bila simu yangu...

Rubi

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,622
1,225
huwa nagombezwa mara kwa mara na bosi kila nikutapo missed call yake na hata mpenzi akinikosa kwenye simu hufikiria nimefanya kusudi au nilikuwa na yangu nikambania.

Bila simu ni matatizo siwezi kuwasiliana na ndugu zangu hasa wakati wa dharura.

Bila simu nakua kama niko kwenye kichuguu chenye giza totoro nisijue yanayoendelea ulimwenguni,
Bila simu kila nitembeapo nashitukashituka nikihisi nimepoteza kitu.
Kuwa na simu kunafanya maisha kuwa rahisi wakati mwingine na kinyume chake ni magumu hasa pale unapohitaji kusaidiwa kwa haraka i.e umefiwa, umepata dharura yoyote, unagonjwa n.k.

Simu imerahisha mengi hasa zile zenye kitochi, internate na radio we acha kabisa.
 

Negrodemus

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
2,303
2,000
siwezi kujua:
1. saa hizi ni saa ngapi..
2. leo ni tarehe ngapi..
3. namba hata moja ya simu
4. njia iko wapi umeme unapokatika ghafla
5. majibu ya haraka haraka kwenye quiz na assignments,

kiufupi simu yangu ni kama mkono wangu wa ziada...

ongezea hapo vitu gani bila simu yako ingekuwa ni miujiza kufanyika

ilinipa kazi utumishi.......

ile simu yangu ipo kwenye kabati la kumbu kumbu ni nokia E71..

nilikabidhi moja moja nikabaki nayo full kugoogle
 
Top Bottom