Bilioni tano kusaidia afya ya bure Afrika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Bilioni tano kusaidia afya ya bure Afrika
t.gif
_46431520_001676522-1.jpg

Malawi ni mojawapo ya nchi zitakazonufaika na msaada huo. Watu wasiopungua milioni 10 katika nchi zinazoendelea wanatarajiwa kupata huduma ya afya bure, watu hao watanufaika kutokana na mpango uliozinduliwa na Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown.
Nepal, Malawi, Ghana, Liberia, Burundi na Sierra Leone zinasema zitaongeza upatikanaji wa huduma ya afya kama sehemu ya mpango huo.
Mpango wenyewe, uliozinduliwa kwenye Umoja wa Mataifa, unagharamiwa kwa dola bilioni tano za Marekani.
Bw Brown alisema dunia inatakiwa kuona aibu na ichukue hatua za kuzuia vifo vya watoto.
Kwa mwaka mmoja uliopita, Bw Brown na mkurugenzi wa Benki ya Dunia, Robert Zoellick, wamekuwa wakiongoza kikosi kazi cha kimataifa kuchangisha fedha kusaidia kuimarisha huduma za afya katika nchi zinazoendelea.
Kati ya dola bilioni tano ambazo zimepatikana, dola bilioni tatu zimetokana na michango ya hiari iliyohamasishwa kupitia makampuni yanayouza huduma za utalii kupitia tovuti.


http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2009/09/090924_msaada_afya_afrika.shtml
 
Ndugu yangu hakuna cha bure, hizo huduma zinalipiwa and this is something everyone should know

Hata ka lugha ka bure, bure, bure ndio kanakowapa wanasiasa platform ya kutupa upupu wao!!!! Lets all tell the truth, hata hizo dawa za ukimwi sio bure but somebody is paying for the drugs

I hope one day yes!!:confused:
 
Back
Top Bottom