Binti Achinjwa Kama Kuku huko Kahama_Kisa Mapenzi

Binti Achinjwa Kama Kuku huko Kahama_Kisa Mapenzi

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,093


VILIO vilitawala Kata ya Nyahanga wilayani hapa wakati wa kuuaga mwili wa binti Jessica Elialinga (19) aliyeuawa kinyama

kwa kuchinjwa kama kuku na mpenzi wake, Musa Petro (27) mkazi wa Shunu kwa sababu zinazodaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu.

Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu.

Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.

"Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha.

"Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine," alisema rafiki huyo.

Hata hivyo, inadaiwa baada ya mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi, lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza masomo.

Inadaiwa siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti huyo hakusimama kumsikiliza.

Baada ya Musa kudaiwa kufaulu kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.

Alipomhoji kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.

Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.

Watu waliobaki nyumbani walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea kupatiwa matibabu.
 
Kina dada kuweni makini sana na watu mnao DATE nao, msiingie ki kichwa kichwa kwasababu tu wana hela, nyumba nzuri na magari ya kutembelea.
Waangalieni, je wana uwezo gani wa kudhibiti hasira?
Je wana upendo kiasi gani?
Siamini kama mtu anayekupenda kwa dhati anaweza kukuchinja kama nyamafu
 
yana-run dunia
hivi dunia ya leo kuna wivu wa kipuuzi kama huo!madem wote hawa
 
::
Nchi ingekuwa yangu ningeagiza somo la JITAMBUE liandaliwe na kufundishwa tangu kidato cha kwanza hadi Vyuo Vikuu ili kunusuru kupoteza raslimali watu.
::
Ila kwa kuwa wapo watu maalum wa kufikiri ktk usahihi,
acha niomboleze kifo hiki.
=
 
Akina dada acheni kula hela za wanaume kama hamna mapenzi ya dhati.
 
Wakina dada jifunzen kama mtu anakugharamia nawe 2lia hata kama unaiba mapenz uwe makin
 
Kina dada kuweni makini sana na watu mnao DATE nao, msiingie ki kichwa kichwa kwasababu tu wana hela, nyumba nzuri na magari ya kutembelea.
Waangalieni, je wana uwezo gani wa kudhibiti hasira?
Je wana upendo kiasi gani?
Siamini kama mtu anayekupenda kwa dhati anaweza kukuchinja kama nyamafu



Umenena vema mkuu....

Ila sidhani kama wamekuelewa, kwa maana kuna msemo usemao ".......mwalimu wao kipofu".
 
RIP dada!!! So and very sad true story!! Come on guys, stop this idiotic methodologies!!!!
 
Namuimagine mzazi wa huyo binti!! Cjui wanangu nitawaficha wapi?!!
 
Pole sana familia yake! R I P. Wosia wangu kwa wadada! Jaman mapenzi yanaumiza sana hakuna haja ya kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja kwani uvumilivu na ustahimilivu wa Wanaume unatofautiana kama humtaki mtu ni afadhali kumkataa mapema na kamwe nasema tena kamwe usijaribu kula vya Watu vinaumiza
 
Duh, Dunia inapoelekea kutakua hamna ubinadamu kabisa.
 
Heee....! Habari nyingine hadi zinatetemesha....!
Mimi siamini kuwa mtu uliyekuwa unampenda unaweza kuchukua jukumu la kuondoa uhai wake hata kama amesalitiwa.
Nakumbuka imeletwa post ya mtu kutaka kujiua kwa wivu wa mapenzi huko Iringa mwaka huu huu.
 
Na hawa watoto wa kike wawe makini!!! alishindwa kuwaza masomo na kuanza kumzengea mchuna ngozi. Hebu fikiria kile kitendo cha kuchinja kimemuaffect vipi mpaka ashindwe kukuchinja wewe? wadogo zangu tuwe makini an haya mamboya wakubwa. RIP my young sister ila wengine kuweni makini. usijilegeze sana hata kama umefeli. Omba Mungu milango ming sana kwenye hii dunia. Poleni sana
 
Back
Top Bottom