Bila JK hali ingekuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila JK hali ingekuwaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tiote, Mar 6, 2011.

 1. T

  Tiote Senior Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wandugu naomba mnivumilie lakini nina hoja ya kuijadili. Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kashfa na tuhuma mbali mbali dhidi ya viongozi wetu na hata wafanya biashara maarufu nchini wakihusishwa na tuhuma au shutuma mbalimbali za kukosa uadilifu na uhujumu uchumi. Kupitia taarifa hizi, wako ambao wamelazimika kuwajibika na wachache kufikishwa mahakamani. Kupitia taarifa hizi, tumeweza hata sisi kutoa michango yetu kupitia kwenye majukwaa mbalimbali likiwemo hili maarufu la JF. Lakini tumewahi kujiuliza uhuru huu wa kuhoji, kushutumu na kushambulia maovu umetokana na nini na umeanza lini.

  Kwa ufahamu wangu hli hii imejitokeza kwa upana huu tunaoufurahia baada ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani na ni matunda ya juhudi binafsi za JK. Katika awamu iliyopita haya yanayojitokeza leo yalikuwepo, tena kwa kiasi cha kutisha lakini tuliyajua kwa undani na ufasaha baada ya awamu hiyo kuondoka. Katika tawala za kidhalimu huko kwa wenzetu, uhuru huu kwa vyombo vya habari na watu binafsi ni ndoto na hata hapa tumeshuhudia watu wakiadhibiwa kiasi hata cha kunyang'anywa uraia kwa kusema kile walichoamini kwamba ni sahihi. Huko nje hali ni mbaya zaidi kwani wapo wanaopoteza maisha wakiusotoea uhuru huu. Hatutaki hilo litokee hapa na nina uhakika halitatokea maana kama ni kutokea lingeshatokea kwani uhuru huo umefikia hata kushambulia maisha binafsi ya rais na familia yake lakini mambo shwari tu.

  Mimi ninavyoamini hili ni matunda ya uvumilivu binafsi wa JK na ni vizuri katika hili tumpe sifa yake, maana kama inafikia kwamba hata mafisadi nao wanapata fursa ya kuongea wakati sasa hivi walitakiwa kuwa wameshalala kule segerea au ukonga, basi hakuna fursa kubwa kuliko hiyo. Waswahili wanasema ukimsifia baba yako kwamba anakimbia sana basi umsifie na yule aliyemkimbiza! Naomba kutoa hoja na samahani kwa wale watakaokwazika.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hii nimeikubali mkuu! Umezama na kutukumbusha kwamba hali hii haikujileta hivihivi na wala hatukumwaga damu kuipata kama wengine huko wanavyofanya. Wahenga wanasema samaki ndani ya maji hajui umuhimu wa maji, wimbi la ukombozi likimtoa ufukweni na kumrejesha bahari kina ndipo anapojua kwamba maisha bila maji kwake si lolote! Big up sana!
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,145
  Trophy Points: 280
  Big up Tiote.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Samahani kwa jibu langu hili: Bila ya Jk nadhani nchi ingekuwa na matumaini makubwa ya kuwapo kwa amani ya kudumu(siyo ya sasa inayopigiwa debe) maana viongozi wangewajibishwa vilivyo -- mafisadi wangepelekwa wanakostahili -- jela -- na nchi ingeokoa mapesa mengi yanayoibiwa hivo serikali kuweza kutoa huduma vizuri kwa wananchi.
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nchi ingekuwa imepiga hatua kubwa kimaendeleo
   
 6. S

  Salimia JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Well said......mnyonge mnyongeni....
   
 7. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa unayosema ila nina mashaka sana kuamini tusubirie utekelezaji wa ahadiiiiiiiiii
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Tuwakumbushe kuwa hata kumi ilianza na moja...
   
