Faida za hii kozi; Kozi inatoa wigi mpana kwa mhitimu. Ana wigi mpana wa kuajiriwa, kujiajiri. Watu wengi wa darasa letu ni Maafisa Mipango kwenye maalmashauri, Wachumi, Bankers, finance planners and analysts, NGO sectors pia imewachukua wengi na sekta binafsi kwa ujumla wana soko huko. Kama mtu ataweza kupat mtaji na kujiajiri, anaweza kuwa mzuri sana kwenye eneo hilo hasa mipango, usimamizi na ubunifu.
Hasara ya kozi hii; Hii kozi pamoja na kukupa wigo mpana wa kuajirika lakini bado haimpi mhitimu ujuzi wa yeye kujiajiri moja kwa moja kwa ujuzi huo, tofauti na ilivyo Agronomy. Maana mtu wa Agronomy anasoma General Agriculture studies, anaweza kufanya ugani au farm mechanization vizuri. Ni kozi inamjengea mtu kuwa analyst au planner mzuri, lakini inakosa ujuzi wa moja kwa moja ambao mtu anaweza kuutumia kukabiliana na mazingira yake.