Bila kitambulisho, hutopata huduma yoyote nchini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), imesema kuwa huduma nyingi kwa sasa zinategemea vitambulisho vya taifa na hayo yanafanyika ili kuongeza msukumo wa watu kufatilia vitambulisho hivyo.

Mdami.jpg

Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio msemaji wa NIDA, Rose Mdami amesema kuwa mamlaka hiyo inataka kila mtu mwenye umri wa miaka 18 awe na kitambulisho, kwani matumizi yataongezeka zaidi ya hapo.
"Mpaka sasa tumeshaandikisha wananchi milioni 19, na lengo tufike zaidi ya hapo na adhma yetu kila Mtanzania awe na kitambulisho cha taifa ili iwe rahisi kutambuana, lakini pia huduma nyingi za muhimu kwa sasa zinahitaji uwe na kitambulisho cha taifa," amesema Mdami.
Ameongeza kuwa, "Huwezi kuanzisha kampuni bila kitambulisho, huwezi kurudisha kadi ya simu iliyopotea, huwezi muwekea mtu dhamana na itafika mahali hutoweza kufanya chochote nchini kama huna kitambulisho".
Aidha amesema kuwa, suala la kuwa na kitambulisho cha taifa sio la hiari, ni lazima kwa mujibu wa sheria za nchi na havitolewi kwa wazawa tu, hata wageni na wakimbizi pia wanapatiwa ilimradi awe ameishi nchini zaidi ya miezi sita na amefikisha umri wa miaka 18.
 
Aliye-disign hivi vitambulisho alitukosea SANA waTanzania. Ni kitambulisho gani hakina sahihi? Juzi kati nimetakiwa kupeleka National ID somewhere nipewe huduma nyeti..kitambulisho kikakataliwa kwamba hakina sahihi yangu. Which is naturally logical!

I am very disappointed na hawa NIDA!
 
Acha uongo. Changu kina signature. Hata kwa wale walipata zamani hakuna sehemu nyeti kinapokataliwa labda kama ulitaka kujiunga na freemason
 
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), imesema kuwa huduma nyingi kwa sasa zinategemea vitambulisho vya taifa na hayo yanafanyika ili kuongeza msukumo wa watu kufatilia vitambulisho hivyo.

Mdami.jpg

Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio msemaji wa NIDA, Rose Mdami amesema kuwa mamlaka hiyo inataka kila mtu mwenye umri wa miaka 18 awe na kitambulisho, kwani matumizi yataongezeka zaidi ya hapo.
"Mpaka sasa tumeshaandikisha wananchi milioni 19, na lengo tufike zaidi ya hapo na adhma yetu kila Mtanzania awe na kitambulisho cha taifa ili iwe rahisi kutambuana, lakini pia huduma nyingi za muhimu kwa sasa zinahitaji uwe na kitambulisho cha taifa," amesema Mdami.
Ameongeza kuwa, "Huwezi kuanzisha kampuni bila kitambulisho, huwezi kurudisha kadi ya simu iliyopotea, huwezi muwekea mtu dhamana na itafika mahali hutoweza kufanya chochote nchini kama huna kitambulisho".
Aidha amesema kuwa, suala la kuwa na kitambulisho cha taifa sio la hiari, ni lazima kwa mujibu wa sheria za nchi na havitolewi kwa wazawa tu, hata wageni na wakimbizi pia wanapatiwa ilimradi awe ameishi nchini zaidi ya miezi sita na amefikisha umri wa miaka 18.
HIVI KAMA WANAKOPITA KUANDKISHA MNAPISHANA NAO YAANI UNAKUAUMEHAMA UFANYEJE ILI KUKIPATA HIKO KITAMBULISHO
 
Hivi vitambulisho kwa sasa vinapatikana wapi especially kwetu sisi wa mikoani nje ya dar????
 
Binafsi nijawahi kujua ama kuona umuhimu/ulazima wa mimi kwenda kupoteza muda wangu huko NIDAni, eti kwasababu nina haja na hicho kitambulika.
Hivi kwanza kazi ya kitambulisho ni nini hasa....[emoji30][emoji30][emoji30]
 
Hivyo vitambulisho wanatoa wapi?
Nime pigwa picha January 2018 hadi leo hakuna kitambulisho na haijulikani ni lini vita toka.. Kwanini sasa walipiga watu wengi kuliko uwezo wao wa kuvitoa? Issue sio kuorodhesha watu 19m issue ni kutoa huduma kwa ulio waorodhesha. Nachukia jizi siasa kwenye mambo ya msingi.
 
Aliye-disign hivi vitambulisho alitukosea SANA waTanzania. Ni kitambulisho gani hakina sahihi? Juzi kati nimetakiwa kupeleka National ID somewhere nipewe huduma nyeti..kitambulisho kikakataliwa kwamba hakina sahihi yangu. Which is naturally logical!

I am very disappointed na hawa NIDA!
Uliomba mwaka gani Mimi mbona sign ipo ya kwangu
 
Ni jambo jema kila Mwananchi kuwa na kitambulisho. Lakini, nadhani, suala siyo kuandikisha tu; Je NIDA wamekwisha chapisha na kutoa vitambalisho vingapi kati ya hao walioandikishwa. Kuna watu wameandikishwa takribani mwaka umepita sasa, hakuna taarifa ya kupata kitambulisho si jana leo wala kesho. NIDA, iliwafuata watu vijijini kuwaandikisha. Watu hao wanasubiri bado NIDA iwaletee vitambulisho hivyo. Lini vinatoka?
 
Huu sasa ubaguzi vitambulisho wanatoa kwa kujuana,watu tuna miezi 7sasa hatupewi hao NIDA waache ubabaishaji na urasimu
 
huku choma cha nkola walipita mwaka jana mwezi wa 5, lakini adi leo hakuna mwanakijiji yoyote aliyepata kitambulisho na wamenyamaza kimyaa
 
Maoni yangu "kw kuwa kutoa ID (kitambulisho) ni bure !!! hapo sasa !! umuhimu wake unakuwa SUBIRI, SUBIRINI, Mtuvumilie, Samahani kwa USUMBUFU, Njooni weeki ijayo, MTANDAO HAMNA, UMEME UMEKATA, MUDA UMEISHA..!!! nk nk nk
Jamani bora mututoze ELFU 20000/- au gharama maalumu LAKINI kazi na utoaaji ID uwe chapchap na UKWELI !!!
TUJENGE TAIFA na MUNGU aibariki TZ !!!
 
Kitambulisho cha uraia anapewa hadi mkimbizi? Anapewa hadi raia wa kigeni? Ama kweli naona mtu anataka awaingize ndugu zake toka uhutuni? Huwezi pewa national ID Kenya, Rwanda, Zimbabwe au popote pale kama wewe sio raia wa nchi husika
 
Back
Top Bottom