Bilioni 4 Kujenga Ambulance Boat Kupitia TASAC Ziwa Viktoria, Mwanza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

BILIONI 4 KUJENGA AMBULANCE BOAT KUPITIA TASAC ZIWA VIKTORIA, MWANZA

Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) December 22,2023 imetia saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa boti yenye vifaa vya matibabu (Ambulance Boat) ambao umesainiwa baina ya TASAC na Kampuni ya LOCA Muhendislik Gemi Mak. PLas Ve Gd. San Tic ltd Sti ya nchini Uturuki kwa kiasi cha Tsh. bilioni 4.2 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 12.

Naibu Waziri was Uchukuzi, David Kihenzile leo amemwakilisha Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa Jijini Mwanza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa boti yenye vifaa vya matibabu (Ambulance Boat) ambao umesainiwa baina ya Shirika la Usalama wa Meli Tanzania (TASAC) na Kampuni ya LOCA Muhendislik Gemi Mak. PLas Ve Gd. San Tic ltd Sti ya nchini Uturuki kwa kiasi cha Tsh. bilioni 4 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 12.

Kihenzile amesema “Leo nimeshuhudia utiaji saini wa kuanza kujenga Hospitali inayotembea majini, ni boti ya Tsh. bilioni 4.2 itakuwa na vifaa vyote vya kisasa kwa ajili ya matibabu ya waliopata ajali majini, speed yake ni 30 KM/HR na inaweza kwenda umbali wa Kilometa 278, ujenzi wake ambao unafanyika Ziwa Victori Mwanza utakamilika baada ya miezi 12.

“Wito wangu kwa Mkandarasi na TASAC ni kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati ma Viwango, nimewasisitiza TASAC kuhakikisha wanaendelea na kaguzi za mara kwa mara ili kuhakikisha usalama wa usafiri huo unazingatiwa
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.31.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.31.jpeg
    126.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.32.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.32.jpeg
    126.2 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.36.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.36.jpeg
    147 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.35.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.35.jpeg
    97.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.35(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.35(1).jpeg
    136.6 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.34.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-23 at 04.54.34.jpeg
    118.4 KB · Views: 7
Back
Top Bottom