GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Leo kwa hasira Kali nilizonazo juu ya kinachoendelea huko Mkoani Pwani hasa eneo ' hatarishi ' kabisa la Kibiti sitoweza ' kutiririka ' na ' kuserereka ' kama kawaida yangu ila niseme tu bila kupepesa macho wala kutikisa masikio na kumung'unya maneno nawaomba hawa wafuatao ambao wana ' mamlaka ' na ' dhamana ' kwa Ulinzi na Usalama wa Watanzania wetu ama ' Wajiuzuru ' wenyewe haraka sana au basi aliyewateua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwani wameshaonyesha kiwango kikubwa sana na kisichovumilika mno cha ' Utendaji ' wao mbovu katika ' Nyadhifa ' zao.
Nao ni.....
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Mwigulu Lameck Nchemba
na
Inspekta Jenerali wa Police nchini Ernest Mangu
Tumewachoka na hatuna tena imani nanyi.
Nao ni.....
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Mwigulu Lameck Nchemba
na
Inspekta Jenerali wa Police nchini Ernest Mangu
Tumewachoka na hatuna tena imani nanyi.