Bill Clinton Bowing Down For Barack Obama

Ameboresha pensheni kwa wastaafu; amejenga mahusiano mazuri ktk ulimwengu wa Waislamu; masuala ya nuclear hatuyasikii sana siku hizi; rate ya ukosefu wa ajira kidogo imepungua; amepunguza makali ya financial crisis kwa kutoa stimulus ya $ 789 bilioni; Kibano kwa Obama; kuweka ratiba ya kuondoa majeshi ya US kule Iraq; sera ya climate change n.k.

Kwa upande wa elimu amefanya makubwa kadhaa ikiwa ni pamoja na:
  • Kuongeza ratiba ya wanafunzi kubaki shuleni hadi saa 10 alasiri badala ya saa nane mchana
  • Wanafunzi kuvaa sare shuleni kuliko ilivyozoeleka kama wanaenda disco
 
Rais wa zamani wa Marekani Mzee Bill Clinton Amuinamia Rais Barack Obama.

561132_429024763827634_2097067265_n.jpg

hiyo ni ishara ya kifree mason
 
Kwa upande wa elimu amefanya makubwa kadhaa ikiwa ni pamoja na:
  • Kuongeza ratiba ya wanafunzi kubaki shuleni hadi saa 10 alasiri badala ya saa nane mchana
  • Wanafunzi kuvaa sare shuleni kuliko ilivyozoeleka kama wanaenda disco

Mzee hii naona unatia chumvi sasa
 
utapata dhambi ukikitaja kifo cha gaddaf bila kumhusisha mmarekani hata kama hakujihusisha moja kwa moja sababu hao wa ulaya marekani ni mume wao.
 
Mzee hii naona unatia chumvi sasa

Mwanzoni kabisa mwa awamu hii, Obama alilitangazia taifa la Marekani kuwa anapendekeza muda wa kuwa shuleni wanafunzi kuanzia grade one to eight uongezwe kwa sababu zifuatazo:
  • Kuwapa nafasi wazazi na walezi kuwachukua wanafunzi mashuleni watokapo makazini, maana kaida ilikuwa wanatoka saa 8.
  • Watoto wasiwe na muda mrefu wa kuzubaa mitaani wakati wazazi wangali makazini
  • Kupata muda zaidi kwa kuongeza vipindi madarasani.
Kumbuka mabadiliko Marekani huchukua muda kutegemeana kila state inavyo respond kwa jambo hilo, na kuna state kadhaa zimeshafanya mabadiliko hayo ya ratiba na nyingine ziko mbioni.

Wanafunzi kuvaa sare ni jambo mojawapo ambalo alilikazia, kama kawaida kumekuwepo na mikakati ya kurudisha hadhi ya wanafunzi kuvaa sare, na kuna baadhi ya state zilishapitisha sheria hiyo na kuachia board of education kufanya uhakiki na muda wa lini utaratibu huo uanze. Ninavyoandika hapa kuna baadhi ya state utaratibu wa wanafunzi kuvaa sare umeshapitishwa na baadhi wameshaanza kuvaa. Wengine wako mbioni na wengine watafuata ujuavyo Marekani ni papo kwa papo, huchukua muda hadi taratibu zikamilike. Kama wakumbuka ile bima ya afya kwa wote licha ya kuwa sheria lakini utekelezaji wake bado uko mbioni.
 
Back
Top Bottom