Binti Achinjwa Kama Kuku huko Kahama_Kisa Mapenzi

Binti Achinjwa Kama Kuku huko Kahama_Kisa Mapenzi

Sasa mtu anachuna ngozi halafu unamchuna vijisenti vyake, sianapata wazimu? Kuweni makini mabinti.
 
wewe imagine una date na mchinja ng'ombe unategemea nini...kila kukicha yeye ni kuchinja tu..kuweni makini jamani na mahusiano yenu na nyie wadada msikurupukie tu wanaume...hebu fikiria mume mchinja ng'ombe,,,,mfanyakazi wa mortuary, askari mnyongaji...mtu wa madeal ya kuteka na kuua...unategemea nini hapo
 
Such an innocent girl!!!beautiful, natural! Mtu anamchinja! Katika literature zamani tulisoma theme ya self awareness and personality! Msichana au mtu yeyote ajitambue na kujifahamu kuwa anathamani na wajibu gani kwa wenzie na jamii nzima kwa ujumla. Ajue yeye akiwa msichana anakabiliwa na changamoto gani duniani na ajiandae vipi kukabiliana nazo! Jamani hata kama leo tuko kidigitali zaidi lakini sometimes old remains and will remain GOLD!!!!!!
 
kila mtu anasema tuwe makini.....tungekuwa makini MSINGEZALIWA

mix with yours
 
Such an innocent girl!!!beautiful, natural! Mtu anamchinja! Katika literature zamani tulisoma theme ya self awareness and personality! Msichana au mtu yeyote ajitambue na kujifahamu kuwa anathamani na wajibu gani kwa wenzie na jamii nzima kwa ujumla. Ajue yeye akiwa msichana anakabiliwa na changamoto gani duniani na ajiandae vipi kukabiliana nazo! Jamani hata kama leo tuko kidigitali zaidi lakini sometimes old remains and will remain GOLD!!!!!!

perception yako juu ya marehemu hata baada ya maelezo yoote kuhusu kuchuna nimeipenda sana

mix with yours
 
Heee....! Habari nyingine hadi zinatetemesha....!
Mimi siamini kuwa mtu uliyekuwa unampenda unaweza kuchukua jukumu la kuondoa uhai wake hata kama amesalitiwa.
Nakumbuka imeletwa post ya mtu kutaka kujiua kwa wivu wa mapenzi huko Iringa mwaka huu huu.
pia wiki iliyopita mbeya kuliwekwa habari juu ya bwana mmoja aliyemuua mwanamme aliyemfumania na mkewe kisha nae kutolewa roho na wanainchi.
 
​


VILIO vilitawala Kata ya Nyahanga wilayani hapa wakati wa kuuaga mwili wa binti Jessica Elialinga (19) aliyeuawa kinyama

kwa kuchinjwa kama kuku na mpenzi wake, Musa Petro (27) mkazi wa Shunu kwa sababu zinazodaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu.

Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu.

Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.

“Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha.

“Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine,” alisema rafiki huyo.

Hata hivyo, inadaiwa baada ya mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi, lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza masomo.

Inadaiwa siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti huyo hakusimama kumsikiliza.

Baada ya Musa kudaiwa kufaulu kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.

Alipomhoji kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.

Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.

Watu waliobaki nyumbani walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea kupatiwa matibabu.

ana miaka 19, alianza mapenz akiwa form 2, shule ya kata, nahs matokeo yake ni div 0, tume iliundwa ya nini? R.i.p dunia imekwisha
 
Sion kosa la huyu mtoto. Kupenda si dhambi. Watoto wanawah kukua na hisia zinawahi vilevile. Ila ukisikia mtu amekusaliti ndio unaua!!!! Ili nini??? Wanaume badilikeni. km hela zinakuuma usitoe, mtu maisha magumu afu bado anahonga!! Achen wenye hela zao wahonge. Apo huenda hela alizohonga jumla haifki ht laki!!!! Ujinga
 
Daa amekatizwa maisha kwa wivu wa kipumbavu wa mchuna ngozi!nahisi huyo kijana anatumia bangi sana pia hana confidence sababu ya shule!
 
Back
Top Bottom