Bila Shaka CCM inahitaji utulivu ili nchi itulie

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Ni wazi wapinzani wa CCM watatumia fursa zote halali na haramu ili kuimaliza CCM ikiwa madarakani na ni haki yao kufanya hivyo.

CCM ilipoteza mvuto kipindi flani hadi kufanya zoezi la kuvua gamba japo gamba liliishia kiunoni.

Mwaka 2015 CCM ilipitia changamoto nzito sana baada ya mgawanyiko mkubwa ambao kidogo utoe fursa kwa wapinzani.

Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alitokea au aliletwa kuokoa jahazi akiambatana na Rais Samia.
wawili hawa waliisimamia na kuitekeleza vyema ilani ya CCM na hatimaye 2020 upinzani ukapotezwa kabisa.

Ni bahati mbaya combination adimu ya Magufuli na Samia inapotea mwaka 2021 ghafla .

WITO:Kamwe tusikate tamaa au kuogopa au kuchonganishwa.

Wananchi wametekeleza nafasi yao yaani wamempa heshima Magufuli na CCM kwa kujitokeza na kuionesha dunia kuwa CCM ilikuwa sahihi kuwaleta wagombea Magufuli na Samia.
Ni mategemei ya wananchi wengi wanyonge na wapiga kura kuwa ilani ya CCM itatelelezwa hata kama mpendwa wao atakuwa ametangulia mbele ya haki.

Kipimo chao ni utekelezwaji wa Ilani ya CCM tena kwa kasi ile ile.
wananchi hao hawakuamini upinzani na propaganda au matakwa yao ya kibeberu bali walitaka zahanati na shule karibu yao,walitaka kufanya biashara zao ndogo ndogo bila bugudha,walitaka wasiwe sehemu ya mikopo ya chuma ulete inayofanywa na wafanyabiashara wanyonyaji,walisikitika kuona wanaojilimbikizia mali na kiwamwagia tope za V8VR barabarani,wslichukizwa na lugha za dharau za watoa huduma na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa,walikasirika kuona wakinyimwa kuwinda swaka halafu twiga wanapanda ndege,walichukia kuonwa kama wajinga.

toka mwaka 2010 walitaka kuiadhibu CCM Lakini baada ya 2015 wameiamini CCM kwa asilimia 98% .

sasa CCM inayo kazi ya kuwaaminisha kuwa bado CCM itaendelea kuwa CCM adilifu.
yote yanawezekana iwapo CCM itatulia kwanza kwa kuendelea na maombolezo ya kumpoteza jemedari Magufuli.

CCM HUWA HAINA HARAKA KATIKA KUAMUA KWANI HUWA IMEJIPANGA.

WITO KWA VIJANA PUNGUZENI MIHEMUKO
 
Tumeanza tena kusema Ccm?
Sio Mtu mmoja anaejua na kuweza kila kitu?
Ooh kumbe hayupo?So akili zimeanza kuwarudia????
uzuri wa CCM wapo flexible sana.kuna wakati itamtaja mtu na kuna wakati itataja Chama.hilo sio tatizo mkuu
 
Magufuli ndiye kaiua ccm lakini naamini kabisa kwa dhati ya moyo wangu Mama Samia Suluhu ataweka sawa upepo uliovuma kwa miaka mitano chini ya nduli Magufuli
 
utaratibu mpya wa CCM mpya kunyang'anya watu fikra ndio uliipa CCM nguvu...ilikuwa ni suala la muda pale fikra zikirudi au zikizaliwa fikra mpya...
 
Eheee sio CCM ya jpm?? yaani Jpm kaimarisha CCM ipi?? Amewahi kuwa hata mwenyekiti wa tawi la CCM??, Au namna ya ujengaje wa chama siku hizi nikuwanunua kina wapinzani.?? Wenye chama wanakitaka nyie CHAWA wa burigi mfuateni mwendazake.
 
Wapinzani wote walitoka CCM Hakuna upinzani nchi hii
 
Umeongea machacha ya miguu ya mnyonge hakuna lolote tulia sindano ziingie zamu yenu sasa
 
Ccm mtuletee makamo mwanamke nchi ina amani na utulivu mkubwa kwa sasa kuliko enzi zile za JPM na makonda tunaambiwa majukwaani nchi iko vitani adhabu ya msaliti ni kuuawa.
 
Ni wazi wapinzani wa CCM watatumia fursa zote halali na haramu ili kuimaliza CCM ikiwa madarakani na ni haki yao kufanya hivyo.

CCM ilipoteza mvuto kipindi flani hadi kufanya zoezi la kuvua gamba japo gamba liliishia kiunoni.

Mwaka 2015 CCM ilipitia changamoto nzito sana baada ya mgawanyiko mkubwa ambao kidogo utoe fursa kwa wapinzani.

Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alitokea au aliletwa kuokoa jahazi akiambatana na Rais Samia.
wawili hawa waliisimamia na kuitekeleza vyema ilani ya CCM na hatimaye 2020 upinzani ukapotezwa kabisa.

Ni bahati mbaya combination adimu ya Magufuli na Samia inapotea mwaka 2021 ghafla .

WITO:Kamwe tusikate tamaa au kuogopa au kuchonganishwa.

Wananchi wametekeleza nafasi yao yaani wamempa heshima Magufuli na CCM kwa kujitokeza na kuionesha dunia kuwa CCM ilikuwa sahihi kuwaleta wagombea Magufuli na Samia.
Ni mategemei ya wananchi wengi wanyonge na wapiga kura kuwa ilani ya CCM itatelelezwa hata kama mpendwa wao atakuwa ametangulia mbele ya haki.

Kipimo chao ni utekelezwaji wa Ilani ya CCM tena kwa kasi ile ile.
wananchi hao hawakuamini upinzani na propaganda au matakwa yao ya kibeberu bali walitaka zahanati na shule karibu yao,walitaka kufanya biashara zao ndogo ndogo bila bugudha,walitaka wasiwe sehemu ya mikopo ya chuma ulete inayofanywa na wafanyabiashara wanyonyaji,walisikitika kuona wanaojilimbikizia mali na kiwamwagia tope za V8VR barabarani,wslichukizwa na lugha za dharau za watoa huduma na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa,walikasirika kuona wakinyimwa kuwinda swaka halafu twiga wanapanda ndege,walichukia kuonwa kama wajinga.

toka mwaka 2010 walitaka kuiadhibu CCM Lakini baada ya 2015 wameiamini CCM kwa asilimia 98% .

sasa CCM inayo kazi ya kuwaaminisha kuwa bado CCM itaendelea kuwa CCM adilifu.
yote yanawezekana iwapo CCM itatulia kwanza kwa kuendelea na maombolezo ya kumpoteza jemedari Magufuli.

CCM HUWA HAINA HARAKA KATIKA KUAMUA KWANI HUWA IMEJIPANGA.

WITO KWA VIJANA PUNGUZENI MIHEMUKO
Hhahaa uzalendo uzalendo kumbe zilikuwa swaga ili muibe na kupora bila maswali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom