KERO Bima ya Afya ya NHIF kwenye kifurushi cha Toto Afya ambayo kinauzwa 150,000/= ni kero

KERO Bima ya Afya ya NHIF kwenye kifurushi cha Toto Afya ambayo kinauzwa 150,000/= ni kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nina jambo ambalo linaumiza sana aisee, ni kuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye Kifurushi cha Toto Afya ambayo kinalipiwa Shilingi 150,000/=.

Mtoto wangu amezaliwa na tatizo la maji mengi kichwani (Hydrocephalus) na akafanyiwa operation Hospitali ya Taifa Muhimbili, anatakiwa kuendelea na clinic pamoja na mazoezi lakini cha ajabu hiki Kifurushi cha Toto Afya hakina uwezo wa kulipia mazoezi, na ukienda kwenye clinic zake za kichwa dawa zote muhimu kwa mfano ya degedege, haipo kwenye bima.

Inachoweza kufanya ni kulipia kuona daktari pamoja na vipimo vya kawaida sana kama damu lakini vile vyote vikubwa na muhimu ni lazima ulipe cash.

Kwahiyo hapa utu kwa watoto upo wapi jamani, wazazi wenye hawa watoto tunateseka sana na bima imekuwa sio msaada kabisa.

Tunaomba JamiiForums mtusaidie kupaza sauti zetu Wazazi tunaumia sana.
Screenshot 2026-02-12 102122.jpg

Screenshot 2026-02-12 102521.jpg
 
Mbona vifurushi husika vimeeleza vizuri hadi ukomo wa gharama?
Usikate tu bima kisa bei rahisi, soma kwanza uelewe unanufaika vipi.
 
Hili ni jambo la muhimu sana, sema watu wanakimbilia kwenye price
Hakuna BIMA utalipa 150,000 utibiwe magonjwa yote.
Kilio kingine kitakuja kwenye hii ya 150,000 watu 6
NHIF wenyewe BIma yao nzuri ni kuanzia 600,000 kwa watoto wadogo
Hiyo anapata matibabu hadi 5mil OP na 21mil IP
 
Back
Top Bottom