Bill Gates: Kosa kubwa la muda wote ni kuacha Android kuongoza.

Sally Salya

Member
Feb 7, 2019
38
24
Habari wana JF !
Katika mahojiano ya hivi karibuni , mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amenukuliwa akisema kuwa katika moja ya kosa lake kubwa la wakati wote alilolifanya ni kuiacha Android kuongoza katika mifumo ya uendeshaji duniani.
Bill Gates alisema, ```Katika ulimwengu wa program anayeongoza katika kuwa na program endeshaji inayotumika kwenye vifaa vingi zaidi ndiye anakuwa mshindi wa masoko yote.
Microsoft ilijaribu kuleta program endeshaji spesheli kwa ajili ya simu iliyokwenda kwa jina la Windows Mobile kwa upande wa simu zake za Windows Phone lakini haikupokelewa vizuri sokoni na pia kwa watengenezaji wa Apps. Microsoft ikajikuta bado inabaki ikitamba katika kompyuta zaidi.
* Microsoft ishakata tamaa katika soko la program endeshaji ya simu, tayar washatuma ujumbe kwa watumiaji wake wa simu za Windows 10 Mobile ya kwamba kufikia Disemba mwaka huu hawataweza kupata masasisho tena ya program endeshaji yao na hivyo wahamie kwenye simu za Android au iOS.

``Source#teknolojia.co.tz
 
Andoid ashaingia pia kwenye pc. Nako wawe na tahadhali
 
Android ni Android na PC ni Pc. Pamoja na wingi wake Android mpaka leo vitu basic kabisa vya production Haina Kama vile Photoshop, decent video editor, Hata full Microsoft office hakuna.

So windows na Android vimegawana, Android imechukua zaidi kwenye consumption ya vitu mfano kuangalia video, games za hapa na pale, kusoma vitabu etc

Windows yenyewe ipo kwenye Creation, ukitaka kutengeneza chochote iwe ni video, kutengeneza picha, ramani za nyumba etc utahitaji windows.
 
so hata iweje ni ngumu android kumpita hata aboreshe vipi?
 
Android ni user friendly sana ndo maana wanapiga bao.

Mfano mimi natumia Windows 8.1 mama enu mdogo imemshinda hadi ananambia bora nimtafune kuliko kutumia windows 8
 
Back
Top Bottom