Pascal_TZA
Member
- Mar 25, 2014
- 35
- 101
Kikao maalum kwa ajili ya wanaume kitafanyika April 2, Mlimani City na kimeandaliwa na @prophetipm kikilenga kuwakutanisha wanaume watu wazima pamoja na vijana ili kujadili masuala muhimu yanayohusu maisha, maadili na juhudi za kujiletea maendeleo binafsi.
Miongoni mwa wazungumzaji ni mfanyabiashara bilionea @lugumisaidi ambaye anatajwa kuwa mfano wa mafanikio kwa vijana wengi nchini Tanzania na barani Afrika. Uwepo wake unatarajiwa kuleta hamasa kubwa kutokana na safari yake ya maisha na mafanikio aliyoyapata kupitia juhudi, nidhamu na uthubutu katika shughuli za kibiashara na kijamii.
Akieleza sababu za kumualika @lugumisaidi kuwa mzungumzaji, @prophetipm amesema “Sababu ya kumualika Lugumi ni upendo wangu kwake, ana upendo , hajivuni lakini pia ana ushawishi Tanzania kwa namna anavyoishi , anasaidia watu , anahudumia yatima, nikaona vijana wengi wa Tanzania wanatamani kufanikiwa sasa yeye anayo mengi ya kuwa-inspire vijana, wanaume wa Afrika kujifunza namna ya kupambana, naamini maneno atakayozungumza machache yataenda kubadilisha maisha ya watu, watakuwa na morali mpya kwenda kufanya kazi kujifuma kupambana katika maisha”
Aidha, waandaaji wa kikao hicho wanaamini kuwa ujumbe utakaotolewa na wazungumzaji, hususan Lugumi, utaweza kuwajengea washiriki morali mpya ya kufanya kazi kwa bidii, kujitegemea na kupambana ili kufikia ndoto zao. Wanatarajia kuwa mafunzo na ushauri vitakavyotolewa vitachangia kubadili mitazamo ya wanaume na vijana wengi na kuwahamasisha kuwa watu wenye maadili mema na mchango chanya katika maendeleo ya jamii. 💼✨📣