Bwana Paul Kijoka,
Hapo naomba nimtetee TB Joshua (haimaanishi kwamba nina amini unabii wake, maana sijui anatumia nini). Kama Mugabe ndo angekufa, then ningeweza kusema unabii wa TB Joshua una walakini. Maana siyo siri tena kwamba Bob Mugabe anaumwa saratani na alishaambiwa na madaktarri wake kwamba anaweza kuishi kwa miaka 5 (hii ni according to ule mtandao wa kutoa siri za cables WIKI).
Mutharika kama wiki 2 au 3 zilizopita alitamka kwenye vyombo vya habari kwamba utabiri wa TB Joshua haumlengi yeye, maana yeye ni mzima wa afya, hana matatizo ya afya. Ni rahisi kutoa prognosis ya mgonjwa wa cancer kuliko magonjwa mengine kama ya moyo ambayo hutokea ghafla bila kubisha hodi. Mfano mzuri ni juzi jinsi mchezaji Muamba alivyozimia ghafla na "kufa kwa muda wa dakika 78", before that he was very fine na alikuwa uwanjani akisakata kabumbu. Kwa hiyo hata kama TB Joshua angekuwa na detailed info za ugonjwa wa moyo wa Mutharika, bado asingeweza kutabiri maana wapo wagonjwa wengi sana wa moyo ambao huishi miaka mingi sana na wengine huwa wana magonjwa ya moyo lakini hawajui kama wanaumwa.
TB Joshua alisema Rais huyo anatokea Kusini na ni ambaye umri umeenda. Wengi walielekeza macho kwa Mugabe maana ndo mzee sana kuliko wenzake Angola, Zambia na Malawi (hawa wote walikuwa kwenye late 70s). Baada ya huo unabii (utabiri?) wananchi wa Zimbabwe walishakaa mkao wa kusubiri breaking news, bahati mbaya imekula kwao, breaking news imeenda Malawi, Mwisho, TB Joshua alisema kwamba Rais atakayekufa, atafariki kwa ugonjwa na kifo chake kitakuwa cha ghafla.
Kwa hiyo sina hakika kama anaweza kufanya mawasiliano na kujua details zote hizo. Hapa cha kujiuliza ni kwamba je ni maono kutoka kwa Mungu au anatumia nguvu za kiza?
Hayo ni maoni yangu tu, wafuasi na waumini wa TB Joshua naomba msinitoe macho.