Binadamu tuna mambo

Balungi

JF-Expert Member
May 25, 2011
234
162
Unakuta mtu anakujia na shida zake umuazimishe pesa ana matatizo mfano Tsh 250,000/- sasa kimbembe ni wakati wa kulipa deni, anakuuliza nikutumie mtandao gani,

Ukimwambia na yeye anakutumia kiwango kile kile ulichompatia kwa cash yaani Tsh. 250,000/- bila fedha ya kutolea. Sasa unabaki unashangaa kuwa unatakiwa ukatwe wewe pesa ya kutolea, kweli tenda wema uende zako.
 
Shukuru hata hivyo ulipata kwa M-pesa.

Wengine wadeni wetu wamehama na mitaa na namba za simu wamebadili.

We shukuru tu umelipwa, Ya kutolea ongezea wewe hesabia kuwa ulitoa ofa baa.
 
Ameniumiza kidogo maana hata nilipomwambia hakuonesha kujali
 
Si ushukuru huyo kakulipa, mi siku hizo sikopeshi ila nilitaka kumsaidia mtu nitafanya hivyo ila akija na gia ya kukopa lazima agonge mwamba
 
Back
Top Bottom