Kuna historia zinasema kaburi lake lipo, pia kwa Mary Magdalene na Elizabeth.
Siyo kweli hata kidogo. Kuondoka kwa Bikira Maria Duniani ni habari iliyoelezwa kwa kina na kwa uwazi na Mtume Yohana kama andiko linalojitegemea ambalo siyo sehemu ya Biblia.
Mama Bikira Maria kuondoka kwake Duniani kuliambatana na miujiza mingi kwa kipindi cha wiki nzima. Nikisema nielezee tukio zima, sijui kama inawezekana kwa kuandika hapa jukwaani, labda ikibidi niweke kama kiambtanisho cha tukio zima.
Kwa ufupisana, niseme tu kuwa Bikira Maria aliondoka Duniani kwa njia ya muujiza mkubwa. Kufuatana na andiko la Mtume Yohana, ni kwamba siku ile walikuja mitume wote wa Yesu, waliokuwa hai na wale ambao tayari walikuwa wamekufa, na kila mtume aliletwa kwa njia ya muujiza. Na hiyo inatajwa kuwa lilikuwa niombi la Bikira Maria kwa Kristo kuwa kabla ya kuondoka anataka aagane na mitume wote waliokuwa hai na wale ambao walikuwa tayari wamekwishakufa. Kutokana na miujiza iliyokuwa ya mfululizo kwa wiki zima, Kuhani mkuu aliamuru kuwa Bikira Maria akifa, mwili wake uchukuliwe ili ukachomwe moto, ili watu wasiwe wanaenda kuabudu kwenye kaburi lake. Lakini siku ile, akiwa ameambiwa na malaika kuwa siku zake za kuishi Duniani zimekwisha, na ombi lake la kutaka kuondoka Duniani, na la kutaka Bwana Yesu aje kumchukua likiwa limepokelewa, akiwa amelala kwenye meza, aliijiwa na mwanawe Bwana wetu Yesu Kristo, akiwa na malaika, kama alivyokuwa ameomba. Bikira Maria kufuatia miujiza iliyotendeka kwa wiki zima tangu aambiwe kuwa ataondoka Duniani, aliomba tena kuwa ikimpendeza, anaomba, yeyote atakayeomba kwa jina lake, ombi lake lisikiIizwe, naye Yesu akamjibu akamwambia, 'hakika atakayeomba kwa jina langu na kwa jina lako, ombi lake litasikilizwa. Kisha Kristo alinyosha mkono wake kumwelekea mama yake, na mara kikatoka kitu katika kinywa chake, akakikabidhi kwa malaika, kisha Yesu na Malaika hawakuonekana tena, ikawa roho imeondoka, bali mwili ukabakia mezani. Mitume wakauchukua mwili kwa nia ya kwenda kuuzika, lakini askari wa kuhani akawapiga mikono, kutaka kuunyang'anya ili aupeleke kwa kuhani kama alivyoagizwa. Alipojaribu kuwapiga mikono walioubeba mwili, yeye askari akapoza pale pale akaanza kulia na kuomba aombewe na mitume wa Yesu. Mitume wakapiga magoti, wakaomba asamehewe arudishiwe mikono yake. Yule askari akapona, kisha akaomba kubatizwa. Wakambatiza, kisha wakauchukua mwili kuupeleka eneo walilotaka kumzika, lakini muda wote malaika wakaja, muda wote walikuwa wakiimba, na eneo lote likajawa na harufu nzuri, watu wakabakia wameuzunguka mwili. Siku ya tatu, wakiwa bado wameuzunguka, mwili ukapotea machoni pao, na malaika wakaondoka. Hivyo ndivyo Bikira Maria alivyopaa mbinguni, kwa kadiri ya andiko la Mtume Yohana, 'Ushuhuda wa Jinsi Mama wa Bwana wetu Alivyoondoka Duniani'. Hapa nimefupisha sana.