvinjari website,sandra kwa mrefu na sunside bila kusahau kibirizi sijui kama bado zipo
kwa kigoma kesi nyingi za jinai ni kuhusu watoto kubakwa na kufanyiwa vitendo kama hivo sijui tatizo nini limewakumba waha.
naimis sana kigoma hasa maeneo ya kilimahewa na disco la j2 bangwe mchana kweupe.

I am glad haikuhusu wewe, naweza iamini kwani nimejifunza there is a lot going on kwenye hii ardhi. The fact kwamba hujashuhudia does not mean kuwa hayapo.

Kuna issue imetokea recently hapa Kigoma,
Anakuja mdada nyumbani kwako, na kujiintroduce as a distance relative na kukutajia maisha yako na ya watu wako wa karibu wote (anavaa uhusika kisawa sawa), anakaa siku kama mbili halafu anaondoka na mtoto wako wa kike less than 2 yrs. Baada ya muda (hadi miezi) unakuja mpata wilaya au mtaa mwingine kabisa unharmed.

Amefanya hivyo kwa familia moja ninayo ifahamu, over the course ya kuhangaika wakakuta hiyo story kwa watu wengine kama 6 hivi (police kituo cha mjini Kigoma wanaifahamu). Huyo dada anajulikana kwao kama Kabula (jini Kabula), na inasemekana anawapeleka hao mabinti ziwani God knows nini kinafanyika huko.

Kwa kweli mambo mengine yanatisha sana, usiombe kukutana nayo!
 
Hapo wala sishangai mzee Mtambuzi,kwani kisa kama hicho kinatusumbua katika ukoo wetu mpaka leo lakini chenyewe ni tofauti kidogo.Dada yangu mtoto wa mama mkubwa alikuja kuishi nasi Dar 1984 toka kijijini.1988 akajifungua mapacha ambao baba yao(mngoni) aliwakataa akisema hamjui binti huyo.Baada ya watoto kukua dada huyo alirudi kijijini na kuolewa na bwana mwingine na hata hajui baba wa watoto wake(wale mapacha) yuko wapi na hata ndugu wa mngoni huyo hawajui.Cha ajabu mmoja kati ya mapacha hao(wa kike) akawa anaanguka kama mwenye kifafa na kuzungumza lugha wasiyoielewa akiwa na hasira ajabu.Katika kutafuta ukweli wakagundua kuwa mtoto huyo anapoanguka huwa anaongea kingoni na kudai kuwa yeye ni malikia anayepaswa kurudishwa kwao ili akakalie kiti chake. Hapo ndio shida ilipo maana hawamjui baba wa mtoto huyo wala ndugu zake zaidi ya kufahamu tu mwenye ujauzito huo alikuwa ni mngoni....kisa hiki nimekifupisha ila ni kisa cha kweli kabisa ambacho kimemtokea mtoto wa mama yangu mkubwa........
 
Last edited by a moderator:

Subiri, kuna wadau humu watakuja kukushauri umpeleke huyo mtoto wa dada yako kwa Kakobe akaombewe............!
 
Kuna wasemao hakuna uchawi wakati uchawi upo. Wanadhani wakisema hakuna uchawi wataonekana watakatifu. Mi si mshirikina lakini ntapenda nijue ukoo ambao mwanangu anaoa.
 
Back
Top Bottom