 9. b

  banyimwa Senior Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakati tunaendelea kusubiri "ahadi zitimie" kama ilivyosemwa hapo juu, ni vizuri tukakubali kwamba so far so good na hilo wala halina uhusianao na ahadi zake kwenye ilani ya uchaguzi. Hapa linalozungumziwa nadhani ni hatua tulizozifikia katika kufungua milango ya kutoa maoni bila woga au hofu ya kutiwa adabu. Hicho tunachokiona sasa middle east ni kupigania mambo kadhaa likiwemo hilo la uhuru wa kujieleza ambao huku uko bwerere. Tukiweza kuutumia responsibly basi tutaendelea kuufaidi kwa muda wote wa utawala wake. Lakini du! tunavyomtia vidole machoni!
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nadhani hata elimu ingekua bora,kwa sasa c unaiona elimu ye2?
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba kuna watu wana-enjoy uhuru ambao hauwastahili kutokana na matendo yao kwa wana wa nchi hii. Lakini hili ni tatizo la karibu nchi zote za kusini mwa jangwa la sahara - kupambana na mnyama anayeitwa impunity ni suala ambalo bado halijawekwa kwenye sehemu inayostahili na hili ni changamoto pia kwa JK, lakini hilo ni somo kwa siku nyingine. Kwa leo lililo wazi ni kwamba score card ya mkubwa huyu kwenye kufungua democratic space na kutufanya tujisikie tuke kwenye taifa huru, iko juu. A pat on the back mkuu!
   
 12. A

  Abba Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani mnasahau jinsi said kubenea na Tegambwage walivyomwagiwa acid? je mnakumbuka gazeti la dar leo lilivyofungiwa?,je mmesahau Mkuchika alivyokuwa anayatishia magazeti mwaka 2009 kuelekea uchaguzi mkuu?JK hajahusika katika kupanua uhuru wa kujieleza na kutoa maoni kwa maana ya nia thabiti ila ni kwa sababu amekuwa rais dhaifu tangia taifa hili lipate uhuru! Sasa amekuwa muumini wa kutumia nguvu ya fedha na dola kunyamazishi sauti na mawazo tofauti-Juzi juzi gazeti la raiamwema lilizuiliwa kuchapishwa coz limemuandika swahiba wake! JK ni incompetent na inakata moyo wa mwenda wazimu kumnadi. THINK AGAINB
   
 13. A

  Abba Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani mnasahau jinsi said kubenea na Tegambwage walivyomwagiwa acid? je mnakumbuka gazeti la dar leo lilivyofungiwa?,je mmesahau Mkuchika alivyokuwa anayatishia magazeti mwaka 2009 kuelekea uchaguzi mkuu?JK hajahusika katika kupanua uhuru wa kujieleza na kutoa maoni kwa maana ya nia thabiti ila ni kwa sababu amekuwa rais dhaifu tangia taifa hili lipate uhuru! Sasa amekuwa muumini wa kutumia nguvu ya fedha na dola kunyamazishi sauti na mawazo tofauti-Juzi juzi gazeti la raiamwema lilizuiliwa kuchapishwa coz limemuandika swahiba wake! JK ni incompetent na inakata moyo wa mwenda wazimu kumnadi. THINK AGAIN!
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Me kwa mtazamo wangu huwezi tofautisha rangi ya tui na maziwa bila J.K ni sisiM tu ingekuwepo so hali ingekuwa hivi hivi yaani ovyo ovyo tu sababu sisiM hakuna aliebakia mwerevu ukitaka kufahamu ukweli sikia kauri zao mmoja mmoja au jaribu kuomba wazo la mwana SisiM Yeyote umuulize nchi inapoelekea ni pabaya usikie majibu yake unaweza kulia kama pinda utawajua mbu hawa wana mawazo mgando hata angekuwepo baba wa taifa angewaambia kuwa mnaipeleka nchi pabaya wangemwambia mzee unazeeka vibaya kumbuka umetokea wapi.. au kama kuna yeyote atuambie ccm kuna hata mwenye uwezo wa kuona mbali na nia haswa ya kuwaletea watanganyika maisha bora ya vitendo halisi... ajitokeze pls
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mimi nawashangaa wale wote wanaompa Kikwete sifa za kufungua nafasi ya demokrasia. Hiyo nafasi Kikwete aliikuta. Angalia jinsi alivyoyatumia magazeti kujipandisha chati na kuwaharibia wote wale aliofikiria kuwa ni maadui/washindani wake. Mtu kama huyu asingeweza kugeuka na kuanza kufuta nafasi aliyoikuta na ambayo ameitumia kwa manufaa.
   
Loading...