Big up ! Simu 2000 bus stand

kimatire

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2008
Posts
371
Reaction score
94
Mambo mazuri hatuna budi kuyaona na kuyasifia, Kituo kidogo cha daladala simu 2000 kimenithibitishia kwamba tunaweza tukiamua. Ni kituo kisafi chenye mpangilio na salama.Nawapongeza wasimamizi ambao nina uhakika ni Manispaa ya Kinondoni.Ila najiuliza huko kwingine wameshindwa nini?TUBADILIKE, Mambo mazuri yatatujengea tabia nzuri pia!

Last edited by a moderator:
hongera zao.....hivi hilo jina la simu 2000 limepatikanaje?
 
Ila vumbi na tope wakati wa mvua katika njia ya kuingilia pale ndio kero.
 
Pale wangepiga lami njia ya kwenda stand mambo yangekuwa poa sana
 
Tupieni photos kwa sisi tulio mbali tukione

Huwa mnadai...oooh,dar kuna nini,kwani lazima kuja dar,afu mnakuwa wa kwanza kuomba picha za maeneo na vitu mbalimbali hapa daslam..ili na ninyi japo msafishe macho na kulijuw jiji thru pics...kudos wakuu..#team mikoani
 
hongera zao.....hivi hilo jina la simu 2000 limepatikanaje?

Jina simu 2000 lilitokana na eneo hilo lilikuwa mali ya Posta na Simu Baada ya kugawanywa Simu kuwa TTCL na Posta kubakia peke yake , Ndipo iliundwa Kampuni ya kusimamia na kuuza mali zilizokuwa za Shirika la Posta na Simu likaitwa Simu 2000.Hivyo kiwanja hicho kikawa mikononi mwa Simu 2000.Baada ya wadau mbali mbali kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa walipoamua kukihamisha kituo kidogo cha Ubungo kukipeleka pale na kukipa jina la Simu 2000.Manispaa walisimamia ujenzi na uendeshaji.Ni chanzo kizuri sana cha mapato pia kuna kituo cha polisi na vyoo/mabafu ya kulipia.
 
okey...shukrani
 
sawa mkuu vipi kuhusu picha au tumsubiri Tyta
 
Last edited by a moderator:
Huwa mnadai...oooh,dar kuna nini,kwani lazima kuja dar,afu mnakuwa wa kwanza kuomba picha za maeneo na vitu mbalimbali hapa daslam..ili na ninyi japo msafishe macho na kulijuw jiji thru pics...kudos wakuu..#team mikoani

Do you think everyone ambae anakaa Dar lazima afike simu 2000? Kutopajua Hapo haijalishi Tuoie mkoa, Wengine hata nauli za daladala tushasahau n sh ngapi
 
PIa kuna huduma ya internet bure... (Wireless Free), Nadhani ndo kituo cha kwanza cha DALADALA Tanzania kuwa na huduma ya bure ya internet.
 
kazi nzuri wamekipanga vizuri sana hata mgeni hapotei maana kuna majina ya route kabisa...ila kituo kipya cha kilombero(arusha) ndo hovyo kabisa
 
Kituo kizuri sema hilo jina bwana limekaa kushoto sana, eti simu 2000 ndio nini sasa?! how comes?? haliji kabisa,
 
Bado sijajua sababu ya hiyo kampuni kuita eneo hilo SIMU 2000.
 
Kituo kizuri sema hilo jina bwana limekaa kushoto sana, eti simu 2000 ndio nini sasa?! how comes?? haliji kabisa,
Inawezekana kuna jamaa mwenye sauti kwenye kampuni alikuwa Bar ameshapendeza kichwani akapewa nafasi ya kupendekeza jina akafyatuka na hilo. Katika majina yoooote mabaya ambayo hayaeleweki hili linaweza kuwa linaongoza DSM.
 
kazi nzuri wamekipanga vizuri sana hata mgeni hapotei maana kuna majina ya route kabisa...ila kituo kipya cha kilombero(arusha) ndo hovyo kabisa
mkuu naona mahesabu yalikuchanganya? naishangaa user id yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…